Waziri mkuu Mwigulu Nchemba, tusaidie kuzuia huu wizi

Gagnija

Platinum Member
Joined
Apr 28, 2006
Posts
13,388
Reaction score
13,793
Naandika haya nikiamini utayasoma kwakuwa wewe ni mmoja wa wanajukwaa JF

Sasa hivi nchini kuna makampuni mengi yanayoagiza mali zilizokwisha tumika toka nje.

Ni jambo zuri sana kwani huwawezesha wenye kipato kidogo wasioweza kumudu kununua baadhi ya vitu vipya, kununua hivi vya mitumba (used).

Tatizo linakuja kwa baadhi ya waagizaji kumtaka mnunuzi kulipia mali ikiwa bado nje ya nchi ndipo iweze kupakiwa kwenye container.

Baadhi ya wanunuzi wamejikuta wakiletewa mali ambazo ni damaged beyond repair, hivyo kupata hasara kwakuwa wauzaji hawakubali kurudisha pesa

Huduma nzuri imegeuzwa wizi, serikali itusaidie kukomesha wizi huu kwa kuwataka waagizaji kufuata utaratibu unaokubalika wa mtu kulipia mali baada ya kujiridhisha na ubora wa kitu anacholipia. Hii itasaidia pia kuzuia kuligeuza taifa kuwa dumping ground.
 
Wafanyabiashara wengi sio waaminifu Kabisa. Haswa hawa wenye fujo fujo sana mtandaoni .. umakini ni muhimu sana watu wanalizwa sana kweli.
Hivi nikuulize inakuwaje unaagiza mzigo kwa mtu ambaye hujui uaminifu wake kisha unapatana naye mnamalizana kila kitu kisha baadae anakuletea mzigo mbovu halafu unaomba serikali ije kukusaidia kwenye ishu ya maelewano baina ya watu wawili?
Ni kitu gani au alama gani ilikuaminisha kuwa huyo mtu ana uwezo wa kudeliver vitu kwenye ubora unaoutaka?
Kwenye suala la umakini hapa Watanzania huwa tunafeli sana tunapenda kufanya vitu na kuamua kwa mihemko
 
Utapeli wa namna hiyo hata serikali ni ngumu kuuzuia maana hawa watu wanapatana kinyemela, wanalipana kinyemela. Akipigwa tukio ndio anajitokeza bila vielelezo zaidi ya maneno.
 
Upo sahihi sana. Ndio maana post ya mwanzo kwenye huu uzii nimeandika "Caveat Emptor" ila pamoja na hiyo siyo sababu ya kuwaumiza wateja masikini.

Wengi wanajikusanya kununua vitu used kwa sababu hawana uwezo wa kununua brand new... Sasa isiwe sababu ya kuwaumiza kwa kuwauzia vitu ambavyo vimekwisha kabisa matumizi yake. Na ukijua kwenye used hakunaga warranty Wala guarantee.
 
Matapeli hawana muda huo wa kuwaza wanachowaza wao pesa iingie tu mfukoni kwao watoto waende maliwato
 
Utapeli wa namna hiyo hata serikali ni ngumu kuuzuia maana hawa watu wanapatana kinyemela, wanalipana kinyemela. Akipigwa tukio ndio anajitokeza bila vielelezo zaidi ya maneno.
Hakuna pesa inayolipwa bila vielelezo.

Serikali haiwezi kushindwa kuzuia utapeli huu, labda kama utashi hautakuwepo.
 
Mkuu mpeleke kwenye vyombo vya sheria upate haki yako!!.

Nasema hamna vielelezo maana wanaotapeliwa wengi hulipa bila kuhifadhi risiti, wanalipa kupitia mawakala wa mitandao ya simu nk.

Cha kwanza kabisa ni elimu kwenu watapeliwa, vipi wale wa "tuma kwa namba hii" wapo au hawapo??
Serikali haijafanya juhudi kuwakamata na kuwadhibiti? Lakini si bado wapo.

Mpaka mitandao ya simu imeendelea kutoa elimu, kuwasanua watu ila wewe ukitaka serikali ikusaidie kwenye hilo utafeli mkuu.
 
Back
Top Bottom