Waandishi wa Habari wa nchi hii hakuna mtu wa kuhoji maswali mazito na yenye udadisi wa kina kiasi cha kumfanya muhusika ajiulize mara mbili mbili kabla ya kujibu,mifano ipo mingi tu,Lowasa wakati anasaka wadhamini wa kumpeleka ikulu pale Arusha aliongea maneno mazuri mno ya kumpamba Mh JK na serikali yake ktk kuleta maendeleo ya wananchi,lkn siku chache baada ya mipango yake Kukwama alimponda sana pamoja na sera zake zote kiasi kwamba ameifanya nchi na watu wake kuwa masikini wa kutupwa,sasa ktk mazingira hayo Waandishi walipaswa kuuliza maswali mengi magumu,ni vipi awe double standard kwa muda mfupi,ni yapi maendeleo aliyowapa wananchi wa Jimbo lake kwa miaka yote ya kuwawakilisha Bungeni,wapi ilikoishia mvua ya Kutengenezwa na Wathailand ili kuondoa ukame kipindi hicho kabla ya kuletwa mzimu wa Richmond nk.Mfano mwingine mgombea kwa nia ya kusaka umaarufu anakusanya maelfu ya watu kuandamana kwenda kuvamia kituo cha polisi kwa nia ya kumtoa mahabusu aliyejeruhi watu hadi kulazwa kwa vile ni kiongozi kwa nafasi fulani,jee ni nani yuko juu ya sheria za nchi kwamba akitenda kosa hapaswi kukamatwa!polisi ktk kutimiza wajibu wao wanavunja maandamano au jaribio hilo mgombea kiti cha Ubunge anakamatwa na kufikishwa mahakamani,akiteremka kizimbani anaita Waandishi wa Habari kwenda kusikiliza akichowaambia na kukiripoti vivyo hivyo kwenye vyombo vyao vya habari bila hata kuuliza maswali ya msingi,Chanzo cha yeye kukamatwa ni nini,Lini na Wapi,Kilitokea kitu gani,Nani alisababisha,Sheria zinasemaje once mtu akitenda kosa, Jee huyo aliyekamatwa ana kinga ya kisheria,Jee wapi imeandikwa kwamba wkt wa kampeni za kisiasa mtu anaruhusiwa kuvunja sheria au kutenda kosa la Jinai,Jee mtu akikamatwa taratibu zikoje hadi kudhaminiwa au ni lazima akatolewe kwa nguvu?,Jee yakitokea madhara kwa watu wasiohusika nani atawajibika kwa hilo?maswali kwa uchache kama haya anapaswa kuulizwa huyo aliyewaita,lkn kwa kuwa Waandishi wengi wanategemea kupokea chochote kunakuwa na mapokeo mabaya mno kwa wale wanaolishwa hizo habari.Rai yangu kwa Waandishi wa Habari kabla ya kwenda kupokea walichoitiwa watafute habari za Upande wa pili na kuhoji mambo kadhaa,Alichokiandika mmiliki wa gazeti la Mwana Halisi,Mawio kwa miaka minane dhidi ya Ufisadi wa Edward Lowasa na anayoyafanya leo kwa mtu huyo huyo ni sawa na Hadithi za Hekaya za Abunuas,mchana mwema.