Waziri mkuu msataafu atembelea shule ya Secondary ya Ann's

Lowassa ni Waziri Mkuu wa ZAMANI na wala si waziri mkuu mstaafu. Hicho ndicho Kiswahili fasaha hata kama mnataka kumpamba.
 
Tahadhari! isije ikawa anafikiri kwamba Dr, Slaa ana mvuto kwa wananchi kwa sababu ya ukatoliki?? laa hasha ni kwa sababu anachokipigania ni kwa maslahi ya wanyonge. Hata rais wetu ambaye awali iliaminika kuwa alikuwa chaguo la mungu kwa wa TZ amepoteza mvuto kabisa baada ya kuruhusu mafisadi kupora raslimali za wapiga kura wanyonge kujitajirisha kupindukia huku wananchi wakitaabika kwa mgao wa umeme, migomo ya madhaktari na mifadhaiko ya moyo inayotokana na Rais kuwafumbia macho wahalifu wenye ushaidi wa wazi mfano waliorudisha fedha za epa na mzee wa vijicent ambaye fedha za rada zilizoibiwa kwa mkataba wa kifisadi aliosaini wakiwa wanatanua kule maisha club bila wasiwasi wowote badala ya kuwa gerezani.
Ushauri wangu: Kama anataka kuingia pale ikulu ambapo ni mahali patakatifu basi na achukue mali zake zote zote na azigawe kwa maskini na wahitaji wengine baada ya hapo awarudie wapiga kura aandamane nao mpaka ikulu na hakuna atakaye weza kumzuia hata kwa vifaru.
 
Back
Top Bottom