Wakuu zangu,
Mtanisamehe lakini Bongo hakuna madaktari ila balaa tupu. Watu wamesoma lakini hawakuelemika na nasema hivi kwa sababu bado Bongo upasiuaji wa mimba wanafanya toka kitovuni kushuka, utaalam ambao hautumiki tena ila tumbo linapasuliwa toka kushoto au kulia kwenda kulia au kushoto. Vifo vya kina mama ktk uzazi vinazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. wanawake wanapewa dawa za kuzuia Mimba pasipo kupimwa damu kujua dawa gani inalingana na mtumiaji, tena basi wengine huchomwa sindano wasipate hedhi kwa miezi mitatu hadi minne.. Jamani huu mwili wa mwanamke unatakiwa kujisafisha kilamwezi sasa mtu asipopata damu kwa miezi minne mnategemea nini. Hawa ndio madaktari wetu, wanatisha jamani wala sii kidogo unakwenda Hospital huku umeacha usia kabisa.
mwisho majuzi tu mdogo wangu alipewa Operation ya Apendix akaandikiwa kutolewa nyuzi baada ya siku 10 nikabisha na kusema huo ni muda mrefu sana.. daktari akanambia leo wewe umekuwa daktari?..sikujibu kitu tukaondoka..Baada ya siku 10 tukarudi nyuzi zikashindikana kutoka kwa sababu tayari zilikwisha shikana na mwili..Hivyo tukarudi nyumbani akambiwa avumilie hivyo hiyvo hadi nyuzi zitakapo toka zenyewe. Yale yale ya Daktari mkuu wa upasuaji Muhimbili kufanya upasuaji wa kichwa mgonjwa wa mguu..
Yaani inatakiwa moyo sana kutibiwa Tanzania leo ndio maana watu wanakwenda tibiwa India au Maleysia, sio sababu ya gharama tu ila uhakika wa kupona kama ilivyokuwa Elimu yetu wakati fulani wazazi wengi walipeleka watoto wao kusoma Kenya na Uganda. Sababu kubwa ilikuwa shule zetu zilitoa Elimu mbaya. Haya ktk mageuzi ya Ufundishaji badala ya kuboresha Elimu ya shule zetu kwa kufuata misnigi yake tumechagua kiingereza kuwa lugha ya kufundishia kuwa ndio kuboresha elimu ya watoto - Matokeo yake more failures toka std 7 hadi Secondary..Hivyo sintaona ajabu kila mzazi akitaka mtoto wake azaliwe nje ya Tanzania kwa sababu pamoja na mikakati yote matatizo ya huduma za Afya na Elimu yanazidi badala ya kupungua.