Waziri mkuu mizengo pinda ni mtoto wa mkulima kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri mkuu mizengo pinda ni mtoto wa mkulima kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rumenyela, May 20, 2010.

 1. r

  rumenyela Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanajii,
  Tumekuwa tukumsikia waziri wetu Mkuu Mhesimiwa Mizengo Pinda akijiita kuwa yeye ni mtoto wa mkulima na hivyo anapinga vitu kadhaa ambavyo vinaongeza matumizi yasiyo ya lazima ya pesa za umma. Kwa mfano aliwahi kuhoji juu ya ununuzi wa magari ya kifahari kwa watendaji waandamizi wa serikali yetu.

  Jana nimesikia na kuona kwenye TV waziri huyo akienda UINGEREZA kufanya uchunguzi wa afya "wa kawaida" Inamaana hapa Nchini hakuna wataalamu /madaktari wanaoweza kufanya kazi hiyo? Ukizingatia kuwa yeye ni mtoto wa mlalahoi kama sisi?
  Je, haya si matumizi mabaya ya pesa za Watanzania? Naombeni maoni yenu juu ya hili.

  Rumenyela
  KIGOMA.
   
 2. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Huenda ameshauriwa na madaktari wake!
   
 3. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  haya mkuu ndio matumizi mabaya ya pesa za serikali...huyu muheshimiwa alisikika akizuia ununuzi wa mashangingi na semina za viongozi akisema ni matumizi ya anasa..sasa je yeye haoni kama ni anasa kwenda uingereza kucheck afya yake wakati tunao wataalamu wa kutosha hapa nchini kwetu?...na hata kama hatuna wataalamu wa kutosha je sio busara kuajiri wataalamu hao na kununua vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa afya ili hata keshokutwa kiongozi mwingine asiende ulaya kupima afya?...

  KWA HILI MZEE MIZENGO PITA KAYAANZA PINDA...UNATAKIWA UTUOMBE RADHI WAZEE WAKO KAMA KWELI WEWE NI MTOTO WA MKULIMA TENA SIE BABA ZAKO WA JEMBE LA MKONO....UMEANZA KUBADILIKA NA KULETA UTOZI PLUS MASHAUZI YASOKUWA YA MSINGI...TUOMBE RADHI WAKULIMA WOTE MAANA SIE TUKISIKIA TUMBO LINAZINGUA HUWA TUNATUMIA MIZIZI TULIYOICHIMBA SHAMBANI WAKATI WA KULIMA..NA HATA TUSIPOPONA HUWA TUNAHISI KULOGWA NA TUNAENDA KWA BABU KUTUSOMEA NYOTA...

  SASA WEWE UNALETA UTOZI KWENDA KUSOMA NYOTA KWA WAZUNGU..."MATUPINKELE"...MAJITU YENYE MATUMBO MEUPE......tutake radhi tafadhali
   
 4. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni kawaida kwa viongozi wa Afrika kutibiwa Ulaya, si hapa kwetu tu. Wenzetu wametuacha kwa huduma bora za utabibu kulinganisha na hapa ingawa wataalamu tunao. Hivyo sishangai Mhe. Pinda kuelekea kuangaliwa afya yake huko kwa kuwa ni utaratibu wa serikali yetu (hata kama yeye hapendi) kupeleka viongozi wakuu wa nchi kupata tiba bora zaidi au kuangaliwa afya zao nje pale ulazima unapokuwepo.
   
 5. N

  Nginana JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 775
  Likes Received: 636
  Trophy Points: 180
  Indeed, Pinda's assertion that he is ‘the son of a peasant' and thus he abhors extravagance is a pure political gimmick (danganya toto). Now he has shown his true colours! Take my word: like Mkapa, Pinda will leave office tight-lipped about the assets that he will have accumulated (while in office) as PM . After all, "Birds of the same feather flock together".
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Walau mtoto wa mkulima atampiku Muungwana kukutana na waziri mkuu mwenzake mpya wa UK.....David Cameroun!
   
 7. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pinda hata msimsikilize jamaa ni mwana siasa kupindukia, kuna siku alikuwa anasema anawashangaa watu wanaovaa suti badala ya kuvaa mashati ya batiki tena dar ni joto wakati yeye anatinga suti pia, kuna siku tena kasema anawashangaa watumishi wanaotumia mashangingi wakati misafara yake mashangingi kibao. Mlimpoteza lowasa hakuna tena cha waziri mkuu wala nini, zinmebaki politic tu
   
 8. T

  Tom JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pia ni kawaida kwa viongozi wa kiafrika kua mafisadi, hivyo Pinda kwenda huko Uingeereza ni ufisadi wa kawaida tu.

  Mabaya wayafanyao viongozi wa Afrika si halali kwa kiongozi wa Tanzania kuyafanya la sivyo TZ itaendelea kua maskini kama nchi za Kiafrika zingine. Matibabu ya hapa kwetu yanafaa kabisa na Pinda akua ni mfano tosha kwa raia akipimwa afya hapa. Lakini CCM wameshajenga mizizi mibaya kweli kwelil maana hata daktari atayeshauri Pinda aende Ulaya anajua naye ana posho yake kwa kutoa ushauri huo ama kuandamana naye huko Ulaya.
   
 9. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Jamani "general checkup" haihitaji mtu kwenda ULAYA!!!
  For God's sake "uchunguzi wa afya wa kawaida unaenda ulaya!! Kama basi ni kutaka viwango kuna hii hospitali hapa nyuma ya seacliff ukiingia ova umeingia vyumba vya hilton hotels na ina manesi wote toka india. Jina limenitoka sasa hivi. Unataka kuniambia yenyewe haina hadhi ya kufanya general checkup ya waziri hata raisi!!!???
  Kwani miili yao ina mabadiliko yoyote na ya kwetu kutokana na hivyo vyeo walivyonavyo???
  If it was brain surgery, liver surgery, heart surgery SAWA lakini GENERAL BODY CHECKUP!!!
   
 10. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Msikimbilie kulaumu.Kwanza inawezekana alichokwendea Pinda ni zaidi ya huo uchunguzi wanaousema.Viongozi wengi wa Afrika wana magonjwa chronic na life threatening na wananchi kamwe hamuwezi kuambiwa.Hata wakienda nje kwa sababu hiyo,media ita cover kuwa ni normal screening tests wakati ukweli wake unaweza kuwa ni kwenda kwa a delicate medical intervention inayohitaji siyo tu uangalizi wa hali ya juu bali pia madaktari makini na waliobobea na vifaa vya kisasa kwa kazi hiyo.
  Pili:Kuishi kwa dhiki/umaskini hakumfanyi kiongozi kuwa kiongozi bora.Pinda kama PM na kiongozi wa muda mrefu serikalini,naamini ana uwezo kabisa (kwa kipato chake halali) kwenda UK kuangalia afya yake.Si kwa Pinda tu,hata raia mwenye uwezo wake na afanye hivyo.Kwanini kuingia hofu na wasiwasi na tiba isiyokuwa na uhakika wakati mfuko unakuruhusu?Na hata hizo hospitali za kibongo zikiboreshwa,amini nawaambia bado watakuwepo watakaokwenda nje kutibiwa.Katika utabibu sisi bado tunabahatishabahatisha tu kuanzia utendaji wenyewe mpaka kwenye maadili ya taaluma.
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  May 20, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu zangu,
  Mtanisamehe lakini Bongo hakuna madaktari ila balaa tupu. Watu wamesoma lakini hawakuelemika na nasema hivi kwa sababu bado Bongo upasiuaji wa mimba wanafanya toka kitovuni kushuka, utaalam ambao hautumiki tena ila tumbo linapasuliwa toka kushoto au kulia kwenda kulia au kushoto. Vifo vya kina mama ktk uzazi vinazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. wanawake wanapewa dawa za kuzuia Mimba pasipo kupimwa damu kujua dawa gani inalingana na mtumiaji, tena basi wengine huchomwa sindano wasipate hedhi kwa miezi mitatu hadi minne.. Jamani huu mwili wa mwanamke unatakiwa kujisafisha kilamwezi sasa mtu asipopata damu kwa miezi minne mnategemea nini. Hawa ndio madaktari wetu, wanatisha jamani wala sii kidogo unakwenda Hospital huku umeacha usia kabisa.

  mwisho majuzi tu mdogo wangu alipewa Operation ya Apendix akaandikiwa kutolewa nyuzi baada ya siku 10 nikabisha na kusema huo ni muda mrefu sana.. daktari akanambia leo wewe umekuwa daktari?..sikujibu kitu tukaondoka..Baada ya siku 10 tukarudi nyuzi zikashindikana kutoka kwa sababu tayari zilikwisha shikana na mwili..Hivyo tukarudi nyumbani akambiwa avumilie hivyo hiyvo hadi nyuzi zitakapo toka zenyewe. Yale yale ya Daktari mkuu wa upasuaji Muhimbili kufanya upasuaji wa kichwa mgonjwa wa mguu..

  Yaani inatakiwa moyo sana kutibiwa Tanzania leo ndio maana watu wanakwenda tibiwa India au Maleysia, sio sababu ya gharama tu ila uhakika wa kupona kama ilivyokuwa Elimu yetu wakati fulani wazazi wengi walipeleka watoto wao kusoma Kenya na Uganda. Sababu kubwa ilikuwa shule zetu zilitoa Elimu mbaya. Haya ktk mageuzi ya Ufundishaji badala ya kuboresha Elimu ya shule zetu kwa kufuata misnigi yake tumechagua kiingereza kuwa lugha ya kufundishia kuwa ndio kuboresha elimu ya watoto - Matokeo yake more failures toka std 7 hadi Secondary..Hivyo sintaona ajabu kila mzazi akitaka mtoto wake azaliwe nje ya Tanzania kwa sababu pamoja na mikakati yote matatizo ya huduma za Afya na Elimu yanazidi badala ya kupungua.
   
 12. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Mkandara nashangaa mpaka leo Muhimbili wanapasua tumbo kwa kutoa appendix.Kama ungekuwa na pesa kidogo ungechanga aende Hindul Mandal ,nafikiri wanafanya key hole surgery,hakuna ya kupasua mtu.Hii ni ya kizamani,ambayo inaacha kovu la maisha.Hii incision ya kwenye tumbo inadumu kama dakika 20-30.
  Labda naanza kuona hata wakuu wetu hawaamini hawa madr Muhimbili.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  May 21, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh! Shukran lakini ndio imeshakua, ndio Bongo yetu hiyo mkuu wangu inatisha wala sii kidogo ukiumwa homa na mafua lazima sindano ya ****. Wanapenda kuchoma masindano hao utadhani tupo mwaka 1956..Kisa kingine Dada yake na JK nadhani kwa baba mwingine akiishi Ukonga alipata ajali akaletwa Muhimbili ilikuwa visa vitupu, hadi JK mwenyewe alipotokea ndipo bibie akapewa huduma..
  Mwacheni mtoto wa mkulima akatibiwe UK..Bongo imekwisha haribika sana wanaweza mwekea sumu asiamke- Uchaguzi ndio huu watu wana roho mbaya kushinda maelezo...
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ana jiita "mtoto wa mkulima" na siyo "mkulima". Baba alikua mkulima ila siyo yeye. Kwani leo hii tajiri ambae amekulia kijijini haweza kusema ni "mtoto wa mkulima" meaning baba ake alikua mkulima? Katoa tungo tata kawaachia kila mtu atafsiri kama anavyo taka.
   
 15. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hili sina uhakika nalo na ninadhani hupo sahihi. Suala la namna ya kupasua linategemea daktari atakavyoona kutokana na mtu anayepasuliwa. Mke wangu alipasuliwa bongo (hospitali ya mission) kwa njia hiyo ya kushoto/kulia kwenda kulia/kushoto wakati huo huo mke wa rafiki yangu alipasuliwa nje ya nchi (China) katika hospitali yenye hadhi ya kimataifa, walimpasua toka kitovuni kushuka chini. Labda madaktari watueleze hapa.

  Kuhusu madaktari kutoelimika nalo ninawasiwasi nalo. Ukienda nchi mbalimbali kuna madaktari wabongo na wanafanya kazi nzuri sana. Kuna siku nilikuwa nimeenda kutibiwa hospitali moja (Asia Pacific) nikawa napiga story na daktari, alipojua kuwa natoka Tz akanieleza kuwa alifika TZ kwenye program maalumu ya mafunzo (exchange program) actually aliwasifia madaktari wa kibongo, ila alilaumu suala la vifaa duni.

  Tukubaliane kwamba matibabu hapa kwetu Tz gharama zake ni rahisi sana, ni vigumu kwa hospitali kumudu vifaa bora na dawa nzuri. Kuna haja ya kuangalia upya mfumo mzima wa huduma za afya. Serikali inaweza kuweka mpango wa kutoa bima za afya kwa wananchi wote then gharama zikawekwa kulingana na matibabu. Kwasasa haiwezekani kupandisha gharama kwakuwa watu enye bima za afya ni wachache sana. Bila bima ya afya ni vigumu kumudu matibabu ya gharama kubwa hasa kwa wananchi wa kawaida.
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  May 21, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nemesis,
  Mkuu wangu nitakwambia kwamba China ni waigizaji wazuri sana. Kazi kubwa wanayoifanya wao ni kuepa gharama za Utafiti hivyo wao ni wepesi sana wa kuiga kitu pasipo kuingia gharama ya research. Ni wachina hawa wanatuletea madawa ambayo yamepigwa marufuku nchi za nje lakini tunayapokea TZ toka Household hadi vifaa vya Hospital with no guarantee ya kudumu au kufanya kazi vizuri. Usitolee mfano kabisa inapofikia ufanisi wa huduma.

  Kuhusu Upasuaji, nimetoka Bongo majuzi tu na kama nilivyosema nilikuwa Muhimbili ktk upasuaji wa mdogo wangu na kama kawaida yangu udadisi niliufanya...Haya nayozungumza sii utani mkuu wangu ndivyo ilivyo na nakuhakikishia hapa Canada haifanyiki hivyo, hakuna cha kuuliza daktari isipokuwa mama mjamzito atapasuliwa hivyo ikiwa tu aliwahi kupasuliwa hivyo (Uzazi uliopita). Jambo ambalo madaktari hapa wanachangaa kuona hadi sasa upasuaji wa namna hiyo bado unatumika Africa.. kwa nini washangae mkuu wangu kama ni kitu cha kawaida au inategemea.

  Kwanza kwa kufikiria tu unapompasua mtu kutoka kitovuni kushuka unakata nyama za muscles badala ya kuzichana kufuatana na marefu ya nyama..Hii haihitaji daktari au mwana sayansi kufikiria uponaji wake unavyokuwa mgumu ukilinganisha na kuchana.

  Tatu, mkuu wangu sizungumzii Watanzania kama jamii isiyoweza kuelimika isipokuwa ni hawa Madaktari wetu nyumbani. Huko nje Daktari ataifanya kazi kama alivyoelekezwa kuifanya hata kama kasoma tofauti. Kwa kila Operation jukumu ni la Hospital nzima ikitokea hitlafu yoyote. Nyumbani kwetu hakuna mtu anajali kitu mkuu wangu, yule jamaa aliyekufa kwa kupasuliwa kichwa nani kapelekwa mahakamani..Daktari anaendelea kufanya kazi ya upasuaji..Ukiuliza watakwambia ilikuwa Bahati mbaya - an accident kama asemavyo Mwanafalsafa.

  Mbali na hivyo sijui kama nimewahi kuandika hapa.. Kuna mshikaji wangu mwingine alipata ajali ya Pikipiki akaumia vibaya sana hadi mkono wake ulovunjika ukaunganishwa na vyuma..alitakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kichwani Daktari akampeleka MRI! mkuu unajua nachozungumza hapa..Kama umewekewa vyuma mwilini haiwezekani kabisa ukapelekwa MRI vyuma vyote vitachomoka mwilini lakini Daktari wetu walimpeleka MRI..Kwa bahati tu jamaa wa pale MRI alishtuka na kumuuliza kama ana chuma mwilini akasema kawekewa vyuma kuunga mkono wake..Na haya nayasema elewa jamaa alikwisha lazwa kwenye kitanda ilibakia tu asukumwe ndani ktk tanuri la kifo chake.

  Bongo inatisha mkuu wangu inatisha, hao Watanzania madaktari nje ni wazuri sana kwa sababu wanatumikia sehemu yenye sheria na kwa bahati mbaya ndio hamtaki warudi nyumbani ati walikimbia na kuikana nchi. Tuna madaktari zaidi ya 200 Brazil, Botswana sijui hesabu yake. UK, Marekani na Canada kibao wote hawa wangeweza kabisa kubadilisha mfumo wa utekelezaji matibabuy nyumbani lakini kwa sababu ya Ununda wetu, Umaskini jeuri tunawakana kwa sababu za kipuuzi kabisa hali tunawaagiza Wahindi na Wachina kuja kujenga na kuhudumia Hospital nchini tena na uhamiaji tunawajazia sisi wenyewe, tunawapa mishahara ya TX, nyumba, magari na hata Uraia wakitaka..Sasa kama hii sii jamii waliosoma lakini hawakuelimika tujiite kitu gani?
  Mkuu nakipaka kweli kwa sababu inaudhi sana kuona misomi ina vitambi kama mimba wala haijui kuwa ni maradhi! kisha inasema sana kusifia utendaji kazi wao wa masaa.
   
 17. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  mh! Bob taratibu, tutaogopa kutiwa sasa. Nimekuelewa mkuu.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  May 21, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu, nakusikia sana na mimi naandika hapa sii kwa ajili yako wewe au labda nasema tu kusema ila nataka hao walioko juu waipate pate. Majuzi tu kabla sijaondoka Bongo rafiki yangu mkewe kajifungua mtoto akawa na ear infection ikimsumbua sana, madaktari wa Bongo waka diagosis kuwa ana heart problem na alihitaji kupasuliwa. Bahati mkuu (mshikaji) alikuwa anaenda South akachukua picha za Xray akasafiri nazo kuwaonyesha madaktari wa huko.. ndio hao walimtonya kuwa hiyo ni ear infection tu watoto wengi huzaliwa nayo na mara nyingi huisha yenyewe....Jamaa ndio kusimamisha Upasuaji na kumtoa mtoto Hospital - leo hii mtoto yuko poa kabisa.
  Sasa nambie huyo mtoto angekuwa wa mlalahoi ingetokea nini..
  Jamani Bongo inatisha... Na ndio maana halisi ya neno - Bongo Tambarare!
   
 19. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #19
  May 21, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Jamani wabongo nao..Mbona wengine wetu hapa hatutubiwi kwenye hospitali za Serikali ingawa tupo hapa hapa nchini??
  tofauti iko wapi?
   
Loading...