Waziri mkuu Mizengo Pinda akana serikali haijamfunga mikono Dr.Hosea

We uoni unafiki wake?
Anashindwa kufanya kazi yake kakaa kulia lia oh nazuiwa si aseme kashindwa na aache ubinafsi aachie kiti watendaji kazi washike.!

Yaonekana hujui mfumo wa sheria zinazotumika na PCCB ktk kutekeleza majukumu yake
 
Wale wa buku saba lumbumba wakina HAMMY D mbona huku hawaji kutoa pumba zao waje hapa wakati taasisi 2 za serikali zinapingana kiutendaji
 
Yaonekana hujui mfumo wa sheria zinazotumika na PCCB ktk kutekeleza majukumu yake

Jaribu kuwa mchambuzi badala yakuwa mtetezi wa ujinga! mfumo unaomfanya mtu agange njaa na kulia lia kama mtoto badala ya kuweka utz mbele na kufanya kzi yenye mrejesho!
 
Acha uvivu.Soma sheria ya kitu husika ndipo utoa hoja.Kwa kukusaidia, Katika sheria namba 11 ya 2007 ya PCCB , Kifungu cha 5 (2) sheria inatambulisha kuwa PCCB ni chombo huru.
Ukisoma kifungu cha 15 (1), (a) & (b) utakuta panaelezewa makosa madogo madogo ya rushwa yasiyo ya maandishi au mikataba ambapa Mkurugenzi PCCB anaruhusiwa kupeleka mahakaman moja kwa moja na kifungu cha 15 (2) ni Adhabu - faini kati ya tshs 500,000/- na 1,000,000/- AU kifungo jela kati ya miaka 3 na 5. AU vyote kifungo na faini.

Ukisoma kifungu cha 16 (1) (a)& (b) na vifungu vingine vingi siweza andika vyote, kinaelezea makosa ambayo Mkurugenzi hana mamlaka kupeleka kesi za makosa hayo Mahakamani moja kwa moja isipokuwa mpaka DPP atoe kibali chake, tena kwa maandishi.

Kifungu cha 57 (1) & (2) Kinamfunga mikono mkurugenzi wa PCCB kutopeleka mafisadi papa mahakamani moja kwa moja, na ndicho anacholalamika Dk.Hosea.

Hebu angalia sheria hii ilivyo ya kibabaishaji. Katika kifungu cha 16 (3) adhabu yake ni kati ya Tshs 1,000,000/- na 3,000,000/- au kifungo jela kati ya miaka 3 hadi 5 AU vyote.

My take:-
*Dk. HOSEA yuko sahihi kuhusu kufungwa kwake mikono kisheria.
* Sheria za adhabu kwa upande wa faini haziangalii mpokea rushwa amepiga bingo la kiasi gani hata kama ni trilioni kadhaa, hakimu au jaji atamtoza adhabu ya faini isozidi Mill. 3
* Wanaotunga sheria ipo haja kuifanyia marekebisho
*@ breki sina, Tusifanye ushabiki wa siasa ktk masuala muhimu kama haya
 
Mh Pinda hakuna kitu na si lolote huyu nimeamini ni sawa na shok up kwenye gari huwezi amini anadai kuwa takukuru haiwezi kuchunguza na kupeleka kesi mahakamani hivyo wameweka utaratibu wa kupeleka kwa Dpp ili yeye ndio ahusike kupeleka hizo kesi mahakamani kuwa ni kutenda haki kwa watuhumiwa anachoficha Pinda na alichosema Hosea ni kuwa kesi zinazohusu mapapa na Nyangumi Takukuru hairuhusiwi kizipeleka mahakamani ila hizi za wezi wa kuku wanaruhusiwa kuzipeleka bila kupita kwa Dpp unaweza kuona jinsi ambavyo anawalinda mafisadi watanzania tusiwe wasahaulifu ni hivi karibuni kulitokea malumbano kati ya Dr.Hosea na Dpp kuhusu faili la Chenge kila mmoja akidai lipo ofisini kwake kuhusu pesa za Rada haya ndio mambo yanayowachikuza wananchi hata mkitupinga mkongoto,mioyo ya watu ikisha ingiwa na kiu ya kutaka mabadiliko hakuna Risasi ya kuizuia kamwe.

Uko sahihi mkuu..
 
Acha uvivu.Soma sheria ya kitu husika ndipo utoa hoja.Kwa kukusaidia, Katika sheria namba 11 ya 2007 ya PCCB , Kifungu cha 5 (2) sheria inatambulisha kuwa PCCB ni chombo huru.
Ukisoma kifungu cha 15 (1), (a) & (b) utakuta panaelezewa makosa madogo madogo ya rushwa yasiyo ya maandishi au mikataba ambapa Mkurugenzi PCCB anaruhusiwa kupeleka mahakaman moja kwa moja na kifungu cha 15 (2) ni Adhabu - faini kati ya tshs 500,000/- na 1,000,000/- AU kifungo jela kati ya miaka 3 na 5. AU vyote kifungo na faini.

Ukisoma kifungu cha 16 (1) (a)& (b) na vifungu vingine vingi siweza andika vyote, kinaelezea makosa ambayo Mkurugenzi hana mamlaka kupeleka kesi za makosa hayo Mahakamani moja kwa moja isipokuwa mpaka DPP atoe kibali chake, tena kwa maandishi.

Kifungu cha 57 (1) & (2) Kinamfunga mikono mkurugenzi wa PCCB kutopeleka mafisadi papa mahakamani moja kwa moja, na ndicho anacholalamika Dk.Hosea.

Hebu angalia sheria hii ilivyo ya kibabaishaji. Katika kifungu cha 16 (3) adhabu yake ni kati ya Tshs 1,000,000/- na 3,000,000/- au kifungo jela kati ya miaka 3 hadi 5 AU vyote.

My take:-
*Dk. HOSEA yuko sahihi kuhusu kufungwa kwake mikono kisheria.
* Sheria za adhabu kwa upande wa faini haziangalii mpokea rushwa amepiga bingo la kiasi gani hata kama ni trilioni kadhaa, hakimu au jaji atamtoza adhabu ya faini isozidi Mill. 3
* Wanaotunga sheria ipo haja kuifanyia marekebisho
*@ breki sina, Tusifanye ushabiki wa siasa ktk masuala muhimu kama haya

Sasa analia lia nini kama si yeye anayefanya kazi yakuamua nani apelekwe mahakamani.i!
Yeye aseme kazi yake amemaliza ataje mafisadi papa, mambo ya mahakamani awaachie akinaDPP.

Hapa hapana siasa watu wanataka mrejesho!
 
Huo mrejesho autoe kwa nani? Autoe ktk style ipi?
Kumbuka huwezi mtaja mtu hadharani kuwa ni fisadi mpaka pale maamuzi yatakapofikiwa na mahakama.Mshtakiwa kabla ya maamuzi yeye ni mtuhumiwa tu na ana haki ya kutochafuliwa kisheria.Sidhani kama Bw.Hosea anaweza kuwa sahihi aanze kuropoka kuwa flan ni fisadi hali kesi iko mahakani.Kama aweza kufanya hivyo itakuwa kama ya akina kinana na msigwa kudaiana fidia
 
Si anaushahidi wa kumtia hatiani, aseme ninani nananani wanatakiwa kufikishwa mahakamani. Hayo ya kuwafunga asiropoke, yeye ataje wanaotakiwa kupelekwa mahakamani tuwajue ili tumpigie kelele DPP awapelelke na aache kulilia kama mtoto.
 
Unao ubavu wa kumpigia na kumshawishi DPP? Kesi ngapi hata za kisiasa anapigiwa kelele lakini bado akiamua habadiliki?Lakini pia kumbuka sheria ya nchi yetu imempa mamlaka makubwa sana DPP kwamba akisema hakuna kesi ya kujibu, mtu au kiongozi awaye yote hana mamlaka ya kumuhoji.Hivyo basi sheria hii inamlinda DPP kuweza hata kuamua chochote hata kwa maslahi yake, viongozi waliompa cheo hicho, hata washkaji zake pia
 
Hizi kesi siyo kwamba ushahidi haujitoshezi,ukweli ni kwamba zinacheleweshwa makusudi na DPP kwasababu anaelewa kadri muda unavyo sogea wahusika muhimu na mashahidi muhimu wanakufa! Baada ya hapo kwa kutumia mamlaka yake atafuta kesi! PCCB wapewe meno ya kushitaki,Mahakama ndicho chombo kinatoa haki.
 
Shida ni kwamba udhaifu wa sheria za Rushwa ndio ngao ya mafisadi papa.Yaan hii kitu ni kuweka sheria makini zisizo na mianya ya kuwapa sababu mafisadi, lakini pia kuipa MENO chombo cha PCCB
 
Chini ya utawala wa CCM sheria hiyo haitabadilika kwasababu ni ngao kwa wanasiasa walafi toka chama tawala na watendaji wezi wa mali ya umma! Nasikia hata ktk rasimu ya katiba mpya taasisi hii muhimu haijazungumziwa,wakati Watanzania wengi wamelalamikia urasimu na rushwa wakati kamati ya kukusanya maoni ya wanachi ikizunguka mikoani!
 
Kwa mujibu wa rasimu hii, majukumu ya PCCB, sasa yatafanywa na Polisi
 
Polisi hawa wabambikaji kesi au wapi? Rushwa inamalizwa na Polisi?! Ninavyo fahamu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imesomesha wataalamu wengi tu ktk nyanja ya uchunguzi wa makosa ya rushwa. Tatizo ni sheria inayofunga mikono!
 
SFO wa UK waliochunguza BAE na uuzwaji wa Radar ni chombo cha serikali lakini kinauwezo wa kuchunguza serikali yao na mashirika ya umma na kuyashitaki bila vikwazo vyovyote, kwanini tusiipe PCCB uwezo huo .
 
Unao ubavu wa kumpigia na kumshawishi DPP? Kesi ngapi hata za kisiasa anapigiwa kelele lakini bado akiamua habadiliki?Lakini pia kumbuka sheria ya nchi yetu imempa mamlaka makubwa sana DPP kwamba akisema hakuna kesi ya kujibu, mtu au kiongozi awaye yote hana mamlaka ya kumuhoji.Hivyo basi sheria hii inamlinda DPP kuweza hata kuamua chochote hata kwa maslahi yake, viongozi waliompa cheo hicho, hata washkaji zake pia

Kama watu walimpigia kelele kikwete na akavunja baraza. Who is DPP wakati analipwa kodi yangu.lol!
 
Shida ni kwamba hata akipigiwa kelele, majibu atakayotoa, yatalindwa na sheria dhaifu inayompa madaraka
 
Back
Top Bottom