Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo hii ametoa taarifa ya kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokaa mapema leo kupokea na kujadili ripoti ya Kamati ya Mawaziri wanane iliyoundwa kubaini idadi ya vijiji vyenye migogoro ya Ardhi na maeneo mbalimbali ya Hifadhi. Katika taarifa ya awali kabla ya kamati hiyo kuundwa ilisemekana kuna vijiji 366 ambavyo viliingia au vinafanya shughuli zao za kilimo, ufugaji na uvuvi katika maeneo hayo. Lakini taarifa ya kamati inaonesha jumla ya vijiji 975 ndivyo vimebainika kuwa katika migogoro hiyo
Taarifa ya Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoendeshwa na Mhe. Rais kimeamua kuwa pasiwepo hata kijiji kimoja kitakachohamishwa kutoka katika maeneo hayo na kwamba kwa baadhi ya Hifadhi maeneo yanayokaliwa na vijiji viachiwe vijiji na kwamba serikali itaweka mipaka mipya bila kuviumiza vijiji.
Kwa hatua ya kwanza maeneo ya jumla ya vijiji 920 yameidhinishwa na imeagizwa vijiji hivi vipatiwe hati za vijiji. Kwa vijiji 55 vilivyosalia, upembuzi na uainishaji wa mipaka unaendelea na taarifa ya awamu ya pili pamoja na majina ya vijiji itatolewa mara baada ya mchakato kukamilika mapema iwezekenavyo.