Waziri Mkuu Majaliwa, naomba ufute posho za wabunge

Mheshimiwa Waziri Mkuu,

Natumaini wewe ni mzima wa afya na pole na majukumu.

Natumia jukwaa hili kukuomba wewe kama mtendaji mkuu wa serikali kufuta posho zote za wabunge kwani nao ni watumishi wa umma kama walivyo wafanyakazi wa serikali.

Ukifuta posho za wabunge tutapata fedha nyingi sana zitakazoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Natanguliza shukrani kwani naamini ombi langu litafanyiwa kazi.

Wako mtiifu katika kujenga nchi
hopetumaini wa JF
Msema kweli Mpenzi wa Mungu. Futa posho za vikao bila kujali ni wabunge au mawaziri nk. Vipi ofisi za wakuu wa mkoa na wilaya bado zina tija kweli zaidi kuongeza matumizi ya serikali
 
Duuh nikiufikiria mshahara wangu halafu nikafananisha na ule alioweka zitto halafu eti mbunge anasema atakwenda kunitetea bungeni
 
Rais anafanya anavyoona sawa kwenye kichwa chake bajeti ambayo bunge lilitakiwa kukaa na kuipitisha rais yeye ndio mwamuzi kama vile anaamua maamuzi ya familia yake hakuna kitu kinachoniuma mpaka leo kama kuchukua pesa za waathirika wa bukoba na kuzitia mfukoni ili azitumie kwa matakwa yake sio waliochanga hizo pesa wakati watu wanalala nje
Mkuu huko ni HOME
2020 HAPATI kura huko na CCM itapoteza wabunge wengi sana Kagera
Kama CHADEMA itapigana kwa TUME huru Magufuli atakuwa ONE TERM PRESIDENT
 
Lengo ni maskini waishi kama mashetani na matajiri waishi kama wako peponi! Hivi hadi sasa bado hamuelewi tu
 
Mimi nilijua tamko la kufuta posho ni kwa watumishi wote wa umma wakiwemo wabunge, kama kwa wabunge halifiki tamko hilo ipo haja wabunge wetu kwa uzalendo wao wasamehe na wakatae posho ili waendane na kasi yetu ya kubana matumizi
 
Rais anafanya anavyoona sawa kwenye kichwa chake bajeti ambayo bunge lilitakiwa kukaa na kuipitisha rais yeye ndio mwamuzi kama vile anaamua maamuzi ya familia yake hakuna kitu kinachoniuma mpaka leo kama kuchukua pesa za waathirika wa bukoba na kuzitia mfukoni ili azitumie kwa matakwa yake sio waliochanga hizo pesa wakati watu wanalala nje
zimepelekwa kujenga muundo mbinu wa Chato International Airport
 
Hasa bunge la bajeti halina sababu ya kuwepo. Hela zake zipelekwe kwenye ununuzi wa bombadia.

Tumuachie Rais maamuzi yote. Akiamua kununua ndege nyingi ili kusaidia watalii wengi kuja, ruksa. Haina sababu ya Wabunge kujadili na kupitisha hii! Akiamua kuwapa Mhimili wa mahakama mabilioni au akiamua kuwapa magereza mabilioni naona aachwe aamue kwa utashi wake na sio kutumia mabilioni kwa wabunge kama posho na kujadili mambo kama hayo!

Maamuzi ya Rais yanatosha!
Hivi bunge la Bajeti huwa linasaidia nini wakati kila kitu wabunge huwa wanasema ndiyooooooo.Mie nashauri bunge La Bajeti lifutwe au lifanyike online kila MTU akiwa kwao
 
Mheshimiwa Waziri Mkuu,

Natumaini wewe ni mzima wa afya na pole na majukumu.

Natumia jukwaa hili kukuomba wewe kama mtendaji mkuu wa serikali kufuta posho zote za wabunge kwani nao ni watumishi wa umma kama walivyo wafanyakazi wa serikali.

Ukifuta posho za wabunge tutapata fedha nyingi sana zitakazoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Natanguliza shukrani kwani naamini ombi langu litafanyiwa kazi.

Wako mtiifu katika kujenga nchi
hopetumaini wa JF
afute na posho za mawaziri pia.
 
Posho za makalio ya Wabunge zitafutwa na Bunge kupitia Wabunge wenyewe sio Waziri Mkuu!!
 
Kama wenyewe wananufaika na hizo posho wawaache na wengine wanufaike.
Vinginevyo itaonekana kuwa tumewapa madaraka ambayo mnatumia kujinufaisha na kutufanya tuishi kama mashetani
 
Mheshimiwa Waziri Mkuu,

Natumaini wewe ni mzima wa afya na pole na majukumu.

Natumia jukwaa hili kukuomba wewe kama mtendaji mkuu wa serikali kufuta posho zote za wabunge kwani nao ni watumishi wa umma kama walivyo wafanyakazi wa serikali.

Ukifuta posho za wabunge tutapata fedha nyingi sana zitakazoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Natanguliza shukrani kwani naamini ombi langu litafanyiwa kazi.

Wako mtiifu katika kujenga nchi
hopetumaini wa JF
 
Mheshimiwa Waziri Mkuu,

Natumaini wewe ni mzima wa afya na pole na majukumu.

Natumia jukwaa hili kukuomba wewe kama mtendaji mkuu wa serikali kufuta posho zote za wabunge kwani nao ni watumishi wa umma kama walivyo wafanyakazi wa serikali.

Ukifuta posho za wabunge tutapata fedha nyingi sana zitakazoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Natanguliza shukrani kwani naamini ombi langu litafanyiwa kazi.

Wako mtiifu katika kujenga nchi
hopetumaini wa JF

Mkuu
Kwa kuzingatia doctrine ya separation of power huo ni muhimili mwingine.
 
Apunguze au kufuta night zote za mawazili haiwezekani night moja ya waziri sawa na mishahara ya walimu watatu kwa mwezi mmoja yeye analipwa kwa usiku mmoja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom