Waziri Mkuu Majaliwa, naomba ufute posho za wabunge

hopetumaini

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
503
500
Mheshimiwa Waziri Mkuu,

Natumaini wewe ni mzima wa afya na pole na majukumu.

Natumia jukwaa hili kukuomba wewe kama mtendaji mkuu wa serikali kufuta posho zote za wabunge kwani nao ni watumishi wa umma kama walivyo wafanyakazi wa serikali.

Ukifuta posho za wabunge tutapata fedha nyingi sana zitakazoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Natanguliza shukrani kwani naamini ombi langu litafanyiwa kazi.

Wako mtiifu katika kujenga nchi
hopetumaini wa JF
 

mshunami

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
3,988
2,000
Hasa bunge la bajeti halina sababu ya kuwepo. Hela zake zipelekwe kwenye ununuzi wa bombadia.

Tumuachie Rais maamuzi yote. Akiamua kununua ndege nyingi ili kusaidia watalii wengi kuja, ruksa. Haina sababu ya Wabunge kujadili na kupitisha hii! Akiamua kuwapa Mhimili wa mahakama mabilioni au akiamua kuwapa magereza mabilioni naona aachwe aamue kwa utashi wake na sio kutumia mabilioni kwa wabunge kama posho na kujadili mambo kama hayo!

Maamuzi ya Rais yanatosha!
 

Manstone

JF-Expert Member
May 12, 2013
481
500
Ivi Unajaribu Kugeuza Jiwe Kuwa Mkate?
Maskini Waishi Kama Mashetani Na Siyo Wabunge
 

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,010
2,000
PM ni MBUNGE hawezi jifutia posho zake mwenyewe
Kama umegundua utawala huu hawafanyi kitu chochote ambacho na wao wataumia
Rais wa TZ bado halipi kodi
Rais wa TZ hajajipunguzia mshahara ingawa kapunguza mishahara ya kada wengine
PM kafuta posho za wengine,zao wabunge akiwemo na yy hawezi zigusa
Utawala wa ajabu sana huu
Utawala wa wachumia tumbo!
 

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,010
2,000
Hasa bunge la bajeti halina sababu ya kuwepo. Hela zake zipelekwe kwenye ununuzi wa bombadia. Tumuachie raisi maamuzi yote. Akiamua kununua ndege nyingi ili kusaidia watalii wengi kuja, ruksa. Haina sababu ya Wabunge kujadili na kupitisha hii! Akiamua kuwapa Mhimili wa mahakama mabilioni au akiamua kuwapa magereza mabilioni naona aachwe aamue kwa utashi wake na sio kutumia mabilioni kwa wabunge kama posho na kujadili mambo kama hayo! Maamuzi ya raisi yanatosha!
HUWA HADI LEO NATATIZIKA SANA:
Pesa za kununulia ndege
Pesa za kuhamia Dodoma
Pesa alizowapa Magereza
ZILITENGWA na Bunge la mwaka gani?Rais kapata wapi mabilion haya?
 

Ndaba

Senior Member
Jan 19, 2014
146
250
HUWA HADI LEO NATATIZIKA SANA:
Pesa za kununulia ndege
Pesa za kuhamia Dodoma
Pesa alizowapa Magereza
ZILITENGWA na Bunge la mwaka gani?Rais kapata wapi mabilion haya?
Rais anafanya anavyoona sawa kwenye kichwa chake bajeti ambayo bunge lilitakiwa kukaa na kuipitisha rais yeye ndio mwamuzi kama vile anaamua maamuzi ya familia yake hakuna kitu kinachoniuma mpaka leo kama kuchukua pesa za waathirika wa bukoba na kuzitia mfukoni ili azitumie kwa matakwa yake sio waliochanga hizo pesa wakati watu wanalala nje
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
kumbuka waziri mkuu mwenyewe ni mbunge nani atakubali kujipunguzia posho? hilo sahau. wafanyakazi wengine safari hii wataburuzwa sana....
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Rais anafanya anavyoona sawa kwenye kichwa chake bajeti ambayo bunge lilitakiwa kukaa na kuipitisha rais yeye ndio mwamuzi kama vile anaamua maamuzi ya familia yake hakuna kitu kinachoniuma mpaka leo kama kuchukua pesa za waathirika wa bukoba na kuzitia mfukoni ili azitumie kwa matakwa yake sio waliochanga hizo pesa wakati watu wanalala nje
kwa sasa rais wetu ndo katiba, sheria, kanuni na taratibu zote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom