Waziri mkuu kuwajibishwa na bunge inawezekana ila sio kwa bunge hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri mkuu kuwajibishwa na bunge inawezekana ila sio kwa bunge hili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Baba Hinda, Apr 20, 2012.

 1. B

  Baba Hinda New Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kusema kuwa kwa mujibu wa sheria na taratibu inawezekana Waziri Mkuu kuwajibishwa na bunge kama alivyoainisha Mh. Zito jana. Lakini naomba mniamini kuwa Bunge hili haliwezi kufanya hivyo.

  Wabunge wengi hawana misimamo thabiti. Ni wabunge wachache wanaoweza kusimamia wanachoamua kwa dhamira ya dhati. Wengi hawana ujasiri huo, hivyo kupata idadi inayostahili kumuondoa Waziri Mkuu kwa sasa si jambo rahisi japo linawezekana.

  Sisi sote ni mashahidi juu ya mambo mbalimbali muhimu kwa Taifa letu na yaliyoamuliwa na wabunge wenyewe, lakini baadaye wakayatelekeza ama kuyapuuza kinyume na walivyoamua awali. Uzoefu unatuthibitishia kwamba wengi wa wabunge, hususan wa kutoka CCM, sio watu wa kuaminiwa.

  Hawana ustaarabu wa kuheshimu makubaliano lakini pia hawana muda au uwezo wa kufikiri kwa usahihi. Na hii ni kwasababu hawakuwa wabunge kwa maana halisi ya ubunge ila kupata njia ya kufanya au kupata yaliyo ya binafsi. Kwahiyo ninaona kuwa haiwezekani kumuondoa Waziri Mkuu japo ANASTAHILI KUONDOKA.
   
 2. babujii

  babujii Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Bunge hili la leo linaweza kufanya miujiza kwani waajiri wa wabunge hao wako hoi,wabunge watapataje mishahara yao?
   
Loading...