Waziri Mkuu kuelekea Japan!

Lanlady

JF-Expert Member
Feb 27, 2019
1,420
4,728
Huku bei za bidhaa zikizidi kupanda, tozo nazo kila mahali; cha kushangaza ni kwamba, hakuna jitihada zozote zinazooneshwa na viongozi wa serikali kuu katika kubana matumizi!

Ziara na misafara imekuwa mingi na ya kila siku. Ni kweli hatuwezi kuwa sawa kiuchumi, lakini angalau zionekane jitihada za pamoja na za wazi, katika kubana matumizi yasiyo ya lazima!

Tukumbuke, 'ngoma ikilia sana, mwishowe upasuka!'

Mtaani hali ni mbaya, mfumuko wa bei ni wa kasi kubwa!

Wananchi wengi wanalalamika!
Hakuna anayeonesha kusikiliza kilio chao!

'Ee Mwenyezi Mungu, tunakuomba uwajalie viongozi wetu utu na huruma kwa wananchi wanaowaongoza" Amen!
 
Huku bei za bidhaa zikizidi kupanda, tozo nazo kila mahali;cha kushangaza ni kwamba, hakuna jitihada zozote zinazooneshwa na viongozi wa serikali kuu katika kubana matumizi!

Ziara na misafara imekuwa mingi na ya kila siku. Ni kweli hatuwezi kuwa sawa kiuchumi, lakini angalau zionekane jitihada za pamoja na za wazi, katika kubana matumizi yasiyo ya lazima!

Tukumbuke, 'ngoma ikilia sana, mwishowe upasuka!'
Mtaani hali ni mbaya, mfumuko wa bei ni wa kasi kubwa! Wananchi wengi wanalalamika!
Hakuna anayeonesha kusikiliza kilio chao!

'Ee Mwenyezi Mungu, tunakuomba uwajalie viongozi wetu utu na huruma kwa wananchi wanaowaongoza" Amen!
Kwahio sasa hivi nchi ipo chini ya nani?
Tulia ackson(PhD) au?
 
Nchi yetu siyo kisiwa, Hivyo Ni lazima ishirikiane na nchi nyingine kidiplomasia na Ni katika ushirikiano huo tunapopata wawekezaji na watalii mbalimbali Kuja hapa kwetu nchini, ukisikia wawekezaji wameongezeka au Tanzania imeongeza uuzaji wa bidhàa nje ya nchi Basi ufahamu kuwa Ni matunda ya safari za viongozi wetu wanazofanya huko waendako kazi ya kujenga mahusiano mazuri na wenzetu

Ili Tuendelee tunahitaji kuongeza na kuvutia wawekezaji ambao watasaidia kuongeza wigo wa Kodi na kutoa ajira kwetu vijana, Kodi zitakazo saidia kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kutatua kero mbalimbali
 
Utasikia kesho kutwa Tulia Ackson naye anasepa na nchi itabakia chini ya Jaji.

Hii utaendelea mpk nchi ibakie chini ya kamanda Muliro


Tozo zetu zinachezewa sana
Nchi yetu Ni salama na IPO katika mikono salama wakati wote, Tanzania chini ya serikali ya CCM Ni salama na ndio maana wananchi wameendelea kuwa na Imani na CCM na kuweka matumaini katika chama hiki kimbilio la wanyonge,
 
Acha gubu
Gubu haliachwi hadi nitakaposikia tamko la kusitisha tozo za uonevu!

Mbona zama za Jk, alisafiri sana na mikutano mingi ilifanyika nje ya nchi, ziara za kikazi nk, lakini hakukuwa na tozo za uonevu?

Kwasasa mambo mengi yameathiri uchumi wa mataifa mengi.
Hizi safari za kwenda msibani kuaga na kuzika zina tija gani kwa taifa?
 
Ukisikia kupatwa kwa Tanzania ndiyo huku sasa! Rais alikuwa Uingereza kumzika Malkia! Alipotoka huko akaunganisha Msumbiji!! Wakati huo huo Makamu naye akapaa kwenda kwa Joe Biden kuhudhuria mkutano wa UNGA gani sijui!

Wakati hao viongozi wawili wajuu wakiwa bado wapo nje ya nchi, na PM naye anataka kupaa!! Muda si mrefu na Spika naye atatafuta kamtoko kake!! Yaani mambo ni bam bam kwa sasa.
 
Nchi yetu Ni salama na IPO katika mikono salama wakati wote, Tanzania chini ya serikali ya CCM Ni salama na ndio maana wananchi wameendelea kuwa na Imani na CCM na kuweka matumaini katika chama hiki kimbilio la wanyonge,
Acha kukera watu basi wewe uvccm.
 
Mfumo wa ujamaa wala haupo hivyo,rc anatembelea gari la m 500 halafu unasema mfumo wa kijamaa,huu mfumo wa kivyao vyao walamba honey

Hata kule Korea Kaskazini yule Kim Jong-Un anaishi maisha ya kifahari sana wakati wananchi wake wanakufa njaa. Wajamaa na wakomunisti ni wanafiki sana usishangae.
 
Nchi yetu Ni salama na IPO katika mikono salama wakati wote, Tanzania chini ya serikali ya CCM Ni salama na ndio maana wananchi wameendelea kuwa na Imani na CCM na kuweka matumaini katika chama hiki kimbilio la wanyonge,
Wanyonge wenye "vieite"?
 
Ukisikia kupatwa kwa Tanzania ndiyo huku sasa! Rais alikuwa Uingereza kumzika Malkia! Alipotoka huko akaunganidha Msumbiji!! Wakati huo hjo Makmu akapaa kwenda kwa Joe Biden kuhudhuria mkutano wa UNGA!

Wakati hao viongozi wawili wajuu wakiwa bado wapo nje ya nchi, na PM naye anapaa!! Muda si mrefu na Spika naye atatafuta kamtoko kake!! Yaani mambo ni bam bam kwa sasa.
Hapo mkuu, hujataja mawaziri, makamishna, makatibu wakuu na misafara yao!

Ukweli ni kwamba, tunapaswa kufahamishwa bajeti ya hizi safari inatoka kwenye fungu gani? Na je zina tija kwa taifa?

Kukatwa tozo na kodi zaidi ya mara moja kwa kipato hicho hicho, inaumiza sana!
Ukizingatia mfumuko wa bei nao uko juu! Ukienda sokoni leo, kesho yake unakuta bidhaa imepanda bei! Twende wapi?

Kuna mtu mmoja jana baada ya kukuta bei ya mahindi imepanda, akauliza "au ndio kiama kimekaribia?"
Wananchi hawaelewi. Wamevurugwa!

Cha ajabu viongozi hawaoneshi ushirikiano katika kubana matumizi ya fedha za umma! 😭😔
 
Acha kukera watu basi wewe uvccm.
Nasema hivi nchi yetu siyo kisiwa Ni lazima tushirikiane na wenzetu kugawana fursa za kiuchumi na kibiashara kwa maslahi mapana ya mataifa yetu, unafikiri sisi vijana tutapata wapi ajira Kama serikali isipovutia wawekezaji watakao Jenga viwanda na kuwekeza katika nyanja tofauti tofauti zitakazozalisha ajira kwetu vijana, lakini pia hata uchumi ukikua ndipo serikali inapokuwa na uwezo wa kutoa ajira nyingi zaidi ambapo sisi vijana ndio wanufaika wa kwanza
 
Back
Top Bottom