Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,668
- 10,092
Ndugu zangu Watanzania,
Nashukuru kuwa viongozi wetu wakubwa ngazi ya Taifa chamani na serikalini wameanza kutambua kiu ya mamilioni ya watanzania waliyo nayo ya vifuani pao ya kuhitaji utumishi wa Rais Samia kwa mhula wa pili.
Mh Kasimu Majaliwa ambaye ni waziri Mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania amemuomba makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Mh Kinana kwenda kuwashawishi wajumbe wa kamati kuu na halmashauri kuu ya CCM Taifa kuchapisha Fomu moja tu ya Urais kwa ajili ya Rais Samia.
Jambo ambalo Mh kinana aliliunga mkono kwa kutambua kazi kubwa iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na Mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan,akasema ni utamaduni wa CCM kumpa muhula wa pili kiongozi anayekuwa amemaliza muhula wake wa kwanza .akasema ameona kila mtu anayesimama kuzungumza anazungumza namna Mh Rais alivyofanya kazi kubwa katika Taifa letu.
Mimi mwashambwa nimewahi kuzungumza humu jukwaani kuwa wanaccm wanapaswa kukata kiu ya watanzania kwa kuwapa chaguo na hitaji lao Ambalo ni Rais Samia. CCM itawakatisha Sana tamaa , kuwavunja moyo na kuwabubujisha sana machozi Watanzania isipowapelekea Rais Samia kama mgombea wake.
Watanzania wanamhitaji Rais Samia.huyo ndio chaguo lako,.ndio chaguo la vijana,akina mama,wazee, bodaboda,waendesha bajaji,wakulima, wafanyabiashara,wanafunzi wa vyuo, watumishi wa umma.n.k.
CCM Haina budi kusikiliza sauti za watu zinazoendelea kupazwa zikimhitaji Rais samia muhula wa pili. Huyo ndiye ambaye atapewa kura za ndio kwa kishindo kitakachoitikisa Tanzania nzima. CCM tuleteeni Rais Samia kukata kiu yetu watanzania.CCM tuleteeni chaguo letu Rais Samia.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.