Asiwapangie hiyo ni taasisi binafsi MBONA WAO SERIKALI WAMESHINDWA KUFANYA HIVYO?WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa, ameutaka uongozi wa Hospitali ya Aga Khan uandae skeli ya mishahara inayofanana kwa watumishi wenye taaluma zinazofafana ili kuondoa manung’uniko baina ya wafanyakazi wa taasisi hiyo.
Ameyasema hayo kutokana na malalamiko ya watumishi wa taasisi hiyo ambao wanadai kuwepo kwa tofauti ya mishahara kwa watumishi licha ya kuwa na taaluma moja na kufanyakazi kwenye kituo kimoja.
Hayo yalisemwa jana (Jumamosi, Machi 9, 2019) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.
Waziri Mkuu alisema suala la maslahi kwa watumishi ni muhimu na linatiliwa mkazo na serikali hivyo uongozi wa Hospitali ya Aga Khan fanyeni mapitio ya mishahara hasa kwa watu walio katika taaluma zinazofanana.
“Serikali imeunda Tume ya Mishahara na Motisha inayofanya mapitio ya ngazi za mishahara ili kuondoa utofauti wa mishahara kwa watumishi waliosoma ngazi moja, wenye taaluma moja wanaofanyakazi kwenye kituo kimoja.”
Waziri Mkuu aliongeza kuwa suala la uwiano wa mishahara kwa watumishi wenye taaluma zinazofanana ni muhimu na linapaswa lifanywe kwa watumishi wote bila ya kujali kama mtumishi huyo ni Mtanzania au anatoka nje ya Tanzania.
Awali, Waziri Mkuu alitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma katika jengo hilo ikiwemo maabara, chumba cha upasuaji, wodi ya watoto, wodi ya wazazi. Ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu sh. bilioni 192, kati yake sh. bilioni 134 ni mkopo wa muda mrefu wenye masharti nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).
Muwe mnajipa muda wa kuvaa uhusika. Ebu jaribu kujichukulia wewe ni mfanyakazi uliyepo pale na una same professional na kanjibai ila wewe unalipwa kidunchu na kanji anakuzunguuka kama Mara 5 ivi na kiongozi wenu kaja na kawapa nafasi na nyie weusi mmetoa dukuduku lenu kisha unaona mtu huku jf kaandika kama ulivyoandika ivi utamuonajeAsiwapangie hiyo ni taasisi binafsi MBONA WAO SERIKALI WAMESHINDWA KUFANYA HIVYO?
Utakuwa haujamuelewa PM. Soma tena utaelewa wameanzisha nini kwa lengo ganiTena huku serikalini ndio kuna maajabu utakuta mwenye degree halmashauri au mashirika ya umma tofauti ya mshahara ni kubwa mbo
Nimemuelewa ila ww ndio umedandia treni kwa mbele hujanielewaUtakuwa haujamuelewa PM. Soma tena utaelewa wameanzisha nini kwa lengo gani
Sent using Jamii Forums mobile app
hata huku serikalini hizo issue zipo sana why asi solve huku kwenye mamlaka naye?Muwe mnajipa muda wa kuvaa uhusika. Ebu jaribu kujichukulia wewe ni mfanyakazi uliyepo pale na una same professional na kanjibai ila wewe unalipwa kidunchu na kanji anakuzunguuka kama Mara 5 ivi na kiongozi wenu kaja na kawapa nafasi na nyie weusi mmetoa dukuduku lenu kisha unaona mtu huku jf kaandika kama ulivyoandika ivi utamuonaje
Sent using Jamii Forums mobile app
Yani bora angenyamaza tu pm vitu vingine asiingilie mashirika binafsiParagraph ya nne na tano, tume ya serikali inafanya mapitio kwa miaka minne, ya wahindi itafanya kwa miaka mingapi?
Sent using Jamii Forums mobile app
ANgeanza na tofauti ya mishahara ya watu wa TRA na huku kwetu halmashauri wakati wote wana Degree na fani moja lakini gap kubwa la salary.