busha
JF-Expert Member
- Jan 21, 2019
- 1,712
- 2,574
Mkuu pale pm anazungumzia ubaguzi wa rangi,skeli kwa wahindi ipo juu kuliko weusi japo level na kazi ni ileileAsiwapangie hiyo ni taasisi binafsi MBONA WAO SERIKALI WAMESHINDWA KUFANYA HIVYO?
Mfano wa Mwalimu wa Degree na Mfanyakazi wa TRA mwenye degree wanatofautiana kuanzia marupurupu mpaka mshahara.Tena huku serikalini ndio kuna maajabu utakuta mwenye degree halmashauri au mashirika ya umma tofauti ya mshahara ni kubwa mbo
Hivi ni wewe ???Mara Aghakan ashushe bei Za gharama Za Matibabu Mara aweke ulinganifu wa Mishahara!
Tuacheni ushamba!
Aghakan sio Shirika la Umma
Asieweza gharama Za Matibabu Aghakhan si aende Sinza Palestina Hospital Au Mwanayamala Hospitali akapate Matibabu ya Bei chee? Ubora wa Matibabu Yao ndio unaosababisha bei Kuwa ya Juu
Ni sawa kulazimisha Bei ya Sahani ya chips ya Thai khan Restaurant or Karambezi Au Serena Kuwa sawa Na bei ya chips ya 'kwa Mangi' ili kuwezesha walalahoi kula chips
Kuhusu Mishahara lazima Viongozi wajue Determinants ya Mishahara sio vyeti pekee Kuwa Mkiwa Na Elimu sawa Au position sawa Basi lazima Mishahara ifanane Mf. Mwepesi Kwenye Makampuni ya Simu Au Banks Mishahara pia inaweza Kuwa determined Na performance
Inatia aibu Sana Sana mambo Mengine
Mie Nina Wafanyakazi Wawili wa ndani lakin Mishahara yao sio sawa kwa Kuwa factors which determine wage rate Ni nyingi mno
tofauti ipo kati a nini na nini?WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa, ameutaka uongozi wa Hospitali ya Aga Khan uandae skeli ya mishahara inayofanana kwa watumishi wenye taaluma zinazofafana ili kuondoa manung’uniko baina ya wafanyakazi wa taasisi hiyo.
Ameyasema hayo kutokana na malalamiko ya watumishi wa taasisi hiyo ambao wanadai kuwepo kwa tofauti ya mishahara kwa watumishi licha ya kuwa na taaluma moja na kufanyakazi kwenye kituo kimoja.
Hayo yalisemwa jana (Jumamosi, Machi 9, 2019) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.
Waziri Mkuu alisema suala la maslahi kwa watumishi ni muhimu na linatiliwa mkazo na serikali hivyo uongozi wa Hospitali ya Aga Khan fanyeni mapitio ya mishahara hasa kwa watu walio katika taaluma zinazofanana.
“Serikali imeunda Tume ya Mishahara na Motisha inayofanya mapitio ya ngazi za mishahara ili kuondoa utofauti wa mishahara kwa watumishi waliosoma ngazi moja, wenye taaluma moja wanaofanyakazi kwenye kituo kimoja.”
Waziri Mkuu aliongeza kuwa suala la uwiano wa mishahara kwa watumishi wenye taaluma zinazofanana ni muhimu na linapaswa lifanywe kwa watumishi wote bila ya kujali kama mtumishi huyo ni Mtanzania au anatoka nje ya Tanzania.
Awali, Waziri Mkuu alitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma katika jengo hilo ikiwemo maabara, chumba cha upasuaji, wodi ya watoto, wodi ya wazazi. Ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu sh. bilioni 192, kati yake sh. bilioni 134 ni mkopo wa muda mrefu wenye masharti nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).
Sio, ukimaanisha nini?Aghakhan polyclinic zao sio aisee
Kuanzia customer care hadi huduma ya mwisho
Ila pale mjini pako poa sana.
MbayaaaaaSio, ukimaanisha nini?
Oooh kumbe.... ahsante kwa kunijuzaMbayaaaaa