Waziri Mkuu Awataka Agha Khan Wabadilishe Skeli Ya Mishahara.....Asema lengo ni kuondoa manung’uniko kwa watumishi wa taaluma moja

kiwenini

Member
Nov 25, 2018
73
43
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa, ameutaka uongozi wa Hospitali ya Aga Khan uandae skeli ya mishahara inayofanana kwa watumishi wenye taaluma zinazofafana ili kuondoa manung’uniko baina ya wafanyakazi wa taasisi hiyo.

Ameyasema hayo kutokana na malalamiko ya watumishi wa taasisi hiyo ambao wanadai kuwepo kwa tofauti ya mishahara kwa watumishi licha ya kuwa na taaluma moja na kufanyakazi kwenye kituo kimoja.

Hayo yalisemwa jana (Jumamosi, Machi 9, 2019) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

Waziri Mkuu alisema suala la maslahi kwa watumishi ni muhimu na linatiliwa mkazo na serikali hivyo uongozi wa Hospitali ya Aga Khan fanyeni mapitio ya mishahara hasa kwa watu walio katika taaluma zinazofanana.

“Serikali imeunda Tume ya Mishahara na Motisha inayofanya mapitio ya ngazi za mishahara ili kuondoa utofauti wa mishahara kwa watumishi waliosoma ngazi moja, wenye taaluma moja wanaofanyakazi kwenye kituo kimoja.”

Waziri Mkuu aliongeza kuwa suala la uwiano wa mishahara kwa watumishi wenye taaluma zinazofanana ni muhimu na linapaswa lifanywe kwa watumishi wote bila ya kujali kama mtumishi huyo ni Mtanzania au anatoka nje ya Tanzania.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma katika jengo hilo ikiwemo maabara, chumba cha upasuaji, wodi ya watoto, wodi ya wazazi. Ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu sh. bilioni 192, kati yake sh. bilioni 134 ni mkopo wa muda mrefu wenye masharti nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).
 
Asiwapangie hiyo ni taasisi binafsi MBONA WAO SERIKALI WAMESHINDWA KUFANYA HIVYO?
 
Muwe mnajipa muda wa kuvaa uhusika. Ebu jaribu kujichukulia wewe ni mfanyakazi uliyepo pale na una same professional na kanjibai ila wewe unalipwa kidunchu na kanji anakuzunguuka kama Mara 5 ivi na kiongozi wenu kaja na kawapa nafasi na nyie weusi mmetoa dukuduku lenu kisha unaona mtu huku jf kaandika kama ulivyoandika ivi utamuonaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hat

hata huku serikalini hizo issue zipo sana why asi solve huku kwenye mamlaka naye?
Huo ni unafiki unaenda ku solve mgogoro wa jirani huku kwako kunawaka moto
 
Mara Aghakan ashushe bei Za gharama Za Matibabu Mara aweke ulinganifu wa Mishahara!

Tuacheni ushamba!

Aghakan sio Shirika la Umma

Asieweza gharama Za Matibabu Aghakhan si aende Sinza Palestina Hospital Au Mwanayamala Hospitali akapate Matibabu ya Bei chee? Ubora wa Matibabu Yao ndio unaosababisha bei Kuwa ya Juu

Ni sawa kulazimisha Bei ya Sahani ya chips ya Thai khan Restaurant or Karambezi Au Serena Kuwa sawa Na bei ya chips ya 'kwa Mangi' ili kuwezesha walalahoi kula chips

Kuhusu Mishahara lazima Viongozi wajue Determinants ya Mishahara sio vyeti pekee Kuwa Mkiwa Na Elimu sawa Au position sawa Basi lazima Mishahara ifanane Mf. Mwepesi Kwenye Makampuni ya Simu Au Banks Mishahara pia inaweza Kuwa determined Na performance

Inatia aibu Sana Sana mambo Mengine

Mie Nina Wafanyakazi Wawili wa ndani lakin Mishahara yao sio sawa kwa Kuwa factors which determine wage rate Ni nyingi mno
 
Ndio maana wakati mwingine naona upinzani ni roho ya shetani, siku zote inaangalia mabaya tu, ujinga mtupu, serikali imeunda time ya muda mrefu kutokana na ukubwa Wa serikali. Serikali kutetea raia wake kuna ubaya? Embu acheni roho za kichawi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka miaka 5 inaisha hiyo tume ya mishahara haimalizi kazi? Ila kwa baniani nako kuna mushkeli kweli ubaguzi waziwazi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom