Waziri Mkuu awaasa viongozi wa dini wasiruhusu vikundi nje ya mifumo ya Taasisi zao kuwasemea!

Mimi kwa maoni yangu hatutafika popote kwenye hili maadamu watoa maamuzi wetu nao ni waumini wa hizi hizi Dini, tufanye kama Wazungu kama Viongozi wetu wanaona wanashindwa kudili na Viongozi fake wa Kidini wanaotumia Dini kwa manufaa yao Binafsi tukabidhi nchi au sehemu ya Serikali inayoadili na mambo ya Dini kwa mtu asiye na Dini kwa kipindi amalize huu mjadala, hili linawezekana na wapo wengi tu wanaoweza kuufunga kwa dakika sifuri!

Wazungu hutumia sana hii mbinu ndo maana hata USA wamemleta D. Trump ili aweke mambo sawa kwa maana wale wengine ni ,,wastaarabu" na waoga sana ona sasa anavyopambana kupunguza trade deficit ya USA kwa nguvu zote dadadeki na hakuna Maandamano USA kumpinga unafikiri ni kwa nini? wako pamoja naye, Ufilipino walimleta Duterte ili aondoe drug barons na kweli aliwamaliza hakusikia umoja wa Mataifa wala nini leo hii tatizo limepugua!

Hivyo hili linawezekana kabisa kama wenye Mamlaka wanawaonea haya viongozi wa kidini, wakabidhi watu ambao hawajali kwa muda, ili kuiokoa nchi yetu, kwani tuna Dini nyingi na kila mtu akitaka Dini isikilizwe hatuwezi kuwa na nchi tena!
 
PM mara nyingi huwa ana busara lakini katika kauli ambazo ni za hovyo na zilizokosa hekima ni hii ya leo.

Najua alicholenga ni vyama vya siasa kuongelea barua ya Msajili dhidi ya waraka wa KKKT na TEC. Siamini kama KKKT na TEC waliwaomba vyama vya upinzani kuwasemea bali wapinzani walilisemea hilo kwa vile waraka wa Msajili ulikuwa wa kipuuzi uliolenga kutishwa taasisi za dini.

Hivi serikali isingetoa ule waraka wa kipuuzi, akina Mbatia wangeanza tu kuuzungumzia waraka wa serikali ambao haupo?

Hivi kwa mfano serikali isingeonekana kufanya au kufurahia mauaji na utekaji wa raia na biashara ya kununua watu, hizo nyaraka zingetoka? Kwa nini serikali inapenda kulaumu watu au taasisi nyingine kwa makosa ya kwao?

Serikali itimize wajibu wake. Viongozi watimize wajibu wao kwa kadiri ya viapo vyao. Watii katiba, walinde katiba. Wawatendee watu wote kwa haki na usawa. Wawe wabunifu. Waweke mipango ya kuinua uchumi badala ya kuua uchumi. Wasimamie kwa weledi mipango ya kuvutia uwekezaji ili kuinua mapato ya ndani na kuongeza ajira. Waheshimu haki za raia na misingi ya demokrasia. Halafu tuone kama atakuwepo wa kutoa waraka au wa kutoa kauli za kupambana na serikali kwaajili ya kutafuta haki.

Lawama nyingi dhidi ya serikali kwa sasa zimesababishwa na serikali yenyewe.
 
Elewa kauli ya PM kwanza ndio ujibu ...usitafute "first reply" halafu huna kiwango cha uchanganuzi.

Waziri mkuu anazuga tu, KKKT au TEC hizo taasisi zinaendeshwa na viongozi wwnye weledi hakuna kikundi wala chama kilicgo nje ya madaraka kina weza kuwatumia. Sanasana chama kilicgoko madarakani kwa kutumia nguvu ya dola ndio kinaweza kulitumia kanisa na sio kinyume na hapo.

Ukweli uko wazi na hauwezi kufichika zile nyaraka za maaskofu zilizungumzia siasa za kishenzi na ukatili uliokuwa unaongozwa na mkulu kwa ulevi wa madaraka kwa kushirikiana na kundi lake la akina Polepole, Bashite nk kuhujumu, kuteka, kutesa na hata kuua wale wenye mitazamo tofauti na serekali. Waziri mkuu asidhani maaskofu walikuwa ni vipofu au viziwi wakati watu wanatekwa, wanauwawa, ukatili kwenye chaguzi za marudio tena kwa uratibu wa vyombo vya dola, yote hayo watanzania wote wakiwemo maaskofu waliona. Na ushahidi toka nyaraka zile zimetoka hatukuona tena watu kutekwa, kuuwawa, kuhama vyama kwenda kuunga mkono juhudi za rais na ushenzi wa aina ile.

Kwanini waziri mkuu anataka kudhani hatuelewi anachomaanisha ni kwakuwa wapinzani waliunga mkono nyaraka zile kwa kuwa kilikuwa ni kilio chao kuhusu ushenzi ule. Walichofanya waoinzani ni kusimamia na kuunga mkono ukweli ulio ndani ya nyaraka zile ili wasitishwe na serekali yenye nia ovu kwani hata barua hizo zimetoka na ukweli kufahamika. PM anajikosha, ila ajue hao maaskofu sio wajinga kiasi hawajui ukweli wala nini wanasimamia mpaka waelekezwe na kikundi au taasisi toka nje yao. Kwa ujumla serekali imefumbia macho tabia mbovu ya viongozi wake waandamizi na ndio hapo hapo walipokutana na nguvu ya nyaraka za kitume, na uzuri maaskofu wamesimamia nguvu ya Mungu ambayo ni ukweli na sio hofu ya mamlaka za dunia.
 
Mimi kwa maoni yangu hatutafika popote kwenye hili maadamu watoa maamuzi wetu nao ni waumini wa hizi hizi Dini, tufanye kama Wazungu kama Viongozi wetu wanaona wanashindwa kudili na Viongozi fake wa Kidini wanaotumia Dini kwa manufaa yao Binafsi tukabidhi nchi au sehemu ya Serikali inayoadili na mambo ya Dini kwa mtu asiye na Dini kwa kipindi amalize huu mjadala, hili linawezekana na wapo wengi tu wanaoweza kuufunga kwa dakika sifuri!

Wazungu hutumia sana hii mbinu ndo maana hata USA wamemleta D. Trump ili aweke mambo sawa kwa maana wale wengine ni ,,wastaarabu" na waoga sana ona sasa anavyopambana kupunguza trade deficit ya USA kwa nguvu zote dadadeki na hakuna Maandamano USA kumpinga unafikiri ni kwa nini? wako pamoja naye, Ufilipino walimleta Duterte ili aondoe drug barons na kweli aliwamaliza hakusikia umoja wa Mataifa wala nini leo hii tatizo limepugua!

Hivyo hili linawezekana kabisa kama wenye Mamlaka wanawaonea haya viongozi wa kidini, wakabidhi watu ambao hawajali kwa muda, ili kuiokoa nchi yetu, kwani tuna Dini nyingi na kila mtu akitaka Dini isikilizwe hatuwezi kuwa na nchi tena!

Ww ni mfaidika wa hizi siasa za kishenzi za awamu hii zilizopelekea nyaraka zile za maaskofu. Na bahati nyaraka zile toka zimetoka tumeona nchi imerejea kwenye utulivu na ulevi wa madaraka upo likizo. Ww ndio ulikuwa ukishabikia yale matendo ya wapinzani kutekwa na hata ulishabikia sana Tundu Lissu kupigwa risasi kuonyesha kuwa ni muhusika wa jambo lile. Toka serekali imeonyesha kurudi nyuma na kuzikana barua zile za vitisho kupitia msajili wa vyama umekwazika kwani unaonyesha ww ni mmoja ya waratibu wa ukatili ndani ya nchi hii kwa kisingizio cha kuleta maendeleo na uzalendo wa jukwaani. Unaamini sana kwenye nguvu na nia ovu ya serekali dhidi ya wapinzani. Siku moja utajuta huu ukatili unaotambia leo.
 
Mbatia ni kiongozi wa dini hadi aulize swali Kwa niaba ya dini?

Akili halisi za kukimbizia mwenge. Unajua ni kwanini mnaishia kuongea upuuzi humu ndani? Mlikuwa mnashabikia serekali kuchafuliwa kwa kutumiwa na viongozi wachache waandamizi wenye ulevi wa madaraka. Matokeo yake viongozi wa dini wachache wakajitoa muhanga kuhoji tena kwa lugha kali ya kitume, na hadi sasa wamesimamia ukweli wao hata kama mamlaka inataka kuwatisha kupitia viongozi wale wale waovu.
 
Muulizeni Bakwata aliwaita wakafanyia mikutano ukumbi Gani? Kwani Bakwata ni Wabunge Mpaka wafanyie mikutano kwenye kumbi za Bunge?
 
Sasa watawazuiaje ? Au kama Nape alivyozuiwa siku ile ? tatizo kanisa halina akina yule jamaa aliyemtolea Nape bastola ...
 
Nawaasa viongozi wa dini msikubali kutumia makundi mengine nje ya taasisi zenu kwa ajili ya kuwazungumzia masuala yenu kwa sababu watawachonganisha na serikali ambayo haipo kwa ajili ya kugombana na taasisi yoyote,”Waziri Mkuu @kassim_majaliwa.

MY TAKE:
Hongera sana mheshimiwa waziri mkuu kwa hekima hii kwani taasisi hizi zilijengwa kwa jasho na damu hivyo anayetaka kuzitumia kwa maslahi yake kwa ajili ya kuvuruga amani na uhusiano uliopo ni lazima apingwe kwa njia yoyote ile.

Hakuna serikali inaweza kugombana na Taasisi ya Dini flani bali wapo vibaraka na makundi ndani ya taasisi hizo yanataka kuharibu uhusiano mwema kwa maslahi ya waliowatuma na kuwanunua.

Nchi hii ina misingi ya dini mbalimbali...yaani kwenye familia unakuta baba mkatoliki,mama mlutheri,mjomba answar,shangazi msabato,bibi hana dini,watoto ni Beyism...kwa hiyo hatutegemei ugomvi wa kidhehebu au kidini unaweza kuwa na afya.
Siasa ibaki kama Siasa na dini iende kwenye mimbari na madhabahuni.
Hivi viongozi wa vyama vya siasa siyo sehemu ya taasisi za dini? Maana nao wana dini zao, sasa wasizisemee wakati wanalelewa na taasisi hizo kiroho? Sielewi ni jinsi gani uwatenge viongozi wa vyama na taasisi za dini. Hata yeye ni kiongozi wa chama lakini pia ana dini yake
 
Back
Top Bottom