Waziri Mkuu ashuhudia Wazee wa Kimila wakila kiapo cha kumaliza mapigano Kiteto

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,280
25,858
Wazee wa makabila manne ya Wamasai, Wanguu, Wagogo na Wabarbaig Wilayani Kiteto mkoani Manyara wamechinja kondoo na kuku kuashiria kumaliza mapigano kati ya wafugaji na wakulima mbele ya Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Wilaya ya Kiteto ilikabiliwa na mapigano makali mwaka 2014 yaliyosababisha vifo vya watu na mifugo,majeruhi na uharibifu wa mazao. Waziri Mkuu amesema Serikali iko imara katika kulinda amani na utulivu nchini Tanzania. Kiapo hicho cha kimila kimefanyika katika msitu wa Paltimbo huko Kiteto,Manyara.

Chanzo : ITV Habari
 
Back
Top Bottom