Waziri Mkuu aagiza wananchi wasizuiwe kuonesha mabango

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,519
9,322
Kassim-Majaliwa.png

Sikonge/Dar. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaka mabango yanayoonyeshwa na wananchi kwa viongozi wa kitaifa wanapowatembelea yasiwe yanazuiwa kwa vile yanakuwa yanaelezea changamoto wanazokabiliana nazo.

Majaliwa alisema hayo baada ya kuona mabango yaliyoinuliwa na wananchi kwenye mkutano wake na wananchi mwishoni mwa juma lililopita mjini Sikonge mkoani Tabora huku wananchi hao wakitakiwa kuyashusha.

“Siku nyingine msirudie na kuanzia sasa waacheni wananchi waonyeshe mabango yao kwani ndiyo njia wanayotumia kuonyesha hisia zao kwa yale wanayokumbana nayo na kuwasababishia kero,” alisema Majaliwa.

Kutokana na hali hiyo, Waziri Mkuu aliwaagiza wasaidizi wake wayakusanye mabango yote wayaandike kisha wampelekee yaliyomo akiahidi kwamba atayafanyia kazi.

Alieleza kuwa malalamiko mengi kwenye mabango hayo yanahusu kero za vyama vya msingi vya ushirika na migogoro ya ardhi na kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri kutenga siku kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi huku akiwa na wakuu wa idara mbalimbali.

Hiyo siyo mara ya kwanza kwa wananchi kuinua mabango kwa viongozi wa kitaifa. Julai 22 huko Kigoma wakati wa ziara ya Rais John Magufuli, wananchi waliinua mabango yao ili ayasome huku wakizuiwa na walinzi.

“Waacheni, waacheni tu jamani…jamani mtulie nitayasoma yote. Nimeyaona yote ndiyo maana nayapitia na wasaidizi wangu wanayapiga picha nyinyi msiwe na wasiwasi,” alisema Rais Magufuli wakati akihutubia katika Uwanja wa Lake Tanganyika huku wananchi wakikazana kumwonyesha mabango yao.

Hali kama hiyo ilijitokeza tena huko Tabora Julai 23, wakati Rais Magufuli akiwahutubia wananchi na kuwataka washushe mabango yao kwa sababu wananchi walikuwa wakipiga kelele, jambo lililokatisha hotuba yake.

“Naomba myashushe mabango yenu ili niendelee na hotuba yangu,” alisema Rais Magufuli lakini wananchi waliendelea kuyainua juu, jambo lililoonyesha kumkera, “Nimesema shusheni hayo mabango, la sivyo siyashughulikii. Ukitaka hata ukayatandike kwenye kitanda cha mke wako, siyasomi.”

Akitoa maoni yake kuhusu vitendo vya wananchi kuinua mabango yao kwa viongozi wa kitaifa, Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Benson Bana alisema hiyo inaonyesha kukua kwa demokrasia nchini.

Alisema wananchi wanatafuta namna ya kufikisha ujumbe kwa viongozi wa kitaifa juu ya mambo ambayo Serikali za mitaa au mkoa zimeshindwa kukabilaiana nazo au wameshindwa namna ya kuwafikia.

“Huko ndiko kupevuka kwenyewe na kukua kwa demokrasia. Viongozi kwenye maeneo hayo wameshindwa kutatua kero za wananchi ndiyo maana wananchi wanaona bora watumie fursa ya kueleza kero zao kupitia mabango,” alisema.

Mwanazuoni huyo alisisitiza kwamba kuna haja ya kuimarisha mifumo ya mawasiliano kati ya wananchi na viongozi wao wa Serikali za mitaa mpaka mkoa ili kumaliza changamoto zao bila kuzifikisha kwa viongozi wa kitaifa.

“Viongozi wa mikoa wawe na mawasiliano ya karibu na wananchi, wawe wanajibu meseji zao na kuwafikia katika maeneo yao. Hiyo itasaidia kupunguza mabango kwa viongozi, japo siyo jambo baya pia kuinua mabango,” alisema.

Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi alisema kitendo cha wananchi kuonyesha mabango kwa viongozi kinaonyesha udhaifu wa Serikali katika kukabiliana na changamoto za jamii husika.

Alisema mara nyingi askari wamekuwa wakiwazuia wananchi kupaza sauti zao ndiyo maana nao wameamua kuja na mtindo wa kutumia mabango kufikisha ujumbe kwa viongozi wao wa kitaifa. “Katiba yetu inaruhusu uhuru wa kutoa maoni bila kujali kwamba yatawafurahisha au kuwakera viongozi. Askari wasitumie nguvu kuwanyamazisha wananchi kwa sababu ni haki yao ya msingi,” alisema Muabhi.

Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu) alimpongeza Waziri Mkuu kwa kutambua umuhimu wa sauti ya umma na kusisitiza kwamba hiyo ni njia moja wapo ya kufikisha ujumbe kwa wananchi.

Alisema siyo jambo baya kwa wananchi kuinua mabango yao kwa viongozi kwa sababu wakati mwingine wanawakumbusha juu ya mambo ambayo wanatakiwa kuyafanyia kaz

Chanzo: Mwananchi
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaka mabango yanayoonyeshwa na wananchi kwa viongozi wa kitaifa wanapowatembelea yasiwe yanazuiwa kwa vile yanakuwa yanaelezea changamoto wanazokabiliana nazo.

Majaliwa alisema hayo baada ya kuona mabango yaliyoinuliwa na wananchi kwenye mkutano wake na wananchi mwishoni mwa juma lililopita mjini Sikonge mkoani Tabora huku wananchi hao wakitakiwa kuyashusha.
“Siku nyingine msirudie na kuanzia sasa waacheni wananchi waonyeshe mabango yao kwani ndiyo njia wanayotumia kuonyesha hisia zao kwa yale wanayokumbana nayo na kuwasababishia kero,” alisema Majaliwa.

Kutokana na hali hiyo, Waziri Mkuu aliwaagiza wasaidizi wake wayakusanye mabango yote wayaandike kisha wampelekee yaliyomo akiahidi kwamba atayafanyia kazi.
Alieleza kuwa malalamiko mengi kwenye mabango hayo yanahusu kero za vyama vya msingi vya ushirika na migogoro ya ardhi na kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri kutenga siku kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi huku akiwa na wakuu wa idara mbalimbali.

Hiyo siyo mara ya kwanza kwa wananchi kuinua mabango kwa viongozi wa kitaifa. Julai 22 huko Kigoma wakati wa ziara ya Rais John Magufuli, wananchi waliinua mabango yao ili ayasome huku wakizuiwa na walinzi.
“Waacheni, waacheni tu jamani…jamani mtulie nitayasoma yote. Nimeyaona yote ndiyo maana nayapitia na wasaidizi wangu wanayapiga picha nyinyi msiwe na wasiwasi,” alisema Rais Magufuli wakati akihutubia katika Uwanja wa Lake Tanganyika huku wananchi wakikazana kumwonyesha mabango yao.

Hali kama hiyo ilijitokeza tena huko Tabora Julai 23, wakati Rais Magufuli akiwahutubia wananchi na kuwataka washushe mabango yao kwa sababu wananchi walikuwa wakipiga kelele, jambo lililokatisha hotuba yake.
“Naomba myashushe mabango yenu ili niendelee na hotuba yangu,” alisema Rais Magufuli lakini wananchi waliendelea kuyainua juu, jambo lililoonyesha kumkera, “Nimesema shusheni hayo mabango, la sivyo siyashughulikii. Ukitaka hata ukayatandike kwenye kitanda cha mke wako, siyasomi.”

Akitoa maoni yake kuhusu vitendo vya wananchi kuinua mabango yao kwa viongozi wa kitaifa, Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Benson Bana alisema hiyo inaonyesha kukua kwa demokrasia nchini.
Alisema wananchi wanatafuta namna ya kufikisha ujumbe kwa viongozi wa kitaifa juu ya mambo ambayo Serikali za mitaa au mkoa zimeshindwa kukabilaiana nazo au wameshindwa namna ya kuwafikia.

“Huko ndiko kupevuka kwenyewe na kukua kwa demokrasia. Viongozi kwenye maeneo hayo wameshindwa kutatua kero za wananchi ndiyo maana wananchi wanaona bora watumie fursa ya kueleza kero zao kupitia mabango,” alisema.
Mwanazuoni huyo alisisitiza kwamba kuna haja ya kuimarisha mifumo ya mawasiliano kati ya wananchi na viongozi wao wa Serikali za mitaa mpaka mkoa ili kumaliza changamoto zao bila kuzifikisha kwa viongozi wa kitaifa.

“Viongozi wa mikoa wawe na mawasiliano ya karibu na wananchi, wawe wanajibu meseji zao na kuwafikia katika maeneo yao. Hiyo itasaidia kupunguza mabango kwa viongozi, japo siyo jambo baya pia kuinua mabango,” alisema.
Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi alisema kitendo cha wananchi kuonyesha mabango kwa viongozi kinaonyesha udhaifu wa Serikali katika kukabiliana na changamoto za jamii husika.

Alisema mara nyingi askari wamekuwa wakiwazuia wananchi kupaza sauti zao ndiyo maana nao wameamua kuja na mtindo wa kutumia mabango kufikisha ujumbe kwa viongozi wao wa kitaifa. “Katiba yetu inaruhusu uhuru wa kutoa maoni bila kujali kwamba yatawafurahisha au kuwakera viongozi. Askari wasitumie nguvu kuwanyamazisha wananchi kwa sababu ni haki yao ya msingi,” alisema Muabhi.

Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu) alimpongeza Waziri Mkuu kwa kutambua umuhimu wa sauti ya umma na kusisitiza kwamba hiyo ni njia moja wapo ya kufikisha ujumbe kwa wananchi.
Alisema siyo jambo baya kwa wananchi kuinua mabango yao kwa viongozi kwa sababu wakati mwingine wanawakumbusha juu ya mambo ambayo wanatakiwa kuyafanyia kazi
 
Alisema hayo mjini sikonge mkoani tabora.
Alipoona viongozi wakiwaamuru wenye mabango wayashushe, aliwaamuru viongozi hao wayakusanye na wanakili maandishi yaliyomo kwenye mabango wampelekee ili yafanyiwe kazi. Kwani kwenye mabango ndipo wananchi hutoa hisia zao.
IMG_20170814_113904.jpg
 
Majaliwa namuelewa sana sometimes naoona ndo kama yeye ndo Raisi.
Busara ni kitu cha bure hakiwezi kununuliwa.
Wengine walipoona hayo mabango waliambiwa wakatandikie kwenye vitanda vyao walalie na wake zao

What goes around always comes around
 
Makonda Na Gambo Ndyo Wenye Kauli Zenye Ngvu Wengne Waliobaki Ukimtoa Sizonje,ni Maigizo Tu
 
kitendo cha wananchi kuitumia hii njia kwa wingi kunaonyesha kukata tamaa au uaminifu na wasaidizi wa rais aliyewateua,pale pana utitiri wa viongozi kuanzia RC,mbunge etc etc but why wananchi hawa hawapeleki malalamiko yao kwao?why wanasubiri hadi viongozi wa kitaifa wawatembelee ndio waonyeshe mabango yenye malalamiko?ingekuwa rahisi kwenda kuwaona wahusika moja kwa moja,mfano suala la ardhi kuna viongozi wengi wa kushughulikia tatizo hili katika ngazi ya wilaya hadi mkoani mbona wananchi hawapeleki kule,?itabidi national leaders kwanza warekebishe hili kwanza,na mbaya zaidi wengi sio wataalam they are just cadre deployed.
 
Wakati Magufuli Aliwaambia Wakayatandike Walalie Majumbani Mwao
 
Hapa naona mtu anatafuta kutumbuliwa. Kupishana kauli na boss wako ni utovu wa nidhamu na tena kwa boss kama huyu dawa ni kukutumbua tu. Benson Bana ni Dr mjinga sana, eti kuonysha ukomavu wa Demokrasia!! Huyu kama ana watoto naona kama anawadhalilisha tu
 
ameongea kwa busara na hekima hata asipoenda kuyafanyia kazi yote ila mwananchi kaona kiongozi wake kamjali
 
Tatizo la nchi hii ni Magufuli tu, lakini hawa viongozi wengine wakuu kama Waziri mkuu Majaliwa na Makamu wa Rais hawana tatizo kabisa.
Mkuu unaweza kuwa sawa kwa upande mmoja wa shilingi lakini upande wa pili mpe kijiti aongoze nchi utasema huyu sio yule Majaliwa ukandamizaji na uvunjifu wa sheria na katiba kwa kwenda mbele ccm wasikie hivyo hivyo.
 
Ipo siku tutalala tukiamka itakua habari mbaya sana...
Kumpinga dereva wa Lori yataka moyo

Psalm 133:1 "Behold, how good and how pleasant it is for brethren to dwell together in unity."
 
Back
Top Bottom