Waziri Mkulo na matusi kwa mtangazaji wa redio

Waziri aliyepewa dhamana na rais kupitia kwa wananchi wa jimbo la kilosa alimtukana mtangazaji wa wako redio wakati alimpomhoji maswala ya DECI. Alimtukana stupid na shenzi live redioni wakati anasikilizwa na watanzania wote.

Huyo ndiye Waziri wa Fedha, nani kampa jeuri hiyo?

Historia inaonyesha kuwa ndio kiburi yake hasa anapokuwa na madaraka. Wafanyakazi waliofanya nae kazi kote alikopita wanasema ndo hulka yake na kiburi

Je nani kampa hiyo jeuri ya kutukana!?

Ni rais au pesa?


Ni hali ya kibinadamu(udhaifu wa kibinadamu). Nadhani alikuwa na jazba na hasira. Naamini kila mtu ameshawahi kupitiwa bahati mbaya akatukana.

Naamini mheshimiwa Mkullo alijuta baadae nafsini kwa hilo. Ila kwa vile hatuna staili ya kuomba radhi ni hivyo tena. si unajua mi mkubwa(madaraka). Naamini angeomba radhi hata kwa mwandishi mwenyewe.

Mtazamo wangu binafsi!
 
Mtu kama huyu ni waandishi wa habari wanaweza kumuadabisha kwa kuifanya hiyo video clip or audio clip kajitangazo kadogo. Wakiweke kila baada ya nusu saa kwa mwezi mzima labda ataona aibu na kujiuzuru, ila tatizo kwenye resiponsibilities issue hatuwaigi waingereza kwenye hilo ila kwenye matanuzi tunajiweka at their level mpaka malipo ya wabunge tunawakaribia.
 
Apparently Huyu ni mmoja wa watu wachache wanaozaliwa na kijiko cha fedha midomoni mwao.Huyu amebahatika kuwa sehemu nzuri tokea aanze kazi na mwishoni baada ya kustaafu akabahatika kurudi tena uwanjani kikubwa - uwaziri.

Ni bahati mbaya sana kama ameweza kutukana maana nimjuavyo ni mtu pleasant mwenye kutabasamu wakati wote.

Hili la DECI nadhani linamshtua ukiangalia kasheshe iliyotokana na sakata hili na hata yeye kidogo auingie mkenge kuizundua jimboni mwake huko Kilosa. Huyo mtangazaji kumuuliza kuhusu DECI ni kama kuongeza chumvi kwenye kidonda.

Nakubaliana nawe dada but ndo yamtoke matusi?..... He could behave better than that!
 
ili kujua kuwa jamaa ni pumba hebu ona Bajeti yake ya kibabe kwa mashirika ya dini imepigwa mweleka.Aibuuuuuuuuuuuuu pamoja na kujieleza na kusigina madhehebu ya kikristu pekee(asivokuwa makini) lakini mwisho wa yote Kijana wa mkulima(Mizingo kayanza Pinda) kwa busara zake alizopewa na Allah amekaa na wadau wenyewe na kuyamaliza kiutu uzima.Hili limkulo bado toto la kijiweni haliwezi kukaa na watu wastaarabu kama viongozi wa dini na kuongea nao.Halina mvuto kwa watu wastaarabu.
 
Nakubaliana nawe dada but ndo yamtoke matusi?..... He could behave better than that!

Ni ubabe ubabe tu wa viongozi wetu walio wengi... kwani nina amini hayo maswali aliyoulizwa iwapo angeulizwa na chombo kama CNN au BBC maswali hayo hayo akiwa nje ya nchi au hata akiwa hapa hapa Bongo asingejibu kinamna hiyo, au basi angenyamaza kimya badala ya kumfyatukia anayemhoji.

Swala hili linaelezea aina moja ya dharau zilizokithiri dhidi ya wenyewe kwa wenyewe zinazo didimiza bara letu la Afrika.
 
sio ulevi wa madaraka tu,pia ni ujinga uliopitiliza wapo wengi wanaoamini wao ndio cream ya Bongo
 
Dr dau hakuleta jipya pale NSSF yote yalianzniashwa na mhishimiwa sana mjinga,stupid mkulo dau aliyakuta.Waulizeni wakubwa walokuwa na mkulo pale nssf na sasa wako na dau.Tatizo la mkulo ni matusi pamoja na tabasamu ila mdomo wake umejaa matusi kwa wa chini yake.Alipoondolewa nssf alipauka hadi tukadhani tayari!!!! sasa ushikaji umemsaidia hadi kuwa waziri.Tanzania yetu hiyo hahahahahahahaaaaaaaaaaaa.Unakumbuka JK aliulizwa swali wakati alipopata Urais kuwa itakuwaje kwa wale washkaji wake walokuwa kijiweni akasema atakuwa anachati nao katika simu,ndo hiyo simu hadi uwaziri,hahahahahaaaaaaaaaa

Lete data na facts kuback up arguments zako..issues kama mapato na mengineyo ndio tutajua who did what
 
Ni ubabe ubabe tu wa viongozi wetu walio wengi... kwani nina amini hayo maswali aliyoulizwa iwapo angeulizwa na chombo kama CNN au BBC maswali hayo hayo akiwa nje ya nchi au hata akiwa hapa hapa Bongo asingejibu kinamna hiyo, au basi angenyamaza kimya badala ya kumfyatukia anayemhoji.

Swala hili linaelezea aina moja ya dharau zilizokithiri dhidi ya wenyewe kwa wenyewe zinazo didimiza bara letu la Afrika.

umesahau kama ana degree feki?
 
Duh Bongo bwana tutaendelea kusubili huyu huyu akirudi kwao kule wanampokea kama mfalme sisi watanzania bado tunasafari ndefu...kwa jamaa anajiona na hicho kicheo cha uwaziri atakuja pigwa chini mpaka afulie kabisa.
 
na nyie waandishi muwe mnauliza vitu vinavyoendana na wakati,mtu yupo kwenye masuala ya bajeti we unamletea masuala ya deci,na unajua huku nako kalikoroga we ulitegemea nini na unabahati anapigaga vibao
 
Huyo mtangazaji anatakiwa aende mahakamani kwa kutukanwa na pia alipwe fidia kwa radio husika, na pia Mkullo amedanganya hata kwenye bajeti yake kuhusu Taasisi za Dini kulipa Kodi sasa tushike ya nani??
 
Alimtukana stupid na shenzi live redioni wakati anasikilizwa na watanzania wote.

Huyo mtangazaji atakuwa stupid kweli kama hakuchangamkia ulaji huu na kubaki kulalama humu kwenye jamvi! Ushahidi anao. Anangoja nini?

Amandla.......
 
Anaweza kushitakiwa na kulipa fidia kwa kumdhalilisha mtangazaji akiwa kazini kama vile yeye akiwa pale wizarani halafu aje mtu amuulize kitu amtukane......anastahili kupelekwa mahakamani akalipe fidia ...................kwa kudhalilisha..tena kwa umma....sijui mnawatoa wapi watu kama hawa....ambao hawajui..............hata nini maana ya madaraka
nakubaliana na wewe kama ushahidi upo, huyo mwandishi ashauriwe amshitaki!
 
na nyie waandishi muwe mnauliza vitu vinavyoendana na wakati,mtu yupo kwenye masuala ya bajeti we unamletea masuala ya deci,na unajua huku nako kalikoroga we ulitegemea nini na unabahati anapigaga vibao

Huu ukiritimba na Orwellian control ya kuamua nini kitaulizwa wapi unatoka wapi? Hawa si public servants?

Jana asubuhi nilimsikiliza Senator Dick Lugar anaongea na CBS kuhusu Iran, anajibu maswali kwa heshima sana na mwisho wa mahojiano akasema "Thank you sir" yani unaona huyu mtu anaelewa kwamba yeye ndiye mtumishi wa watu, na wala si bwana mkiritimba.

Sasa mtu kama huyo mara nyingi anaweza kuulizwa maswali asiyajibu kwa ufasaha, au kuyaruka kabisa kwa kujiuliza maswali yake na kuchomeka talking points katika fashion yao ya kusema "the question is ...." halafu ana hijack mazungumzo, lakini unaona kabisa hii ni political tact, na kwa kweli si kila swali linaweza kujibiwa openly.

Lakini the Mkulos of this world wanaonyesha sio tu kwamba hawaelewi au kukubali kwamba wao ni watumishi, na sio tu kwamba wana dharau iliyokubuhu, bali pia kwamba hawana akili ya kuweza kukwepa maswali na kupiga spin za "the question is ...."

Yaani watanzania wanakosa bread hilo washakubali, basi hata hiyo circus nayo iwe this bad?
 
Back
Top Bottom