Waziri Mkenda, ameteua kamati ya mpito kusimamia Shughuli za Skauti Nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf Mkenda ambaye pia ni Rais wa Skauti ameteua kamati ya mpito ya watu watatu kusimamia shughuli za kiutendaji za Skauti nchini na Uchaguzi.

Waziri Mkenda ameteua kamati hiyo leo tarehe 18 Machi 2022 Jijini Dar es salaam wakati wa kikao kazi na kamati tendaji ya Skauti ambapo pia katika Kikao hicho alishiriki Skauti Mkuu Bibi Mwantumu Mahiza .

Wajumbe wa Kamati hiyo teule ni Bw Stewart Kiluswa, Omary Mavura pamoja na Suleiman Takadiri ambao wamepewa jukumu la kuhakikisha inaandaa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa uongozi wa Skauti

Waziri Mkenda ameitaka kamati hiyo ya mpito kuhakikisha kuwa inatoa Notisi ya Mkutano ifikapo tarehe 21 Machi 2022 huku akiagiza mkutano mkuu kufanyika ndani ya siku 60 baada ya tangazo hilo.
IMG-20220318-WA0037.jpg
IMG-20220318-WA0040.jpg
IMG-20220318-WA0036.jpg
 
View attachment 2155777View attachment 2155778View attachment 2155779
 
Kuuliza si ubaya... Skauti wana kazi gani? Je, ukiweka na JKT Mujibu kwenye picha mbona kama hakuna muendelezo??
 
Back
Top Bottom