Naibu Waziri Khamis Hamza: Serikali Kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa Kusimamia Taka Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo imeibua miradi ya kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia taka nchini.

Amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mikakati ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira kwenye mito na mifereji katika jiji la Dar es Salaam, mafanikio na changamoto kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma leo Oktoba 23, 2023.

Mhe. Khamis amesema Serikali ilitoa mwongozo wa usafishaji mito kwa lengo la kuondoa taka ngumu, mchanga na tope kwa mito ya Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza madhara yanayoweza kutokea kutokana na uchimbaji holela wa mchanga katika mito hiyo.

Amesema katika utekelezaji wa Mwongozo, usafishaji ulianza katika mito mitano na hadi sasa jumla ya mito tisa mkoani humo ikiwemo Msimbazi, Mbezi, Tegeta, Nyakasangwa, Mpiji Luhanga, Kibangu, Kibwegere na Kigori imeanza kusafishwa.

Aidha, Naibu Waziri Khamis ametaja mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa mikakati ya kukabiliana na uchafuzi wa mito na mifereji kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa usafi wa mito katika maeneo ya jiji ambapo jumla ya urefu wa eneo la mito lililosafishwa ni takribani mita 99,677 ambapo wakandarasi wamesafisha mita 41,150 na vikundi vya machepe mita 58,527.

Pia, amesema uimarishaji wa kingo za mito ambapo miti rafiki kwa mazingira 24,000 imepandwa katika maeneo mbalimbali kama vile mto Msimbazi eneo la Pugu Station, Mto Mpiji maeneo ya Mgemuzi, Mabwepande Mitiki na Mbweni.

Dar es Salaam ni mojawapo ya majiji makubwa likiwa na jumla ya watu milioni tano kwa mujibu wa Sensa mwaka 2022, ongezeko likiambatana na shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa changamoto za kimazingira ikiwemo uchafuzi unaotokana na taka ngumu na taka maji.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni uzalishaji wa taka ngumu ni wastani wa tani 4,161 kwa siku ambapo kati ya hizo, uwezo wa Halmashauri kukusanya taka ni asilimia kati ya 45 hadi 50 tu.


395407485_18055792984485070_8821352844939281925_n.jpg
395404850_18055792993485070_2672288087449286575_n.jpg
395412403_18055793002485070_8791308758967586121_n.jpg
395407744_18055793014485070_1865154606491014879_n.jpg
395422658_18055793023485070_8976885279864327620_n.jpg
 
Back
Top Bottom