Ngalikivembu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,959
- 874
Nampongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni. Tarehe 20. November 2015 alipolihutubia bunge aliahidi kutumbua majipu. Alisema amejipa kazi ya kutumbua majipu. Tumeona anatekeleza ahadi hii.
Kwenye utumishi kulioza sana. Nampongeza kwa tumbua tumbua hii. Waziri wake wa ujenzi na mawasiliano anafanya kazi nzuri. Na hakika tunajua sisi watumishi wa umma tulilala lakini pia tulikuwa tuna hujumu nchi kwa ufisadi.
Tangu aletwe wizara hii Mbarawa ameshatumbua majipu kadhaa kama kumtoa mkurugenzi mkuu wa tcaa na waandamizi wake.
Lakini leo ninachomwomba ni kutupia jicho wale waliohusika kununua rada ya hali ya hewa ambayo imefungwa huko mwanza yapata miaka miwili imepita sasa.
Cha kusikitisha ni kuwa rada hii haifanyi kazi na majibu ya wahusika wanasema hatuna umeme wa kutosha kuendesha mitambo hii. La ziada hatuna wataalamu kuendesha rada hii. Sasa maswali ni haya kabla ya kununua hawakuliona hili? Hawakujua kama hawana wataalamu? Billion 7 zimetumika kununua rada hii. Waziri Mbarawa ameenda mara mbili huko mwanza tulitegemea angeelezwa hili tatizo. Hebu jaribu kurudi huko kupata majibu ya maswali haya. Tumbua jipu hili.
===============
UPDATE Kutoka TMA
===============
Tafadhali husika na somo tajwa hapo juu na taarifa inasambaa kwenye mitandao ya kijamii
Mamlaka inapenda kukanusha taarifa zinazosambaa kuhusu kutokufanya kazi kwa Rada ya Hali ya Hewa iliyopo Mwanza. Taarifa sahihi ni kwamba Rada hiyo inafanyakazi kama ilivyopaswa vilevile tunapenda kuutarifu umma wa watanzania kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa ina wataalamu wa kutosha wa kuendesha Mitambo ya RADA za hali ya hewa tulizanazo. Aidha gharama halisi za ununuzi wa Rada hiyo si kama bilioni 7 kama ilivyosambazwa.
Kwa taarifa hiyo fupi, tunapenda kuisihi jamii kuacha kuichafua Mamlaka na Serikali kwa ujumla kwa taarifa zisizo rasmi zenye upeo hasi na pindi wanapohitaji kupata taarifa sahihi wasisite kuwasiliana na Ofisi zetu.
Tunawatakia kazi njema katika ujenzi wa Taifa.
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI,UCHUKUZI NA MAWASILIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA

TAARIFA KWA UMMA
YAH: UFANISI WA RADA YA HALI YA HEWA MWANZA