Profesa Ndakidemi aitaka TMA ishushe huduma za Hali ya hewa hadi ngazi ya Kanda, Mikoa na wilaya

Jun 20, 2023
74
94
Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini(CCM), Profesa Patrick Ndakidemi, ameitaka mamlaka ya Hali ya hewa nchinj(TMA) kusogeza huduma za Hali ya hewa hadi kupeleka watendaji kuanzia ngazi za Kanda, Mikoa na wilaya ikiwa ni mkakati wa kuboresha huduma za mamlaka na Kwa wananchi kwa ujumla.

Profesa Ndakidemi alikuwa aliuliza swali kwa wizara ya uchukuzi Bungeni mjini Dodoma jana ambako pia alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuboresha utendaji kazi wa TMA ili kuweza kutoa utabiri sahihi.
Katika maswali yake mawili ya nyongeza Profesa Ndakidemi alihoji ni je serikali haione haja ya kutumia simu ya viganjani kuwatumia wananchi taarifa za Hali tete za hewa Katika maeneo husika.

Akijibu swali Hilo,Naibu wazori wa uchukuzi, Davis Kihenzile alisema Katika Mwaka wa fedha wa 2024/2025 serikali imetenga shilingi Bilioni 13 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa rada, vifaa na miundombinu ya Hali ya hewa ikiwamo ufungaji wa rada mbili za hali ya hewa Katika Mikoa ya Mbeya na kigoma.

Naibu Waziri Kihenzile alisema serikali pia imeingia mkataba wa kununuq rada mbili kwa ajlli ya mikoa ya Dodoma na Kilimanjaro na hivyo kufikisha lengo la kuwa na rada Saba kwa nchi nzima.

Katika majibu yake wa Profesa Ndakidemi, mheshimiwa Kihenzile alisema TMA imeingia mkataba wa kununua mitambo ya kisasa ya kuandaa utabiri wa Hali ya hewa ambayo itaimarisha uwezo wa kupokea data za Hali ya hewa, picha za satelaiti, kuchakata na kuchapisha kidijitali matokeo ya utabiri wa hali ya hewa.

"Mheshimiwa Spika,TMA imenunua mitambo mitatu ya uangalizi wa hali ya hewa Katika pwani ya bahari ya Hindi ambayo itafungwa Katika pwani ya Zanzibar na Bagamoyo na hivyo kuongeza huduma za Hali ya hewa Katika uchumi wa bluu"

"Aidha mitambo 15 ya kupima Hali ya jewa mahususi Katika sekta ya kilimo imeshanunuliwa na itafungwa Katika maeneo mbali mbali hapa nchini"

Alisema jumla ya mitambo 10 ya kupima ya Hali inayojiendesha yenyewe imepokelewa ambapo mitambo mitatu imefungwa Katika vituo vya Hali ya hewa vilivyopo Mtwara, Songoe na Arusha na kuongeza maandalizi ya ufungaji wa mitambo Saba inaendelea.

"Mheshimiwa katika kuboresha utendaji kazi wa Hali ya hewa, serikali imeajiri watumishi wapya 31 wa kada tofauti na kuwapangia Katika vituo vya Hali ya hewa nchini na hivyo kuimarisha uwezo wa TMA Katika kuendelea kutoa huduma Bora nchini"

Mheshimiwa Kihenzile alisema serikali imeendelea kuimarisha shughuli za mamla ya Hali ya hewa kwa kujenga ofisi ya TMA ya kanda ya mashariki na kituo cha tahadhali ya Tsunami Jijini Dar es salaam.

Uta
 
Prof asubiri pensheni ya ubunge akapumzike sasa. Huku jimboni Barabara hazipitiki yeye anaulizia hali ya hewa?
 
Af TMA HAWA WAMEKUWA WARASIMU SANA WAMEHODHI SANA YAANI INAFIKIA HATUA HATA KITUO CHA RAINFALL HUWEZI KUANZISHA MPAKA UWA CONSULT SIO SAWA BANA WAPENI HATA MA MAMLAKA YA MABONDE WAWE HURU KIDOGO KUFANYA KAZI ZAO ZA HYDROMETEREOLOGY
 
Back
Top Bottom