Waziri Mathias Chikawe: Hakuna watanzania waliohusika kashfa ya BAE!

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,507
11,883
Wabunge wamekomaa mheheshimiwa membe awataje wahusika rushwa ya rada!eti wahusika hawajulikani huku tunadai chenji
Waziri Mathias Chikawe amemtetea anasema hakuna ushahidi, akaendelea kwamba kama kuna mtu yeyote ndani na nje ya Tanzania mwenye ushahidi 'concrete' aulete; anasema sio ushahidi wa kwenye magazeti.
 
Mkuu hapo kwenye kusema mwenye ushahidi alete wakati tunavyombo mahsusi kwa ajili ya upelelezi huwa pananitia kichefuchefu sana kwani vyombo vetu vya police,usalama wa taifa au takukuru kazi yake nini kama wanataka ushahidi toka kwa wananchi hii Mungu tuondolee hii mijitu imeshiba rushwa na wizi hata wanashindwa kutambua wajibu wao
 
Lakini Jk si kashasema Isue ya rada hakukuwa na rushwa?
sasa watakaotajwa hapo ni akina nani tena?
 
Mimi Namsaidia kuwataja
1. Andrew Chenge
2. Dr. Idrissa
3. Vithlan
4. ..........

Kama mnasubiri haya magamba yawataje mta kesho. Kumbuka kesi ya Tundu Lissu na wabunge wala Rushwa.
 
Sasa kama hakukuwa na rushwa yule muhindi Shailesh P Vithlani nini kilichomfanya aikimbie nchi na hatimaye kuwekwa katika "wanted list" ya Interpol? Na vile vijisenti vilivyokutwa kwenye bank accounts za Chenge na Idissa Rashid nchi za nje ambavyo vilisemekana vilitokana na malipo toka kwenye bank account ya Vithlani ni nani anayeweza kuvitolea maelezo ya kuridhisha kwamba havikutokana na rushwa ya ununuzi wa rada? Wahusika wa rushwa katika manunuzi yale ni Mkapa, Mramba, Vithlani, Chenge, Idrissa Rashid na wengineo wengi ambao Serikali imeamua kuwakingia kifua.

The former Attorney General and cabinet minister, Andrew Chenge, is among senior public officials investigated for allegedly receiving kickbacks to endorse the sale. A local businessman, Tanil Somaiya and his trading partner Shailesh P. Vithlani, who is wanted by the Interpol over the dubious deal, were also named in the SFO report.

This excerpt is from Daily News dated 18th August 2010
 
Sio Werema ni Mathias Chikawe! Kwa maneno ya Chikawe du,hii ni dharau kwa Membe. Hivyo Membe won't mention anyone though it's obvious.

Ni kweli Mkuu. Nilivyotafsiri mimi kwenye kauli ya Chikawe ni kama amem pre empty Membe ambaye kulikuwa na dalili za Membe kuwataja
 
Membe amekwepa kuongelea suala la radar. Amesema 'waziri mwenzangu amesema na ninyi wahe. Wabunge mkashangilia'. Amemwambia Wenje waonane kesho
 
Asiishie hapo tu aseme na pesa za walibya zimeenda wapi? anaposema zipo TIB bank ni majibu ya ubabaishaji lengo lilikuwa kujenga kiwanda cha cement mkoani Lindi kitu ambacho hakijafanyika mpaka leo.Membe fisadi tu amepora pesa za walibya.
 
Pesa za waliby zipo mzeiya..nyngne Membe alimpa yule mwekezaji wa kiwanda cha Cement,walibya hawataki riba...
 
na nyie mnawaendekeza tu.. waacheni.. kadizoo!!! kama hakuna si hakuna. Waondoeni madarakani ili tuje kuwashughulikia. Mmesahau kuwa panya hawakamatani na pia hawatajani?
 
Sasa kama hakukuwa na rushwa yule muhindi Shailesh P Vithlani nini kilichomfanya aikimbie nchi na hatimaye kuwekwa katika "wanted list" ya Interpol? Na vile vijisenti vilivyokutwa kwenye bank accounts za Chenge na Idissa Rashid nchi za nje ambavyo vilisemekana vilitokana na malipo toka kwenye bank account ya Vithlani ni nani anayeweza kuvitolea maelezo ya kuridhisha kwamba havikutokana na rushwa ya ununuzi wa rada? Wahusika wa rushwa katika manunuzi yale ni Mkapa, Mramba, Vithlani, Chenge, Idrissa Rashid na wengineo wengi ambao Serikali imeamua kuwakingia kifua.

The former Attorney General and cabinet minister, Andrew Chenge, is among senior public officials investigated for allegedly receiving kickbacks to endorse the sale. A local businessman, Tanil Somaiya and his trading partner Shailesh P. Vithlani, who is wanted by the Interpol over the dubious deal, were also named in the SFO report.

This excerpt is from Daily News dated 18th August 2010
Mkuu huyo Mhindi hakukimbia nchi bali ni Serikali iliyokula njama za kumtorosha kwa kuhofia kutaja wahusika waliojificha mithili ya Mbuni.Wameficha vichwa ili hali viwiliwili vikionekana.
 
CHAVDA,VITHLANI,BALALI wamefichwa wasiwataje mafisadi!Jeetu PATEL aligoma na kesi anashinda
 
Haya ndiyo matatizo ya watawala kudai na kujiona wana uwezo wa kuendelea kuwadanganya Watanzania. Hebu fikiria Mzee wa Vijisenti alivyojibu kuwa ana ng'ombe wenye kuweza kupata Dollar milioni? Kazi yao kubwa ni kulindana tu.
 
Hebu wana Jf tujaribuni kuchambua maelezo yaliyo tolewa na muheshimiwa Chikawe kuhusu sakata la rada kwa siku ya jana na leo alipokuwa ana jibu swali la muheshimiwa Mnyika.
 
Mkuu hatufiki popote. Ila isikupe presha kwa sasa. Mambo ya kulindana yana mwisho wake. Hata wengine.....waliwahi kulindwa lakini ikafika kipindi tukawasepesha.

Lets keep insisting.........:israel::israel:
 
Ni kweli mkuu tuwekeni nia ili kwa kutumia sanduku la kura tuondoe wote wanao kula na wanaowajua watuhumiwa lakini wana wafunika kwa shuka jeupe let do it tanzanian tuonyesheni nguvu zetu kwa hawa mchwa wala nchi yetu
 
Back
Top Bottom