Waziri Masauni: Serikali haiwezi kukaa kimya wakati wananchi wanauawa. Aunda kamati kuchunguza matukio ya mauaji nchini

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,548
142,828
Waziri wa mambo ya ndani mh Masauni amesema amewasikia kupitia mitandaoni mzazi wa polisi aliyefia mahabusu Mtwara na wazazi wa watu waliopotea Dar es salaam wakitoa malakamiko yao, na ameahidu kulifuatilia suala hilo kwani Serikali haiwezi kukaa kimya wakati wananchi wanapoteza maisha.

Masauni amewataka polisi kuwasaka wauwaji wote ambao taarifa zao zimeripotiwa polisi ili sheria ichukue mkondo wake.
------
masauni.jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni akiwa na watendaji wa ngazi za juu wa Jeshi la polisi nchini.

WIZARA ya mambo ya ndani ya nchi imeunda kamati ya kuishauri Serikali kuhusu namna ya kufanya katika kupata suluhisho la kudumu katika kuzui uhalifu na mauaji yaliyokithiri nchini huku ikitoa siku 21 kukamilisha kazi yake na kurudisha mrejesho kwenye wizara hiyo.

Hatua hii imekuja zikiwa zimebakia siku mbili tu mara baada ya Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdory Mpango kutoa siku saba kwa Jeshi la polisi nchini na idara zake zote kutafuta ufumbuzi wa mauaji yanayoendelea nchini

Hayo yameelezwa leo Januari 31,2022 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni wakati akiongea na waandishi wa habari Jijini Dodoma mara baada ya kikao chake na uongozi wa ngazi ya juu wa Jeshi la polisi ili kutoa mrejesho wa matokeo ya kilichojadiliwa kuhusu kadhia ya matukio ya mauaji yanayoendelea nchini.

Amesema kuundwa kwa kamati hiyo kutasaidia kupatikana kwa suluhisho la kudumu katika kuzuia mauaji na uhalifu mwingine nchini huku akitaka watanzania kutoa ushirikiano katika kuwabaini wahalifu.

Masauni amesema,kamati hiyo itahusisha jopo la wataalam kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Wizara ya mambo ya ndani ya nchi,Tamisemi,Jeshi la polisi,Ofisi ya wakili mkuu wa Serikali,Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali,Usalama wa Taifa,Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka,Takukuru,Wizara ya habari na elimu ya juu.

Sambamba na hayo ameeleza kuwa kutokana na kukithiri vitendo vya mauaji nchini hadi sasa Jeshi la polisi linawashikilia watu zaidi ya 150 huku akitaja mikoa vinara kwa mauaji kuwa ni Kagera, Dodoma,Mara ,Songwe na Kigoma.

Ametaja sababu mbalimbali za mauaji hayo kuwa ni pamoja na imani za kishirikina,wivu wa mapenzi,wivu wa maendeleo,visasi,migogoro ya ardhi,mali na ulevi na kueleza kuwa Serikali haiwezi kukaa kimya na kudharau malalamiko ya wananchi .

Chanzo: Malunde
 
Waziri wa mambo ya ndani mh Masauni amesema amewasikia kupitia mitandaoni mzazi wa polisi aliyefia mahabusu Mtwara na wazazi wa watu waliopotea Dar es salaam wakitoa malakamiko yao, na ameahidu kulifuatilia swala hilo kwani serikali haiwezi kukaa kimya wakati wananchi wanapoteza maisha.

Masauni amewataka polisi kuwasaka wauwaji wote ambao taarifa zao zimeripotiwa polisi ili sheria ichukue mkondo wake.

Source: ITV habari

A187E419-F70A-4B1A-8657-05FF05837C59.jpeg
 
Wengi sana kina BEN SAANANE,AZORY
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ameunda kamati ili kushauri na kuja na mkakati wa kitaifa wa kukomesha mauaji.

Aidha alisema katika kipindi cha Januari Mosi mwaka jana hadi Januari 31 mwaka huu kulikuwa na matukio 176 na watuhumiwa 150 walikamatwa.

Masauni alitaja sababu kubwa za mauaji hayo kuwa ni kuwania mali, wivu wa mapenzi, visasi, ushirikina, migogoro ya ardhi, ulevi na kuchukua sheria mkononi

Aliwaeleza waandishi wa habari kuwa baada ya kufanya kikao na maofisa wa ngazi za juu ya jeshi hilo, ameamua kuunda kamati ya kuishauri serikali nini kifanyike ili kupata suluhisho la kudumu la mauaji.

Alisema kamati hiyo ambayo itatakiwa kutoa taarifa baada ya siku 21, itashirikisha wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Polisi, Ofisi ya Wakili wa Serikali, Usalama wa Taifa, na Ustawi wa Jamii.

Wawakilishi wengine ni kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU), Taasisi ya Elimu ya Juu, Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Alisema jopo hilo limepewa siku 21 kuja na mkakati wa Kitaifa wa kukomesha mauaji Nchini.

Alisema Serikali hailali usiku na mchana ili kuhakikisha matukio ya mauaji yanakomeshwa.

Alisema katika kikao hicho alipokea taarifa kuanzia Januari Mosi hadi Januari 31, katika maeneo Makuu mawili, Mosi,kuhakikisha matukio yanapotokea hatua za haraka zinachukuliwa ikiwemo watuhumiwa kuchukuliwa hatua za haraka.

Alisema katika kipindi hicho cha Januari Mosi hadi Januari 31 jumla ya matukio ya mauaji 176 yalitokea na mikoa vinara ni Kagera, Dodoma, Tabora, Mara, Kigoma na Songwe.

Pia aliwataka wananchi kujitokeza kutoa taarifa kwa kamati.

“Kuna Mzee mmoja analalamika sana kule Mtwara baada ya mtoto wake kuuawa, Serikali kukaa kimya jambo hilo litafanyiwa kazi.,” alisema.

Alisema wote wenye malalamiko kwenye matukio yaliyotokea waende kwenye vituo vya Polisi milango iko wazo

Chanzo: HabariLeo
 
Anayefahamu namna na kupata nafasi ya kuwa kwenye hizi tume/kamati anielekeze tafadhali, naona kuna kulaji unapita mbele yangu nikiwa naona kabisa!
 
Waanze na ya Mtwara, Haya ya mapenzi ya watu wayaache, tuanze na matatizo ya jeshi Lao!

Dogo Ana 25 years, Ka hastle kapiga pesa take ndefu, mnampora, then mnamuua!

Hivi hii dame yake Jaman Kwa jeshi la police Ni changamoto kubwa, na Haki isipofanyika hii ni lana Sana!

Ni kwamba watu hawasomi vizuri vitabu vyako vya dini, hili halikibaliki, Kamati ya nini sasa? Italeta nini kipya?
 
Kamati kamati hizi hazijawahi kuja na mwarobain zaidi ya kuwa chanzo cha ulaji na ufujaji wa fedha za walipa kodi
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ameunda kamati ili kushauri na kuja na mkakati wa kitaifa wa kukomesha mauaji.

Aidha alisema katika kipindi cha Januari Mosi mwaka jana hadi Januari 31 mwaka huu kulikuwa na matukio 176 na watuhumiwa 150 walikamatwa.

Masauni alitaja sababu kubwa za mauaji hayo kuwa ni kuwania mali, wivu wa mapenzi, visasi, ushirikina, migogoro ya ardhi, ulevi na kuchukua sheria mkononi

Aliwaeleza waandishi wa habari kuwa baada ya kufanya kikao na maofisa wa ngazi za juu ya jeshi hilo, ameamua kuunda kamati ya kuishauri serikali nini kifanyike ili kupata suluhisho la kudumu la mauaji.

Alisema kamati hiyo ambayo itatakiwa kutoa taarifa baada ya siku 21, itashirikisha wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Polisi, Ofisi ya Wakili wa Serikali, Usalama wa Taifa, na Ustawi wa Jamii.

Wawakilishi wengine ni kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU), Taasisi ya Elimu ya Juu, Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Alisema jopo hilo limepewa siku 21 kuja na mkakati wa Kitaifa wa kukomesha mauaji Nchini.

Alisema Serikali hailali usiku na mchana ili kuhakikisha matukio ya mauaji yanakomeshwa.

Alisema katika kikao hicho alipokea taarifa kuanzia Januari Mosi hadi Januari 31, katika maeneo Makuu mawili, Mosi,kuhakikisha matukio yanapotokea hatua za haraka zinachukuliwa ikiwemo watuhumiwa kuchukuliwa hatua za haraka.

Alisema katika kipindi hicho cha Januari Mosi hadi Januari 31 jumla ya matukio ya mauaji 176 yalitokea na mikoa vinara ni Kagera, Dodoma, Tabora, Mara, Kigoma na Songwe.

Pia aliwataka wananchi kujitokeza kutoa taarifa kwa kamati.

“Kuna Mzee mmoja analalamika sana kule Mtwara baada ya mtoto wake kuuawa, Serikali kukaa kimya jambo hilo litafanyiwa kazi.,” alisema.

Alisema wote wenye malalamiko kwenye matukio yaliyotokea waende kwenye vituo vya Polisi milango iko wazo

HabariLeo
Waende vituo vya polisi milango iko wa" hapo ndio tunaposhindwa kupata suluhu ya changamoto kwakua polisi ni walalamikiwa wakubwa kwenye hizi kadhia
 
Back
Top Bottom