JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Changamoto kubwa ya umeme Nchini imetajwa kuwa ni kutofanyika kwa uwekezaji wa kuboresha miundombinu inayoendana na mahitaji kwa miaka mingi, ndio maana gridi ya umeme imekuwa ikizidiwa uwezo wa kufanya kazi.
Waziri wa Nishati, January Makamba akiwa Mkoani Tabora wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu, leo Mei 19, 2022 amesema: “Miundombinu ni kama waya zenye urefu na unene sahihi, transfoma, vituo vya kupokea na kupoozea umeme.
“Kukosekana kwa uwekezaji matokeo yake mfumo wa gridi yetu umeelemewa kutokana na kuongezeka mahitaji na uchakavu, lakini kwa sasa Rais Samia ametoa Tsh. bilioni 500 ambazo zitatumika kuimarisha gridi ya taifa.”