Waziri Makamba ameanza rasmi project alizotumwa TANESCO

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,550
11,879
Shirika la TANESCO limeingia mkataba wa kusimika mfumo wa kisasa wa ufanisi,wenye thamani ya dola milioni 30 za marekani na kampuni ya Mahendra kutoka India.

My take:
Hao wataalamu walipopewa nafasi ya kuongea wanasema ni pamoja na utawala pamoja na kumonitor mfumo mzima wa Tanesco kutokea satellite.

Yalee ya Net group solutions waliowahi kutupiga miaka ile ya JK.

Sasa tumeelewa maana ya kumtoa Kalemani.

Chanzo: ITV news jioni ya 09/11/2021.
 
Kwa kweli nimeshangaa sana, Tanesco wana Ingia mkataba wa Bilioni 69.3 bila kuelezea huo ufanisi utapimwa vipi na kwa mambo gani, yaani ni ujanja ujanja tu.

Tena wameona waseme kwa dola ili watu wasione kama ni nyingi, dola milioni 30 mkataba wa kuongeza ufanisi kwenye mfumo bila kueleza huo mfumo uko wapi na unatakiwa uende wapi? Hapa kuna harufu ya kupigwa
 
Kwa kweli nimeshangaa sana, Tanesco wana Ingia mkataba wa Bilioni 69.3 bila kuelezea huo ufanisi utapimwa vipi na kwa mambo gani, yaani ni ujanja ujanja tu. Tena wameona waseme kwa dola ili watu wasione kama ni nyingi, dola milioni 30 mkataba wa kuongeza ufanisi kwenye mfumo bila kueleza huo mfumo uko wapi na unatakiwa uende wapi? Hapa kuna harufu ya kupigwa
Tunarudi kule kwa DOWANS bila aibu!
 
Kumbe Tanzania haina wasomi kwenye fani ya management mpaka kuwaagiza toka nje tena kwa gharama ya $30 milion, hawa watu hawana credibility kuongoza hizi wizara, vetting ni kujuana tu.

Naona hii ndio kazi ya kwanza Makamba aliyoshauriana na ile bodi yake mpya aliyowaweka wale watu wake, tutapigwa sana, bado mrejesho wa kule Dubai alikotoka juzi.

Hizo pesa badala zikatumike kurekebisha miundombinu ya umeme upatikane wa kutosha ili tuachane na hii biashara ya kukatika hovyo, wao wanaenda kuweka satelite ili ku-monitor jinsi unavyokatika mara kwa mara.
 
Umendika kwa hisia zisizo na uhakika. Subiri ujiridhishe kabla ya kuweka mawazo yako hadharani.
Nimekuwa nafuatilia shirika hili kwa muda sasa.
Tangu makamba alipoingia cha kwanza kufanya ilikuwa kuipangua safu ya Tanesco iliyokuwepo tena yenye wataalamu wabobezi, akaweka wajumbe wasio wazoefu tena wengine kutoka Tigo.

Priority za Tanesco sio utawala kutoka nje, bali source zaidi za umeme sababu mahitaji yanazidi kuongezeka kutokana na idadi ya watumiaji kuongezeka. Ndio maana tunajenga bwawa la Nyerere.

Tungemuona mzalendo pale ambapo angeliwezesha shirika kupeleka umeme kwenye migodi mikubwa nchini ambako wangepata mapato mara dufu.

Mfano kwa mgodi wa Geita ambapo umeme upo mjini lakini umeshindwa kuunganishwa na mgodi uliopo kilomita 4 toka mjini.kwa hapo tu shirika linapoteza zaidi ya bilioni kadhaa kila mwezi.

Sijakurupuka.
 
Kumbe Tanzania haina wasomi kwenye fani ya management mpaka kuwaagiza toka nje tena kwa gharama ya $30 milion.

Naona hii ndio kazi ya kwanza Makamba aliyoshauriana na ile bodi yake mpya aliyowaweka wale watu wake, tutapigwa sana, bado mrejesho wa kule Dubai alikotoka juzi.
Ukitangaza nafasi ya kazi moja Tanesco, kesho watakuja zaidi 1000 kuleta application.
 
Back
Top Bottom