Waziri Maghembe: "TANESCO, ukiritimba too much"

Waziri Maghembe: "TANESCO, ukiritimba too much"

wale dada poa bado wapo wegi kakora ? ile bus bar bado ipo ?ile recodi mliovunja ya kunywa pombe zote kwenye bar zote mpaka mji ukawa haunahata kiroba kimoja mshairudia tena
 
Wadau maeneo ya kitunda toka asubuhi wamekata umeme,umekuja kurudi saa moja usiku,sasa wamekata,wanarudisha kisha wanakata sasa mara ishirini nzima,na leo ndio nimepata machungu ya bei ya luku,kudadek bad service

Yaani hawafai kabisa umeme kukatika muda wowote, Ukitaka kuongezea units mitambo yote hadi head office out of service the whole day, ukipiga simu kuulizia hawapokei simu haswa Tegeta branch kwa kweli majanga makubwa haya jamani kama vile tanesco yote ifutwe tuanze upya Khaa!!!!
 
Tanesco imeisha pimwa na wataalam na Dawa inajulikana ila serikali inakuwa na kigugumizi kuitumia sijui kwa nini
 
Hawa tanesco mimi sina hamu nao kabisa sisi wakazi wa majohe ni mwaka karibia wa tatu huu umeme ni mdogo wakazi ni wengi transfoma iliyokuwepo ni ndogo haiwezi ku supply umeme kwenye nyumba zote yaan tv haziwaki mafriji hayafanyi kazi vitu vinaungua ukienda wanakuambia swala lenu lipo ofisini yaan ni kero kwakweli....
 
Nimetoka kwenye ofisi zao hapa mbezi kutaka kubadilishiwa tarrif yaani customer care yao mbovu,anachokueleza engineer tofauti na customer relation officer kila mtu ana majibu yake. naboreka sana shirika kubwa kama hili linaongozwa na maamuzi ya mtu binafsi na sio kanuni na taratibu.
 
wadau maeneo ya kitunda toka asubuhi wamekata umeme,umekuja kurudi saa moja usiku,sasa wamekata,wanarudisha kisha wanakata sasa mara ishirini nzima,na leo ndio nimepata machungu ya bei ya luku,kudadek bad service

we ndio umejua leo??mabibo makuburi ulikatika saa nne asubuhi km leo ukaja kurudi siku ya pili saa 0018 baada ya wanafunzi wa udsm (mabibo hostel)kugoma, ulidumu kwa dk 5 then ukakatika tena mpaka 0038 then ukarudi.! Tulikaa jumla ya masaa 38 bila umeme. Hakujawai kutolewa taarifa yoyote kama ilikuwa ni itirafu au la.
 
Habari wanaJF!


Kuna kero tumekuwa nayo toka mwezi wa 10/2013 hasa wakazi wa Tungi na Tubuyu hapa Morogoro mjini ya kutokuunganishiwa umeme ilihali tulishalipishwa Sh. 320,000/- ikiwa ni gharama ya kuunganishiwa umeme tangu wakati huo. Cha ajabu mpaka sasa tunaambiwa Hakuna nyaya lakini tayari kuna wenzetu umeme ushaunganishwa sasa hao sijui wametoa wapi hizo nyaya?


Nimeona hili suala nililete kwenye JF ili kujadili je hii Hali ni kwetu tu au hata maeneo mengine matatizo ni haya? Sijui ni kwa nini wanapandisha gharama ya umeme wakati hatuoni huduma nzuri au uboreshaji wa huduma zaidi ya kuongezeka kwa rushwa?


Karibu kwa mchango.......
 
Hata hivyo hii ni changamoto kubwa ya uendeshaji wa miradi ya maji vijijini, kwani ukiangalia mamlaka kubwa tu zinashindwa kulipia gharama za umeme ili wapate maji, sasa kwa mwananchi wa kawaida wa kijijini hata umeme ukifika. gharama za kila mwezi za umeme zitamshinda tu, ukizingatia na umeme ulivyopanda ni balaa. Watanzania/wataalam bado mna kazi ya kutafuta njia mbadala ya kutoa huduma ya maji uko vijijini ya gharama nafuu

Labda ungeuliza vipi na Wizara yake iliyopo hapa mjini inadaiwa na Tanesco?
 
Shirika la tanesco hivi karibuni limeongeza bei kwa unit hivyo kuongeza gharama za maisha.mojawapo ya sababu zinazotolewa juu ya kuomgeza bei ni kuboresha huduma na kufanya mapinduzi kulifanya shirika linalotengeneza faida. Cha kushangaza hawa wanaoelekea kuwa wafanya biashara watakaotengeza faida hawana habar ya namna gani unaweza kuwafanya wateja wakaridhika na huduma au kuhakikisha huduma inapatikan muda wote maana matumizi ya mteja ndo faida yenyew. Kinachonifanya niseme hivyo niko ifakara na kumekuwa na kawaida umeme kukatika kila jnne na alhamis siku nzima na siku za kawaida muda wowote tanesco wakijiskia. Najiuliza huku si kupoteza mapato?.kuns transforms imeungua wiki ya tatu haijapatikana mbadala na watu wanakosa huduma hii si kwa kupenda ila kea kulazimishwa. Tanesco yenyew imeshindwa kutatua Hilo tatizo kwa muda wote huu na hivyo kupelekea mpka halmashaur yenyew kukosa umeme nakuwek ugumu wa kufanya kazi na wadau Hasa huduma ya umeme inapohitajika. Najiuliza hawa tanesco watarejesha huduma sawa na makato wanayotukata ? Hivi kweli wanajua wanatakiwa kujiendesha kibiashara na kujali kutoa huduma bora kwa mteja. Hebu tusaidiane kwenye hili.
 
hongera kwa mada murua. Tanesco ni tatizo, kwao faida wataisikia tu. Mm nipo songea, nyumba ninayoishi ina tatizo la umeme kwenye nguzo, tangu j2 nipo gizani, nimeripoti kwao j5 kitengo cha dharura, nimesubiri nyumban hadi leo ijumaa hawajafika, leo nimeenda tena, jibu tutakuja, kimya, sijui duniani kuna nn. Pili, Nimelipia kuingiza umeme kwa wazazi wangu sept mwaka jana, hadi sasa ni stori tu, mara vifaa hakuna, tunaingiza kwa kufuata aliyewahi kulipia nk, yaani hata wazazi wangu wananiona mm msanii, sasa najikuta kuwachukia hata watumishi wake, naona wote si waungwana. Hawajui kama cc tunachangia kwenye mishahara yao. Kweli unyonge ni kitu kibaya sana, has hapa tz kwani utaishi kwa kusononeka na kumkosea hata mungu na kusababisha hata maisha ya ahera kuyakosa.
 
Kama watu tunavyofahamu kwa hivi sasa, kila kona ya nchi hii, wananchi wanalalamikia makali ya maisha wanayokabiliana nayo kutokana na kupanda kwa bei ya umeme kwa asilimia 40, tokea Januari mosi mwaka huu.

Uniti moja ya umeme hivi sasa inauzwa kwa zaidi ya shilingi 300 toka bei yake ya awali ya shilingi 221, wale wanunuzi wa Luku, ambapo hapo kabla walipokuwa wanakwenda na shilingi elfu 10, walikuwa wakipata uniti 37 kama weshakatwa service charge, hivi sasa ukienda na elfu 10 hiyo hiyo mwanzo wa mwezi, unaambulia uniti 8 peke yake!!

Hata hivyo TANESCO wametoa taarifa ambayo imenukuliwa na vyombo vya habari ya kuwa wanazidai Taasisi mbalimbali za serkali yetu, kiasi kisichopungua shilingi bilioni 174!!

Sasa swali la kuwauliza TANESCO, kumbe operesheni zao zote za kata umeme huwa wanawalenga wananchi wanyonge wa majumbani wenye vibili vidogo vidogo vya shilingi elfu 10 au 20, wakati wale wadeni sugu, hususani Idara mbalimbali za serikali, kama vile majeshi ya ulinzi, Polisi, Vyuo mbalimbali vya Umma na wizara za serikali, wakizigwaya, ambapo kumbe huwa hawathubutu kuzigusa, wakati wanajua wanawadai mabilioni ya shilingi!!

Hili la TANESCO "kuwang'ang'ania" wateja wadogo wanaodaiwa "vijisenti" na kuwaacha wateja wakubwa wanaodaiwa mabilioni wakiendelea kupeta wakitumia umeme "bure" sasa hawawezi tena kulikanusha, kwa kuwa ni tamko lililotolewa na wenyewe TANESCO, na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari.

Swali lingine ambalo tungependa kuwauliza TANESCO, ni kwa nini wanapata "kigugumizi" kuyakatia umeme hayo mashirika na Taasisi mbalimbali za serikali, wakati kila bajeti ya kila mwaka, Idara hizo za serikali na Taasisi zake hutengewa bajeti maalum za kulipa bili hizo za umeme, ambapo pesa hizo ni kodi zetu sisi wananchi?!

Swali lingine ambalo tungependa kuwauliza EWURA ni kwa vipi wanabariki upandishaji mkubwa wa umeme, wakati wakijua fika kuwa, chanzo cha uzorotaji wa utendaji wa TANESCO ni uzembe wao wa kutokusanya madeni yao toka serikalini?!

Lipo swala lingine ambalo tungependa kuwauliza EWURA, ni kwa vipi wamekubali ongezeko hilo la umeme, wakati wanawaidhinishia watumishi wa TANESCO watumie umeme wa "dezo" wa uniti 750 kwa kila mwezi, kwa kila mfanyakazi wa TANESCO?!

Mimi nadhani watanzania tumeonewa kiasi cha kutosha, tumegandamizwa kiasi cha kutosha, na unyonge wetu ndiyo uliotufanya tuonewe hivyo na kugandamizwa, na sasa tunapaswa kutamka sasa BASI, hatutakuwa tayari kuonewa tena na kugandamizwa tena, na tunapaswa kuzikomesha kwa vitendo kauli za kifedhuli zinazotolewa na viongozi wetu tuliowakabidhi dhamana za kutuongoza, kama ile kauli iliyotolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, ambaye alidiriki kuwakebehi watanzania, kwa kiwango cha kutisha, pale alipotamka kuwa, wale wote ambao watashindwa kumudu bei mpya za umeme, ni bora wakawasha vibatari au wakalala giza majumbani mwao!!!
 
Huku kwetu toka jana umeme unakatika katika mara kwa mara almost kila baada ya dakika tano na kurudi. hakika huu sio mgawo maana ni kama mtu anawasha na kuzima, mpaka nahisi kama kuna watoto wanachezea yaani wanawasha na kuzima. Migawo yote ya umeme haijawahi kutokea wa namna hii. tanesco vipi?
 
Hii ndio tanesco,ni full majanga..gharama imeongezeka na umeme wanatukatia.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mambo yote shaghala bhaghala ndani ya Utawala Wa CCM. Vumilia tu Mkuu mpaka siku watanzania watafanya maamuzi sahihi
 
Mambo yote shaghala bhaghala ndani ya Utawala Wa CCM. Vumilia tu Mkuu mpaka siku watanzania watafanya maamuzi sahihi

Moja ya sababu za kupandisha gharama huwa ni kuboresha huduma lkn tanesco pamoja na kupandisha gharama huduma bado iko hoi sana, kweli hili ni janga
 
Hapa ndio ninapozidi kuipenda CCM,gharama za umeme juu,maji juu na vyote havipatikani kwa uhakika,maisha magumu lkn Serikali ni kama haioni au inafurahia hii hali.........tumeanza kupiga kelele pengine ni ishara ya kuchoka na tutafanya maamuzi magum 2015.......CCM endeleeni hivi hivi mpk tukolee rangi vizuri.
 
kama huduma haiboreshwi sasa hizi gharama zinapanda kwa sababu ya nini? inamaana pesa zinaenda kwingine sio kuboresha huduma ya umeme.
 
Back
Top Bottom