EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,347
Waziri wa maji, Prof Jumanne Maghembe ameelezea kukerwa kwake na shirika la umeme nchini (TANESCO) kwa madai limeshindwa kufikisha umeme vijijini na hivyo miradi ya maji kusuasua.
Kadhalika waziri huyo ametamani kuwapo kwa shirika mbadala ambalo litatoa ushindani kwa TANESCO ili iweze kutekeleza shughuli zake na hivyo miradi ya maji kukamilika kwa watati.
"Tungekuwa na mashirika mengine ya umeme tungeweza kufungiwa umeme haraka, lakini kwa vile ni TANESCO peke yake, sasa wananchi hawana maji…. TANESCO, ukiritimba too much," alisema.
Profesa Maghembe alisema hayo wakati anazindua mradi wa usambazaji majisafi katika kata ya Kiboroloni na viunga vyake. Aidha waziri huyo alisema kati ya vijiji hivyo 74, ni vijiji 28 ambavyo miradi yake imekamilika na wananchi wanapata huduma hiyo huku Vijiji 17 miradi yake ipo katika hatua za mwisho lakini tatizo lililopo ni kukosekana kwa umeme.
"Lakini kwa kweli tatizo tulilonalo sasa ni Tanesco…. Kwa muundo walionao ni lazima TANESCO wapandishe soksi zao juu," alisema.
Source: Waziri Maghembe azindua mradi wa maji Kiboriloni, asema "TANESCO ukiritimba too much"inakwamisha mipango; Atamani ipate mshindani - wavuti.com