Waziri Maghembe atoa fursa za mafunzo ya ufugaji nyuki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,429
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amewataka wananchi wa Tabora kutumia fursa ya uwepo wa Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki(BTI) kupata mafunzo ya ufugaji nyuki.

Alisema ni vyema mkuu wa mkoa huo, Aggrey Mwanri kutengeneza mpango wa wananchi kimakundi na hata kvijiji kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi ya ufugaji nyuki chuoni hapo kuboresha uzalishaji wa asali na nta.

Waziri Maghembe ametoa kauli hiyo juzi alipotembelea chuo hicho wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Tabora. Ziara hiyo ni ahadi aliyoitoa bungeni wakati akihitimisha mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018.

“Mkuu wa Mkoa, tafadhali andaa utaratibu maalumu kwa wananchi wako, wale wafugaji wa nyuki wanaweza kwenda kwenye chuo chetu hapa (Tabora) hata kwa siku tatu ili wafundishwe namna bora ya kufuga nyuki, yaani watoke kabisa huko Sikonge, waletwe hapa, walale hapa siku moja au mbili wafundishwe baadae warudi makwao wajue namna bora ya kufuga na kuvuna asali,” alisema Maghembe.

Kwa upande wake mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alisema maelekezo hayo kwao ni faraja na kwamba watahakikisha wanatumia fedha zilizopo kuwapa taaluma. Mkuu wa chuo hicho Semu Daudi alisema kwa sasa wana wanafunzi 155 wanaosoma Cheti na Diploma ya Ufugaji wa Nyuki.

Aidha alisema kuwa chuo hicho kina changamoto kadhaa lakini kitakuwa na uwezo wa kutoa elimu ya darasani kwa wakulima wa mkoa huo.


Chanzo: HabariLeo
 
Inatakiwa iwe ni vision ya nchi nzima sio huko sikonge tu. Chuo kiwe na maono mapana
maana pote pana maeneo yanayokubali ufugaji.
na Tanzania ni ya pili afrika kwa Kuzalisha asali, Kama ikichukuliwa kama kitu makini kinaweza kuongeza pato kubwa tu kwa wengi wanaoishi chini ya dola moja na taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom