Waziri Lukuvi piga jicho Kitengo cha Leseni ya makazi Manispaa ya Kinondoni

Tanaluza

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
212
121
Mhe Lukuvi heshima kwako baba

Mimi na wananchi wengine wa Manispaa ya Kinondoni tumekuwa tukipata tabu katika kupata Leseni zetu za makazi.
1. Tunalipia Leseni zetu za makazi bila ya kupewa risiti halali zaidi tunapewa kikaratasi kilichosainiwa na Mhasibu bila muhuri wowote.

2. Ukiapply kwa ajili ya kurenew leseni iliyopotea utalipia miaka yote ya nyuma tangu tarehe ya kwanza ilipotolewa leseni.

3. Hata ukilipa malipo yote ya no.2 watakupa ahadi ya muda wa kusubiri wa mwezi 1 ndo leseni yako itakuwa tayari. Baada ya mwezi 1 ukiwa na matumaini ya kwenda kuchukua leseni yako utakutana na barua ya kumtaka mtendaji wa mtaa wako athibitishe kwamba eneo lako halipo mabondeni.

4. Baada ya kuipeleka barua ya uthibitisho kutoka kwa mtendaji wa mtaa watakujibu leseni yako bado haijafanyiwa kazi sasa urudi baada ya mwezi 1 itakuwa tayari.

Mhe Lukuvi haya yote ni masaibu yanayotupata tukifuatilia leseni za makazi yetu ndani ya manispaa ya kinondoni. Tunaomba usaidizi wako kutatua kadhia hii.
 
Kiukweli lukuvi anapiga kazi
Nsmpongeza sana
Kwamwendo huu migogoro mingi ya Ardhi itapungua
 
Kiukweli lukuvi anapiga kazi
Nsmpongeza sana
Kwamwendo huu migogoro mingi ya Ardhi itapungua
Achungulie na huku kitengo cha leseni ya makazi wamekuwa wakitupa tabu sana mpaka watu wanakata tamaa kutafuta leseni
 
Back
Top Bottom