Muheshimiwa William Lukuvi kwanza nikupongeze kwa jitihada zako katika wizara ya Ardhi, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni umejitahidi kwa kadiri unavyoweza na angalau sasa kuna afadhali upande huu wa ardhi maana ilikuwa majanga, nina malalamiko yangu najua huku hata kama si wewe binafsi unapita basi vijana wako watapita na kukupatia ujumbe.
Nimehangaika kupima viwanja vyangu kwa miaka miwili na nusu sasa nilianza kabla ya huu utaratibu wa kutumia kampuni binafsi haujashika kasi, kwa miaka miwili nimekuwa mtu wa kuzunguka kuanzia ofisi za manispaa ya kinondoni mpaka finally mwezi January hati zikawa tayari zimeandaliwa imebaki kusainiwa tu,
Tatizo limekuja hapo kwenye kusainiwa ni mwezi wa pili sasa nasubiri saini ya kamishna wa ardhi ili niweze kupata hati zangu maana ni zaidi ya moja,kiukweli naona hili zoezi lina kila dalili ya kuchukua si chini ya miezi sita kitu ambacho ni ajabu sana maana najiuliza hivi kweli hata kama kamishna yuko busy vipi kusaini na ana kazi nyingi kiasi gani hivi kweli inaweza chukua zaidi ya miezi miwili kusaini hati?
Wewe mwenyewe waziri umekuwa ukionekana kwenye vyombo mbalimbali vya habari ukieleza kwamba utaratibu wa sasa hati ikishakuwa tayari haichukui zaidi ya mwezi kuipata napenda kukuambia hili jambo si kweli na kama ndio dhamira yako basi wasaidizi wako wanakuangusha hati zangu ni za manispaa ya Kinondoni.
Mara ya mwisho nimekwenda pale nimepangiwa kwenda baada ya wiki mbili yaani mwisho wa mwezi huu wa tatu ambapo nitakuwa na miezi miwili na nusu nasubiri hati isainiwe,hii inakatisha tamaa sana muheshimiwa kama nimehangaika miaka miwili na nusu nashuhulikia hati,hati imekamilika nayo ichukue miezi sita kusainiwa kweli mnapaswa kujipanga kwa upya si kwa utaratibu huu,na mimi nakushauri ili kupima utendaji kazi wa mtu kila mtu apimwe kwa utoaji mafaili mezani kwake akiwa chini ya kiwango basi nafasi hiyo apewe mtu mwingine.
Ni hayo tu muheshimiwa waziri ila naomba kitengo hiki cha hati kiangaliwe kwa jicho la tofauti watu wanajenga mazingira ya rushwa kwa makusudi japo hawasemi lakini mtu anakuambia njoo uangalie baada ya wiki mbili ukija hakupi sababu wala taarifa faili limefikia wapi anakuambi njoo baada ya wiki mbili tena namna hii ukiwa mwepesi au hutaki usumbufu huu ni rahisi sana kushawishika kutoa rushwa ili mambo yako yashuhulikiwe haraka. Natumaini hili litashuhulikiwa kwa namna ifaayo.
Sina mawasiliano ya senior personel yoyote pale wizarani ambaye ningeweza kufikisha ujumbe huu ndo maana nimeandika huku kwa wenye mawasiliano yako watakufikishia ujumbe, pale wizarani napendekeza badala ya maboksi ya maoni wekeni namba ya mtu anayeweza kupokea malalamiko ya wananchi tena iwe waziwazi kila mtu aione ili tuwe tunatoa mrejesho wa huduma inayotolewa pale kama ni mbaya au nzuri.