Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
- Thread starter
-
- #21
Mkuu wanasema hawana uwezo wa kujua nani ana uwezo nani hana, kwa hiyo inabidi wanyang'anywe wote tu.Nafunga mkono hoja. Sio wote waliopata viwanja Wana Hali nzuri ya kujenga kwa haraka.
Kuna watu Wana maviwanja mengi na hawaendelezi hao ndio wanaweza kutaifishwa. Mfanyakazi wa serikali au sekta binafsi kabahatika kupata kiwanja kilichopimwa halafu umnyanganye.
Mfano Kibada, mbweni na meneo mengine wapi watu wa kipato Cha chini.
Waziri asidhani Kama Ana uwezo wa kununua nyumba Mbezibeach labda mil 500 ni watu wachache wenye baraka za Aina hiyo.
Sijawahi tembea Dar hii bila kukuta eneo la Patel & Co. Hao ndio wasipoendeleza wanyanganywe
Kwani lazime tujue ujinga wako? Ungekaa kimya tusingejua u mjinga kiasi gani. Anyhow the choice is yours.
Mkuu jielekeze katika mantiki za mtoa hoja. Ameelezea kwa kina na uhalisia kuhusu umiliki wa viwanja na uwezo wa mtu binafsi kuviendeleza ktk mazingira ya sasa ya kiuchumi. Epuka "perception errors". Siyo ukweli ya kwamba yeyote aliyepewa kiwanja, labda cha "low density" na kushindwa kukiendeleza ana historia ya kuwa fisadi. Hizi roho za kimaskini na kifukara za kutaka mwingine anyang'anywe upewe wewe sijui zinatokea wapi nyakati hizi!
Sasa wajitokeze waeleze wana malengo gani na hivyo viwanja,
Tatizo mkuu kuna sehemu ni mapori na kama umejenga basi utakuwa na wakati mgumu wa kufukuzana na wadudu wabaya na wezi, wanatupa shidaaa
Kuna miradi ya NHC inafanya hivyo!Historia ya Mh. Lukuvi inaonyesha kuwa alitokea unyongeni sana, na wapo waliomsaidia kufika hapo alipofika. Cha ajabu sasa badala ya kutumia uzoefu na uwezo alioupata kuwasaidia wanyonge kuinuka, yeye amebaki kuwatisha kama walivyofanya wakoloni. Nchi za wenzetu real estate ndio huwa wanajenga nyumba, wafanyakazi wanachukua morgage wanakwenda kuishi kwenye hizo nyumba huku wakikatwa kidogo kidogo kutoka kwenye mishahara yao.
Lakini suala jingine la msingi ni kwamba, wakati Lukuvi anapiga kelele kuwa watu wanyang'anywe viwanja, je serikali imefanya nini kupeleka huduma za msingi kama maji na umeme huko? Leo hii nikijenga nyumba huko, nitapata maji ya bomba? Je nitavuta umeme kirahisi? Barabara zimechongwa?Kuendeleza maana yake si ujenge nyumba iishe, hata ukiweka msingi umeendeleza.Mimi mtazamo wangu ni speculator tu ndiye ananunua viwanja haombi hata kibali cha ujenzi fikra yake bei ipande apate faida.
Hili nalo neno, siyo kulazimisha watu wajenge wakati hakuna miundombinu wezeshiLakini suala jingine la msingi ni kwamba, wakati Lukuvi anapiga kelele kuwa watu wanyang'anywe viwanja, je serikali imefanya nini kupeleka huduma za msingi kama maji na umeme huko? Leo hii nikijenga nyumba huko, nitapata maji ya bomba? Je nitavuta umeme kirahisi? Barabara zimechongwa?
Kweli Mkuu. Nimesema hakuna mtu mwenye kiwanja, ana shida ya nyumba, ana uwezo wa kujenga lakini hataki kujenga. Kama wapo ni wachace ambao wanavizia kuviuza kwa bei za juu. Na hao ni wale ambao Wizara ya ardhi yenyewe iliwapa viwanja kwa mlango wa nyuma, au wafanyakazi wa wizara yenyewe!Mara nyingi hali ngumu ya kipato ndo inawabana watu wasiweze kuendeleza maeneo yao, mishahara haiongezeki, biashara hazi perform, uwekezaji kwenye sekta binafsi unachechemea, kilimo hakieleweki, vijana wengi wanalandalanda tu bila kuwa na kazi za kufanya lakini kutwa kujisifia tumenunua ndege na bado tunaongeza zingine, ni shida aisee..
kwa hiyo bora tunyan'ganywe halafu wewe ndo utafaidika na nini?Ishu ni kuhodhi viwanja bila kuendeleza wakati wanyonge hawana pa kuishi.
Lukuvi baba shika hivyo hivyo hadi wa PUU
cha kwangu barabara hazipitiki halafu mtu aliyejilimbikizia ardhi kila kona ya nchi hii anaamua kuninyanganya yeye aliyebadili open space kuwa viwanja na akiwa mwenyekiti wa bodi ya CDA wakati ule alishindwa kutengeneza mazingira rafiki watu wamiliki viwanja lakini yeye kila siku kujilimbikizia maeneo.Hili nalo neno, siyo kulazimisha watu wajenge wakati hakuna miundombinu wezeshi
Kuendeleza maana yake si ujenge nyumba iishe, hata ukiweka msingi umeendeleza.Mimi mtazamo wangu ni speculator tu ndiye ananunua viwanja haombi hata kibali cha ujenzi fikra yake bei ipande apate faida.
Shirika la nyumba tatizo ni kama benki, wanatoza hela nyingi sana. Yaani gharama ya kufikisha msingi tu wewe binafsi unaweza kuwa umemaliza nyumba!Walipashwa kuweka utaratibu wa shirika la nyumba linajenga kwenye viwanja vya watu hao walipewa wanakopeshwa ili visikae wazi wakati watu wengine wanataka, na Lukuvi shirika la nyumba liko chini yake utaratibu ungewekwa wangejenga wanakopeshwa thamani ya nyumba, kiwanja kinabaki kama dhamana
Du umeongea kwa uchungu sana Mkuu!kwa hiyo bora tunyan'ganywe halafu wewe ndo utafaidika na nini?
binafsi akiamua kuchukua mwache achukue najua thamani niliyonunulia hicho kiwanja wakati huo nikifanya kazi kwa mtu nikilipwa shilingi 120,000/- kama mshahara. nikakopa kwa watu nikaweza kununua kiwanja cha 690,000 wakati huo lakini nilifanikiwa kwa kutoa awamu mbili kwa kuandika barua kwa meneja wa mradi.
kwa muda mrefu kweli sijakiendeleza na sio sitaki ila kwa changamoto zinazonikabiri kwa zaidi ya miaka saba sasa na nimeshindwa kuendeleza ujenzi.
sasa kama kaamua kukichukua mwache achukue tu ili ninyi ambao hamkupata wakati ule mfurahi japo ikumbukwe ilikuwa ni kwenda tu kujaza form na kisha unagawiwa kiwanja.
roho zetu zitauma kwa kuwa tutakuwa tumepoteza kitu cha thamni lakini ikumbukwe pia tutakuwa tumethurumiwa kwa kuwa sisi ni wapangaji kwa miaka zaidi ya 60 kwa kadri ya hati ya mkataba wa kiwanja.
Kwanza hujamuelewa lukuviKila wakati Lukuvi anapenda kutoa tishio kwa Watanzania waliopewa viwanja na serikali kuwa watanyang'anywa kwa kuwa hawana uwezo wa kujenga. Yaani Lukuvi anachosema ni kwamba, hawakustahili kupewa hivyo viwanja kwa kuwa wao hali yao ya kuichumi iko chini na hawana uwezo wa kujenga hara
Mwambie Lukuvi kwamba nataka kujenga, lakini kiwanja changu kilipo hakuna barabara wala maji. Na umeme uko mbali sana. Aweke basi angalau hiyo miundo mbinu mie nitajenga angalau chumba kimoja.Kwanza hujamuelewa lukuvi
Pili sheria inataka hivyo
Anachokataa lukuvi usiache pori,jengawalau chumba kimoja weka mtu awe anasafisha
Sio vitisho utanyang'anywa kweli nenda ukurasa wa pili wa hati yako kasome kuna masharti ya kuazimwa hiyo ardhi na ukaweka saini yako,anachofanya lukuvi ni kufuata sheria tu
Basi kachukue viwanja huko mkuranga dar hapakufaiMie hapa. Lengo langu ni kujenga nikilipwa mafao yangu ya kustaafu kwa kuwa kwa sasa sina uwezo wa kujenga