Waziri kivuli CHADEMA aachia ngazi

Dr wa ukweli

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
900
264
WAZIRI Kivuli wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), na Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Leticia Nyerere amejiuzulu wadhifa huo.Hatua ya kujiuzulu kwa mbunge huyo imekuja kipindi kisichozidi miezi minne tangu kuundwa kwa baraza hilo katika Mkutano wa Bunge la Februari.

Taarifa za kujiuzulu kwa Nyerere zilivuma kuanzia jana mchana huku Spika wa Bunge Anne Makinda, akisema anasubiri taarifa za uteuzi kutoka kwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.

Akizungumza kwa simu jana jioni, Nyerere alithibitisha kujiuzulu akisema hatua yake ni uamuzi aliouita wa kidemokrasi kwani unalenga kutoa fursa kwa wengine kuongoza. Hata hivyo, hakutoa sababu za kuchukua hatua hiyo. Alisema Chadema kina wabunge 48 wakati nafasi za mawaziri ni 18 ukiacha manaibu, hivyo ameamua kuwapa nafasi wengine wapate uzoefu.

Mbunge huyo aliyeingia bungeni kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa Oktoba, mwaka jana alisema tayari amesambaza nakala ya barua hiyo hadi Ofisi ya Spika wa Bunge."Nimeamua kuachia ngazi ili kupisha wengine wapate uzoefu. Ni uamuzi wa kidemokrasi na hii ndiyo demokrasi. Demokrasi ni kuruhusu wengine waweze kuonyesha uwezo wa kuongoza," alisisitiza na kuongeza:,

"Kwa hiyo mkakati kama huu wa kutoa nafasi kwa wengine ili waongeze nadhani ni mzuri. Nimechukua uamuzi huu mchana na tayari nimeshasambaza barua kunakohusika na nakala ipo hadi kwa Spika."

Baraza kivuli la mawaziri lililotangazwa Februari mwaka huu linaundwa na wabunge wa Chadema pekee.
 
Ameishaona mambo ndivyo sivyo ndani CDM a.k.a. MAGWANDA, sasa hapo kwa nn asijiuzulu ili kulinda heshima yake na ya ukoo wake
 
Kujiuzuru ni kuzuri, lakini sababu ya msingi ni ipi?

Mwenye kujua sababu za kujiuzuru kwake atujulishe


Sababu anataka kuwaachia na wengine wapate uzoefu, na hio ndo demokrasia.ukiona ngoma haieleweki achia ngazi...usiwe kama nanii!
 
Letcia , anadhani ile nafasi ni yafamilia ya nyumbani kwake ! ile post ni ya umma, anapojiuzulu ni vyema akawajuza wananchi, iwe kwa maslahi ya chama, taifa au ya kwake binafsi.
19144_100229920007453_100000613353513_3411_1109588_n.jpg



 
Hata kujiuzuru kwake ni kivuli, sasa Regia chukua na hicho kivuli maana unapenda sana vivuli.
 
I salute Leticia! Lets be positive on her move. Kumbukeni ni waziri kivuli (waziri copy) siyo waziri mwenyewe hivyo impact siyo kihivyo kama mawaziri wa CCM wenye nguvu za kisheria!!!
 
Kuchanganya mapenzi na kazi ni sumu, Ngoswe penzi kitovu cha uzembe.
 
Mbona Kafanya Fasta!
Awaachie wengine wapate uzoefu wakati yeye Hana Uzoefu!Kuna Kitu Kaficha!
Ila kumbukumbu zangu zinaniambia huyo Letisia Siyo Mke tena wa Mtoto wa Ukoo bora!
Ila anakula Mafao ya jina la Nyerere!
Kasheshe!
 
Back
Top Bottom