Lambardi
JF-Expert Member
- Feb 7, 2008
- 16,499
- 17,373
Aache upuuzi....wake tena asitufanye sisi wapuuzi awache upuuzim..Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo amesema kwa mujibu wa mujibu wa sensa ya viwanda ya Julai 2021 (NBS/WVB), idadi ya viwanda ni 80,969
Amebainisha kuwa kati ya viwanda hivyo, Viwanda vikubwa ni 628, Viwanda vya kati ni 684, Viwanda vidogo ni 17,267 na Viwanda vidogo sana ni 62,400
Ameeleza kuwa kisera, tafsiri ya ukubwa wa kiwanda ni kuwa Kiwanda kikubwa kina ajira zaidi ya 100 na uwekezaji wa zaidi ya Milioni 800
Kiwanda cha kati kina ajira 50-99 na uwekezaji wa Milioni 200 hadi Milioni 800. Kiwanda Kidogo kina ajira 5-49 na uwekezaji wa Milioni 5 hadi Milioni 200. Kiwanda kidogo sana kina ajira 1-4 na uwekezaji wa chini ya Milioni 5