Waziri kapuya ndani ya pekecha pekecha kujiandaa na mgomo wa tucta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri kapuya ndani ya pekecha pekecha kujiandaa na mgomo wa tucta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sijafulia, Mar 27, 2010.

 1. s

  sijafulia Member

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Katika hali isiyo ya kawaida kwa viongozi wa juu nchini kuonekana katika kumbi za starehe tena katika sare sambamba na waimbaji wa bendi, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya aliingia ukumbini na kuyarudi mapigo ya pekecha pekecha ya wana wa Akudo.Huku akiwa amevalia sare sawa na waimbaji wa bendi ya Akudo, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya alijitosa ukumbini na kuanza kuyarudi mapigo ya pekecha pekecha ya bendi ya Akudo Impact iliyokuwa ikitoa burudani kwenye ukumbi wa Msasani Beach.

  Kapuya ambaye ndiye mmliki wa bendi hiyo alijimwaga stejini na kusakata muziki kwa nguvu zote huku jasho likimtoka akiwa pamoja na mpambe wake ambaye jina lake halikufahamika.

  Kapuya anakuwa kiongozi wa pili wa juu serikalini kumiliki bendi wa kwanza alikuwa Waziri Mdhihiri Mdhihiri ambaye aliwahi kumiliki bendi ya Mchinga Sound ambayo baadaye ilivunjika.

  Kutokana na jinsi anavyoithamini bendi yake, waziri Kapuya amefanikiwa kuifanya bendi ya Akudo iwe miongoni mwa bendi zinazopendwa sana nchini kiasi cha kuleta ushindani mkubwa katika medani ya muziki wa dansi hapa nchini.

  WAZIRI KAPUYA AKIJIANDA NA MAZOEZI YA MGOMO WA TUCTA HAPA AKIWA KWENYE ""PEKECHA PEKECHA"""AKUDO ...KAMA UNA MUDA KARIBU UMWONE WAZIRI WETU AKIFURAHIA MAISHA.NI MMOJA WA MAWAZIRI ANAEMILIKI BENDI ..MWINGINE ALIKUWA MH MUDHIHIRI MUDHIRI!!!

  SRCE NIFAHAMISHE DOTI COMU
   

  Attached Files:

 2. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,807
  Likes Received: 1,142
  Trophy Points: 280
  mkuu hii kitu ipo hapa jamvini tayari mkuu,mods unganisheni hizi mada
   
 3. s

  sijafulia Member

  #3
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ooohh ahsante mkulu
  sijaona uzee
   
 4. m

  matambo JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  is it immoral for him to attend the concert?
  i just want to know
   
 5. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Hili ni dogo.
  Ukitaka kumfahamu Kapuya, Uliza waliokuwa naye pale UDSM. Utasikia uchafu wa mkuu huyu kiasi cha kutia wasiwasi ya uzima wa akili yake.

  BTW, jamaa huyu nilisikia siyo m-TZ. ana asili ya nchi ya Burundi na hakuwahi kuingia uraia rasmi. Ndivyo nilivyowahi sikia.
   
Loading...