Waziri Kamwelwe asema atawaweka ndani wote wanaohoji ajiuzulu kutokana na MV Nyerere kuzama

Wew

Wewe ndio una matatizo ya akili,kujiuzulu sio kwamba yeye alitakiwa akahesabu abiria,kujiuzulu ni kuwajibika kwa uzembe uliofanywa na waliochini ya uongozi wako. Siamini kama haya maneno aliyatoa waziri..hata kama hajasoma hata modole moja ya uongozi. Hivi viongozi kuweka watu ndani siku hizi ndio jambo la kujivunia!.Hii awamu ni ya kishetani.
Akisha jiuzuru what next?
 
Tatizo watanzania wengi wana matatizo vichwani. Swali unaulizwa alitakiwa alijibu yeye kama kiongozi, hasira na povu lote la kutisha kuwaweka watu mahabusu lilitoka wapi?. Uongozi ni kazi sana, kupanic kunatoka wapi?....kiongozi unashusha presha unawajibu kawaida kutoonesha hasira za namna hiyo. Ukosefu wa uvumilivu/ustahimilivu kwa kiongozi ni hatari sana!!!.

Hahaha!, ajibu bila kuwatisha mbona inawezekana. Watu wana hasira wamepoteza ndg, jamaa, marafiki, wapiga kula, washabiki wa miziki, wachezaji, watumishi, wakulima, nk... kwahiyo kila mtu ana hasira hapo. Mm kama msanii siku leo nikienda ukerewe kufanya shoo wajue mashabiki zangu watakuwa wamepungua kwasababu ya hiyo ajari nk... kila idara imeumia kwa kiwango chake. Watujibu taratibu maswali wanayoulizwa, wala wasitumie hasira za kupanic na kutisha watu
 
Mkuu.
Hiyo ya mwinyi sikuwahi kuifahamu
Lakini nina swali
Mbona tunasikia ilikuepo bodi na mamlaka ya kusimamia hayo mambo sijui inaitwa Eula kama sijakosea
Na hiyo bodi ilikua chini ya mwanajeshi fulani sasa swali langu ni kuwa
Ile bodi na mamlaka ipo chini ya waziri ? Kama ndio je rais si ameshaifumua pamoja na yule mwanajeshi kufukuzwa hii si inatosha mkuu ?
Nilichogundua ni kuwa huna kosa kuuliza isipokuwa unakosa kitu kinaitwa maarifa ya namna ofisi za umma zinapaswa kuwa hususani taaratibu za kawaida za kiuendeshaji.
.
.
Kuachia madaraka ya kiofisi baada ya kutokea dosari kwenye taasisi au sekta unayoiongoza au kutokana na tabia za kiongozi husika si adhabu bali ni sehemu ya uwajibikaji wa kawaida na kulinda heshima ya taasisi au ofisi husika na hata kiongozi husika ili ofisi na kiongozi huyo waendelee kupata heshima kama ilivyokuwa awali.
Mfano;Ally Hassan Mwinyi.

Si swala la ajabu kwenye nchi za kidemokrasia na lisichukuliwe kama adhabu au kitu kingine kinachofanana na hicho.
.
.
Ipo mifano ya mawaziri wengi nchi za wenzetu wanaoachia ngazi kutokana tu na majanga ya asili licha ya waziri au kiongozi husika kutoyasababisha.
 
Ngoja tuone...

Ingekua nchi za wenzetu penye demokrasia... kwa matamshi hayo... maandamano yangeitishwa nchi nzima ajiuzulu...

Cc: mahondaw
 
Yaani
Mbona Mwinyi alijiuzulu uwaziri kwa issue tu ya mauaji ya vikongwe ambapo kimsingi yeye hakuhusika ila alijiuzulu kuonyesha uwajibikaji kama kiongozi

Kama waziri alipaswa kuweka mipango na system nzuri kumonitor kiwango cha abiria kwenye vivuko kwa sababu hakuna hicho kitu ndiyo maana tunaona haya maana siyo mfuatiliaji huyo wanaotaka ajiuzulu wana hoja Mkuu
Yaani badala ya kutafutia tatizo ufumbuzi we unajiudhuru?? Sasa kujiudhuru ni kuwajibika au kujitenga na uwajibikaji??sasa mbona mlimkejeli dr silaa alipojiudhuru baada ya kuona jitihada zake za kupambana na ufisadi hazijazaa matunda?
 
Huyu KAMWELE ivi anangoja nn kung'oka mpaka sasa??! Kama anakwama rais nae anakwama nini kutuondolea hii garbage??
 
“Tupo katika masuala ya uokoaji na msiba ninyi mnaleta masuala ya kisiasa, hilo siyo swali, nashangaa watu wapo katika majonzi ninyi hamuonyeshi majonzi, mkieendelea kuuliza nitawaweka mahabusu” Waziri Mh. Izack Kamwelwe akijibu kuhusu wanaotaka ajiuzulu.

ukiona waziri anatishia nyau ujue amechungulia shimo. sasa mimi najiuliza kwanini asijiudhuru au njaa kali?
 
“Tupo katika masuala ya uokoaji na msiba ninyi mnaleta masuala ya kisiasa, hilo siyo swali, nashangaa watu wapo katika majonzi ninyi hamuonyeshi majonzi, mkieendelea kuuliza nitawaweka mahabusu” Waziri Mh. Izack Kamwelwe akijibu kuhusu wanaotaka ajiuzulu.
Ningekuwa mimi namuweka ndani kabisaa huyo mwandishi, mpaka achangie uokoaji.
 
“Tupo katika masuala ya uokoaji na msiba ninyi mnaleta masuala ya kisiasa, hilo siyo swali, nashangaa watu wapo katika majonzi ninyi hamuonyeshi majonzi, mkieendelea kuuliza nitawaweka mahabusu” Waziri Mh. Izack Kamwelwe akijibu kuhusu wanaotaka ajiuzulu.
afadhali ya lawama kuliko fedhea
 
Mkuu kwa heshima na taadhima naomba unitajie viongozi 5 wa afrika 3 na nje ya Africa 2 ambao wamewahi kujiuzulu kisa uzembe wa watu waliochini yao
Mwinyi alipokuwa waziri wa mambo ya ndani alijiuzulu kwa kashfa ya polisi wa chiniwaliokuwa wakiua wazee kwa tuhuma za uchawi
 
“Tupo katika masuala ya uokoaji na msiba ninyi mnaleta masuala ya kisiasa, hilo siyo swali, nashangaa watu wapo katika majonzi ninyi hamuonyeshi majonzi, mkieendelea kuuliza nitawaweka mahabusu” Waziri Mh. Izack Kamwelwe akijibu kuhusu wanaotaka ajiuzulu.
heshima na uwajibikaji (collective responsibility) ilitakiwa ajiuzulu day one... Kisha ashiriki msiba akiwa nje ya ofisi
 
Back
Top Bottom