Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,697
- 9,048
Sijui hadidu za rejea kwa Tume ya Jeneral mstahafu Waistara katika uchunguzi wa chanzo cha kuzama kwa MV Nyerere hadi kupelekea kupotea kwa maisha ya Watanzania 224.
Mimi kama raia napenda kumshauri Kiongozi wa Tume Jenerali Waistara aanze na kuchunguza Mapato ya Kivuko hichi kwa muda wote kilipokuwa kinafanya kazi kabla ya ajali. Tunajua uwezo wa MV. Nyerere ni abiria 101, Tani 25 za Mizigo na magari 3 tu. Kama kweli hawa Wafanyakazi wa MV.Nyerere walikuwa wanabeba idadi ya Abiria na Mizigo inayotakiwa basi Mapato yake yatakuwa constant kwa safari hizo 2 kwa siku, kwa wiki, mwezi na mwaka.
Kama walikuw awanzidisha abiria kila siku kwa ujazo wa karibu mara 2 au 3 na mizigo kadhalika tunategemea Mapato yalikuwa ni makubwa sana na Serikali ilikuwa inapata mapato mazuri lakini kwa kuvunja sheria. Hapa ndipo tunaweza kujua kama Serikali ilikuwa ikijinufaisha kwa mapato haya ya ujanja ujanja.
Iwapo Makusanyo siku zote yalikuwa wastani kwa kiwango cha abiria 101 na mizigo tani 25 kwa siku kutwa mara 2 kwa miaka yote(2004-2018) basi TEMESA,SUMATRA na WATUMISHI WOTE MAZI GA NYANZA. Na iwapo Serikali ilikuwa inakusanya mapato makubwa kupindukia kutokana na kuzidisha Mizigo na Abiria basi SERIKALI IWAJIBIKE kwa maana ya Waziri mwenye dhamana na Timu yake. Waziri wa Ujenzi Mhe. KAMWELWE aache kuwatisha watu wanaomtaka ajiuzulu kuwa atawaweka ndani!!!.
Kujiuzulu ni sehemu ya Uongozi kuonesha kuwa umewajibika kwa madudu yaliyotokea chini ya Wizara unayoisimamia ingawa wewe mwenyewe huhusiki moja kwa moja.
Kamwele anatakiwa akapate ushauri nasaha kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya 2 Mzee Alhaji Ali Hassani Mwinyi ambaye mwaka 1974 alijiuzulu kutokana na mauaji ya vikongwe yaliyofanywa na Jeshi la Polisi yeye akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani....Lakini huyuhuyu Mzee Mwinyi mwaka 1985 akaja kuwa Rais wa Awamu 2...Simple!