Waziri Kamwelwe asema atawaweka ndani wote wanaohoji ajiuzulu kutokana na MV Nyerere kuzama

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
“Tupo katika masuala ya uokoaji na msiba ninyi mnaleta masuala ya kisiasa, hilo siyo swali, nashangaa watu wapo katika majonzi ninyi hamuonyeshi majonzi, mkieendelea kuuliza nitawaweka mahabusu” Waziri Mh. Izack Kamwelwe akijibu kuhusu wanaotaka ajiuzulu.
 
Wew
Ila siasa zetu unajua za ajabu sana
Huyu mzee ni mzito mno ni vigumu kusimamia abiria wa vivuko yani atoke dodom aende ukerewe kuhesabu watu

Hao wanaotaka afukuzwe wanatatizo la akili
Wewe ndio una matatizo ya akili,kujiuzulu sio kwamba yeye alitakiwa akahesabu abiria,kujiuzulu ni kuwajibika kwa uzembe uliofanywa na waliochini ya uongozi wako. Siamini kama haya maneno aliyatoa waziri..hata kama hajasoma hata modole moja ya uongozi. Hivi viongozi kuweka watu ndani siku hizi ndio jambo la kujivunia!.Hii awamu ni ya kishetani.
 
Mkuu kwa heshima na taadhima naomba unitajie viongozi 5 wa afrika 3 na nje ya Africa 2 ambao wamewahi kujiuzulu kisa uzembe wa watu waliochini yao
 
Ila siasa zetu unajua za ajabu sana
Huyu mzee ni mzito mno ni vigumu kusimamia abiria wa vivuko yani atoke dodom aende ukerewe kuhesabu watu

Hao wanaotaka afukuzwe wanatatizo la akili
Mbona Mwinyi alijiuzulu uwaziri kwa issue tu ya mauaji ya vikongwe ambapo kimsingi yeye hakuhusika ila alijiuzulu kuonyesha uwajibikaji kama kiongozi

Kama waziri alipaswa kuweka mipango na system nzuri kumonitor kiwango cha abiria kwenye vivuko kwa sababu hakuna hicho kitu ndiyo maana tunaona haya maana siyo mfuatiliaji huyo wanaotaka ajiuzulu wana hoja Mkuu
 
Mbona Mwinyi alijiuzulu uwaziri kwa issue tu ya wale mahabusu kujazwa kupita uwezo wa selo kwani yeye alienda kuwahesabu

Kama waziri alipaswa kuweka mipango na system nzuri kumonitor kiwango cha abiria kwenye vivuko kwa sababu hakuna hicho kitu ndiyo maana tunaona haya maana siyo mfuatiliaji huyo wanaotaka ajiuzulu wana hoja Mkuu
Mkuu.
Hiyo ya mwinyi sikuwahi kuifahamu
Lakini nina swali
Mbona tunasikia ilikuepo bodi na mamlaka ya kusimamia hayo mambo sijui inaitwa Eula kama sijakosea
Na hiyo bodi ilikua chini ya mwanajeshi fulani sasa swali langu ni kuwa
Ile bodi na mamlaka ipo chini ya waziri ? Kama ndio je rais si ameshaifumua pamoja na yule mwanajeshi kufukuzwa hii si inatosha mkuu ?
 
Mkuu kwa heshima na taadhima naomba unitajie viongozi 5 wa afrika 3 na nje ya Africa 2 ambao wamewahi kujiuzulu kisa uzembe wa watu waliochini yao
JANA KUNA HABARI ILIKUWA INAZUNGUKA YA WAZIRI WA KOREA ALIYEJIUZULU KWA SABABU YA KIVUKO KUZAMA. JAPO NAJUA HABARI HIYO NI YA KITAMBO ILA JANA ILIPANDISHWA KWA MAKUSUDI ILI VIONGOZI WETU WAIONE. PIA MZEE ALI HASSAN MWINYI ALIJIUZULU UWAZIRI WA MAMBO YA NDANI KWA MAUAJI YALIYOTKEA TABORA (KAMA NIMEKOSEA ENEO NISAHIHISHWE)
 
“Tupo katika masuala ya uokoaji na msiba ninyi mnaleta masuala ya kisiasa, hilo siyo swali, nashangaa watu wapo katika majonzi ninyi hamuonyeshi majonzi, mkieendelea kuuliza nitawaweka mahabusu” Waziri Mh. Izack Kamwelwe akijibu kuhusu wanaotaka ajiuzulu.
Akishawaweka mahabusu nini kinafuata? After all hayo ni maswali tu yana ugumu gani kuyajibu? Si tumeambiwa na Job kuwa wao ni wasomi?
 
“Tupo katika masuala ya uokoaji na msiba ninyi mnaleta masuala ya kisiasa, hilo siyo swali, nashangaa watu wapo katika majonzi ninyi hamuonyeshi majonzi, mkieendelea kuuliza nitawaweka mahabusu” Waziri Mh. Izack Kamwelwe akijibu kuhusu wanaotaka ajiuzulu.
Hahahaaaa jamaa kafura kinyama baada ya kuona kitumbua chake kanataka kutiwa mchanga.
 
Back
Top Bottom