Waziri Hussein Mwinyi awataka waganga wa kienyeji wapeleke dawa zao NIMR

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Waziri wa afya Dr. Hussen, amewataka waganga wa kienyeji wapeleke dawa zao NIMR ili zichunguzwe kama hazina madhara.

"Hizi dawa za kienyeji zimekuwa zikisaidia sana watanzania, sasa imefikia wakati wa dawa hizi kupelekwa nimr ili zifanyiwe uhakiki kama hazina madhara, wapo ambao wameshaanza kupeleka dawa NIMR"

MY VIEW:
Kipindi cha nyuma kuna waziri alipiga marufuku waganga wa kienyeji na kuagiza wafutiwe leseni. Imekuaje sasa? serikali imeshindwa kununua dawa za kuwahudumia watanzania? Ikoje hii?

mia
 
Hakuna waziri aliyewahi kupiga marufuku waganga wa kienyeji Tanzania. Kinachofanyika siku zote ni kuwahamasisha wafuate taratibu za kujisajiri ili watambulike rasmi...
 
Waziri wa afya Dr. Hussen, amewataka waganga wa kienyeji wapeleke dawa zao NIMR ili zichunguzwe kama hazina madhara. "Hizi dawa za kienyeji zimekuwa zikisaidia sana watanzania, sasa imefikia wakati wa dawa hizi kupelekwa nimr ili zifanyiwe uhakiki kama hazina madhara. wapo ambao wameshaanza kupeleka dawa nimr.MY VIEW;Kipindi cha nyuma kuna waziri alipiga marufuku waganga wa kienyeji na kuagiza wafutiwe leseni. Imekuaje sasa? serikali imeshindwa kununua dawa za kuwahudumia watanzania?Ikoje hii?. mia

Kuna wakati Tanzania walipiga marufuku kuvaa vi mini na suruali zilizobana. Mbona sasa zinavaliwa? Ikoje hiyo?
 
Duh?!..Sijaelewa halisi, katika medicine kuna kitu kinaitwa Alternative medicine, which is partially acceptable, swali langu ni vipi je ndiyo hii au wanataka ile ya Traditional healer"wapiga ramli" ndio ihalalishwe?..msaada wakuu.
 
Unajuan sometime kama hujawa covered kwa muda mrefu na vyombo vya habari ndo madhara yake haya.

Nafikiri wanataka kuleta mambo kama yale ya loliondo kwa babu. kwanini serikali isitoe huduma za afya za kutosha?. Mi naona hawa waganga wa kienyeji tusiitegemee sana. mia
 
Kuna wakati Tanzania walipiga marufuku kuvaa vi mini na suruali zilizobana. Mbona sasa zinavaliwa? Ikoje hiyo?

wakati gani huo? elezea vizuri. Mi ninachojua ni zanzibar ndo walikatazwa kuvaa vimini wakati wa ramadhan. Mia
 
Duh?!..Sijaelewa halisi, katika medicine kuna kitu kinaitwa Alternative medicine, which is partially acceptable, swali langu ni vipi je ndiyo hii au wanataka ile ya Traditional healer"wapiga ramli" ndio ihalalishwe?..msaada wakuu.

yeye kazungumzia dawa za kienyeji zote zipelekwe nimr. mia
 
Hakuna waziri aliyewahi kupiga marufuku waganga wa kienyeji Tanzania. Kinachofanyika siku zote ni kuwahamasisha wafuate taratibu za kujisajiri ili watambulike rasmi...

Ni Pinda alietoa kauli ya kufuta leseni za waganga wa kienyeji,ni baada ya kukithiri kwa mauaji ya maalbino nchini. Hatua iliyofikia Pm.Pinda kulia bungeni.!
 
yeye kazungumzia dawa za kienyeji zote zipelekwe nimr. mia


Tanzania leo hii haina TOXICOLOGY SCREENING, huwa nashindwa kuelewa wanapitishaje/wanaruhusu madawa kwa namna gani kutumiwa na wananchi ikiwa hata uwezo wa kutamvua kemikali zilizo ndani ya dawa husika hatuna.
..na kuja kugundua wanaruhusu tu dawa kutumika kama wakiona madhara kadhaa yanayoweza kutokea mapema(Immediate drug effects) hayataonekana...but then what abt long term effects?

Tanzania tutaendelea kuwa "wasanii" hivi hivi, nakumbuka enzi za kikombe cha babu, viongozi wakuu wa Nchi wote walikwenda kule, then wananchi wa kawaida nk.. i was wondering where is the National Security?
Je, dawa ikianzishwa sasa na madhara yakawa baada ya miezi/miaka kadhaa, tutajua? Je hatuwezi kupoteza viongozi wetu wa nchi kirahisi namna hii? what abt wananchi pia?.. ikiwa Tanzania Food and Drug Authority(TFDA) wanaporuhusu madawa kutumika kama walipoidhinisha vikombe kutumika(bse vilikuwa almost kila sehemu nchi)..wananchi wakiacha kutumia tena dawa!! nakumbuka kufiwa kwa wagonjwa watatu mikononi mwangu, simply bse waliacha kutumia dawa zao...

What if a rogue pharmacist/chemist etc use above means, Je tutafika?..Again where is the Nations' Health security, especially now with Minister's statment?!!
 
Back
Top Bottom