Waziri wa Afya, Dkt. Gwajima ataka fedha za dawa ziheshimike

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Viongozi wa vituo vya kutolea huduma za afya vya umma wametakiwa kuheshimu fedha za dawa kadri zilivyopangwa kwenye bajeti ya Serikali kuu na vyanzo vingine ili kuweza kuondoa kero ya upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya afya nchini.

Rai hiyo imetolewa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 21 wa kutathimini utekelezaji wa vipaumbele vya kisera katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dodoma.

Dkt. Gwajima amesema kuwa bado kuna maoni mengi kutoka kwa wananchi kuhusiana na ukosefu wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini,hivyo viongozi wa hospitali na vituo vya kutolea huduma vya umma wanapaswa kuanisha matumizi ya fedha za dawa walizopokea au kutoka kwenye makusanyo ya mapato ya hospitali hiyo Pamoja na matumizi yake.

“Ili kufikia azma ya Mhe. Rais, sisi kama sekta ya afya inabidi kuongeza kasi katika uwajibikaji wa Pamoja katika malengo tuliyoyaweka, ni lazima tufanye upekuzi wa matumizi ya fedha za dawa,vifaa na maabara lazima ziheshimike na kufika kwa mgonjwa ili wananchi watuamini na kuweza kutatua kero zao”. Alisema

Aidha, Dkt. Gwajima amesema katika kutekeleza hilo, Wizara itatoa maelekezo ya kuongeza ufanisi katika uwajibikaji kuanzia kwa watumishi wote wa sekta ya afya,ngazi mbalimbali za usimamizi na uendeshaji katika sekta na taasisi zilizo chini ya wizara Pamoja na wadau wote wanaotekeleza masuala mbalimbali katika sekta ya afya.

Hata hivyo Dkt. Gwajima amewahimiza wadau wote kuweka kipaumbele kwenye utekelezaji kwa kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa na serikali kwa miaka mitano ijayo (2020-2025),kwa uwajibikaji wa Pamoja katika ngazi zote za kutolea huduma za afya nchini na hivyo kuboresha huduma zitakazotolewa ili kuwafikia wananchi wote na kuwapatia huduma kulingana na mahitaji ya kiafya yanayowakabili.

Aliongeza kuwa licha ya mafanikio ya sekta ya afya nchini ,sekta hiyo bado inaendelea kuwa na changamoto ambazo juhudi za Pamoja zinahitajika ili kukabiliana nazo ikiwepo ile ya wananchi wengi bado wako nje ya mfumo wa bima ya afya na hivyo kukosa huduma za afya kwa wakati kutokana na changamoto za kifedha ambapo hadi sasa ni asilimia 11 tu ndio wamejiunga.

Kwa upande wa tiba asili na tiba mbadala Dkt. Gwajima amesema zimekuwa zikisaidia katika kutibu magonjwa mbalimbali kwa wananchi na hivyo serikali inakusudia kuimarisha kitengo cha utafiti wa tiba mbadala.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amesema ili kufikia lengo la kuwawezesha wananchi wote kuwa na bima ya afya kunahitajika kuimarisha kwa mifuko ya bima ya afya na ili kuwafikia wananchi wengi zaidi ni kuweza kukamilisha mpango mkakati wa sera ya ugharamiaji wa huduma za afya Pamoja na sheria ya bima kwa wote.

“Mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa kwa sasa unachangia asilimia 5 ya wanufaika wote waliojiunga katika mifuko ya bima za afya nchini na katika kipindi cha utekelezaji wa mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa kuanzia Julai 2018 tumefanikiwa kusajili kaya 557,882 sawa na wanufaika 3,347,112 kufikia Novemba 2020”. Alisema Dkt. Dugange.

Hata hivyo amesema jumla ya shilingi bilioni 16.2 zimekusanywa katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2020 ambapo zimewezesha kuimarisha huduma za afya kwenye vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na kuwawezesha wananchi yakiwemo makundi maalum kuzifikia huduma hizo bila vikwazo vya kifedha.

Wakati huo huo, Naibu Waziri wa afya Dkt. Godwin Mollel amesema upo uwezekano wa sekta ya afya kufanya vizuri endapo viongozi na wadau wa maendeleo wakijipanga na kushirikiana ili kufikia malengo ya kuwahakikishia watanzania wanapata huduma za afya bora na kwa uhakika.

Dkt. Mollel amesema matatizo na kero nyingi ambazo zipo kwa wananchi zinahitaji uelewa kwani wananchi wengi bado hawajafikiwa na hii ni kutokana na mfumo wa mawasiliano,hivyo amewata waganga wakuu wa Mkioa,Wilaya na waganga wafawidhi wa hospitali kutoa mawasiliano yao ili wananchi waweze kusaidiwa pale pasipohitaji msaada.
 
Yeye ndiyo anafikili ndiye wa kwanza kuwa waziri wa afya? Yake maduka ya dawa yalivyofunguliwa kwa mbwembwe yameishia wapi?

Walipiga marufuku wagonjwa kupelekewa vyakula pa mhimbili, eti wagonjwa Watapikiwa na Hospital, sijui hilo igizo liliishaje?
 
Yeye ndiyo anafikili ndiye wa kwanza kuwa waziri wa afya? Yake maduka ya dawa yalivyofunguliwa kwa mbwembwe yameishia wapi?

Walipiga marufuku wagonjwa kupelekewa vyakula pa mhimbili, eti wagonjwa Watapikiwa na Hospital, sijui hilo igizo liliishaje?

Ukitaka kujua zaidi nenda katafute dawa pale MSD Muhimbili ndipo tongotongo zitakutoka
 
Back
Top Bottom