Waziri Dkt Ndugulile aipongeza TTCL uboreshaji vituo vya huduma kwa wateja

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Na Mwandishi wetu - Zanzibar

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe Dkt Faustine Ndugulile aipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania kwa kuboresha muonekano wa Vituo vya Huduma kwa Wateja nchi nzima ili kuongeza mvuto kwa wateja wa huduma za mawasiliano.

Amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja uliofanyika katika ofisi za Shirika hilo zilizoko Kijangwani katika Mkoa wa Mjini Magharib- Unguja Zanzibar.

“Nawapongeza TTCL Corporation kwa ukarabati mkubwa mliofanya katika kuleta muonekano mpya wa ofisi yenu hii, mmeboresha mazingira ya utoaji huduma na ninaamini Kituo hiki kitaleta mvuto kwa wateja wetu kuja kupata huduma” amesema Dkt. Faustine Ndugulile (Mb).

Waziri aliongeza kuwa pamoja na muonekano mpya huo ambao utasaidia kuleta mvuto wa kibiashara kwa wateja wa bidhaa na huduma za shirika hilo amewapa rai watumishi na watoa huduma wa TTCL kuendelea kuboresha huduma na utoaji wa huduma hizo ili kuifanya Kauli Mbiu ya Shirika hilo ya Rudi Nyumbani Kumenoga kuwa na uhalisia.

Aliongeza kuwa Wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania wanapaswa kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wateja wao huku wakizingatia uzalendo, weledi, kasi na kutafuta masoko badala ya kusuburia wateja ofisini.

Naye, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe, Rahma Kassimu alisema Wizara yake itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na TTCL ili kuhakikisha huduma bora za mawasiliano kwa wateja zinatolewa kwa wananchi wa Zanzibar.

IMG-20210312-WA0054.jpg
IMG-20210312-WA0050.jpg
IMG-20210312-WA0053.jpg
IMG-20210312-WA0052.jpg
IMG-20210312-WA0051.jpg
 
Wangeboresha Kwanza upatikanaji wa vocha za vikaratasi na mawakala wa miamala ya simu.

Kama vocha mtaani hamna

Hiyo huduma kwawateja itakwenda kuhudumia nini sasa.

Nnachokiona

Kelele nyiiiingi, utekelezaji na ufanisi ni sifuri.
 
Sionagi tofauti ya vifurushi kati ya TTCL na mitandao mingine taabu tupu.
 
TTCL hawa hawa wanaotuuzia MODEM zinazopendeza kwa macho kwa 60000+ na bila aibu wanakwambia hawatoi risiti, kama ukihitaji risiti urudi siku nyingine?

TTCL hawa hawa ambao mtandao wake unasuasua na kutoa huduma mbovu ya internet kwa bei ile ile ya washidani wao lakini kwa ufanisi angalau?

Waziri hakutakiwa kushabikia ufunguzi wa vibanda vya huduma mbovu kwa wateja tena vyenye gharama kubwa kuliko tija... TTCL inahujumiwa.😳
 
Back
Top Bottom