Waziri Chamurilo: Familia(Mfugale) wameonesha sintofahamu (ombwe) kwamba ilikuwa haifahamu, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya kikaoni

Jamani kuweni makini na hizo AC hasa ukiwa na magonjwa nyemelezi.
Kuna maofisi mengi tu watu wanajiua kimya kimya. Yaani unaingia ofisini unakuta baridi ya kwenye friji! Wapendwa! Mnajiua!
Ukiwa na AC zingatia yafuatayo:
1. Room temperature
2. Refrigerant iliyopo ndani ina madhara gani? Refrigerant nyingi huku Tz ni sumu kamili!
Nothing to do with AC!
Inaweza kuwa ni heart issue, BP na mengine mengi.
Kama tatizo lilikuwa ni AC ingewazuru pia wengine kwenye hiyo ofisi!
 
Jamani, tunahitaji kujifunza kuwa na uharaka wa kuwasaidia wale tunaokuwa nao penye changamoto za afya.
Mfano, mtu anatoka kwenye kikao kwamba anajisikia vibaya, akimbizwe hospital badala ya ofisi nyingine kupumzika.
Anaposema ongezeni AC iwe baridi zaidi, ninadhani ilikuwa ni muda muafaka wa kuita Dr.
Hata hivyo, hizi ni juhudi za kibinadamu ambazo zina ukomo.

Natoa pole sana kwa familia yake, pamoja na ndugu, marafiki na wale aliokuwa nao mkutanoni.
Watu wengine hapa Tanzania hawana elimu ya huduma ya kwanza. Wangeweza hata ku check heart rate(pulse) manually, and respiration!
 
Kikao kilisogezwa mbele kwa kuwa alikuwa na majukumu mengine kaja kwenye kikao hajisikii vizuri kikao kinaendelea kaambiwa kapumzike sasa kikao kilihairishwa kwa sababu zipi? kwa haraka uwepo wake haukuwa wa lazima huwezi kusukuma masiku kikao kwa kuwa hatoweza kuja siku kaja hawezi kukaa kwenye kikao lakini kapumzike kikao kinaendelea hivi inaingia kwenye akili kweli? mtu mzima hajisikii vizuri kitu cha kwanza utaita first aid na kikako utahairisha kidogo kumshughulikia key person kwenye kikao sio nenda kampumzike kwani alisema kachoka au hajisikii vizuri? Kufa kwa ghafla kupo sana tu na sisemi labda kafanyiwa kitu ila uwezo wetu wa ku deal na emergency ni very poor au hakuna kabisa. pale mji wa serikali ni lazima ijengwe clinic first aid kwa wafanyakazi wa wizara zote pale.
We nae husomi.?
Alisema hajiskii vizuri lakini alikua anaweza kutembea mwenyewe ndo akaenda kujiskilizia kwanza chumba kingine..

haya hio first aid ukileta utafanya nini?.
Hata mkiahirisha kikao ndo yule anapona?.
 
Mkuu,
First aid(Huduma ya kwanza) ina serve life.
 
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamurilo: Poleni sana kwa kumpoteza Injinia Patrick Aron Mfugale, mheshimiwa Rais tumesikia maelezo mengi yametolewa kuhusu elimu na ajira ya marehemu, tumesikia vilivile kuhusu mchango wake wa kitaalamu, tumesikia vilevile kuhusu tuzo mbalimbali ambazo amezipata kutokana na utumishi wake uliotukuka.

Vilevile tumepata ushuhuda kutoka kwa watoto na viongozi mbalimbali walioshiriki katika miradi ambayo ameisimamia, itoshe hapo nisiongeze mengine bali niseme nasi tuendelee kumuenzi katika yale aliyokuwa akiyafanya na tujitahidi kadri tuwezavyo kuhaulisha yale yote aliyoyasimamia ili nasi tuendelee kuyafanya kama alivyokuwa akiyatekeleza.

Mheshimiwa Rais, katika salamu za familia wameonyesha ombwe kwamba familia ilikuwa haifahamu ni jinsi gani limetokea na mimi kama msimamizi mkuu wa wizara ninawajibika kutoa maelezo mafupi.

Katika uongozi wa wizara tuna mikutano mbalimbali na ambapo tulikuwa na mkutano kati ya wizara na Tanroads siku ya Ijumaa wiki iliyopita ambao haukufanyika kwasababu marehemu aliomba kikao kisogezwe hadi Jumanne kwani alikuwa ana majukumu mengine ambayo kasababu hakuweza kuyaahirisha.

Kwasababu tunafanya kazi pamoja tuliridhia ombi hilo na kikao kilifanyika Jumanne kama ilivyopangwa, Jumanne tuliamka mimi nikaelekea Bungeni na katibu mkuu wangu sekta ya ujenzi aliongoza kikao hicho.

Katika kikao hicho majira ya saa nne, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya na ndipo katika mkuu akamueleza aende akapumzike katika ofisi jirani ambayo ni ofisi yake ili kikao kiendelee.

Aliamka mwenyewe bila usaidizi wowote na kwenda katika ofisi ya katibu mkuu sekta ya Ujenzi na kikao kiliendelea lakini katibu mkuu aliwaambia kwenye kikao endeleeni na kikao kwanza niende nikamuangalie mhandisi mfugale kisha tuje naye tuendelee na kikao chetu.

Katibu mkuu alipofika ofisini kwake, alimkuta marehemu ameketi kwenye kiti lakini alionekana dhahiri hali yake si nzuri kwahiyo aliuliza wale wasaidizi, kumetokea nini.

Wasaidizi wakasema hapana, alipofika hapa aliomba kiyoyozi kiongezwe ubaridi, kitu ambacho kilifanywa kisha akaketi kwenye kiti, kwahiyo katibu mkuu alifanya uratibu haraka wa magari pale na kumchukua marehemu Mfugale kumtia kwenye gari na kumkimbiza katika hospitali ya Benjamin Mkapa, wakati huo alifanya uratibu na katibu mkuu Afya ambae aliandaa madaktari ambao walipofika pale Benjamin Mkapa, walikuta wanasubiriwa na wakamchukua na kumkimbiza ili apate huduma stahiki.

Baada ya kufanya uchunguzi mfupi, walisema Mhandisi Patrick Aron Mfugale tayari amekwishafariki, baada ya hapo tulianza uratibu wa kuitafuta familia ili tuijulishe kabla ya taarifa nyingine kuifikie jamii.

PIA, SOMA=> Erasto Mfugale: Kilichotokea kazini sisi hatujui
Safari ilianzia Ubungo daraja la Kijazi, kituo kikichofuata stendi ya JPM, Kituo cha tatu daraja la Mfugale, Kituo kinachofuta ni soko kuu la Ndugai Chamwino Idodomya.
 
"Katika kikao hicho majira ya saa nne, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya na ndipo Katibu Mkuu akamueleza aende akapumzike katika ofisi jirani ambayo ni ofisi yake ili kikao kiendelee".

Mtu akijisikia vibaya si hupewa huduma ya kwanza na endapo hali ikizi kudhoofu si hulazimika kupelekwa hospitali!?

Sisi ni watanzania mkuu, kuna vitu akili zetu zimedumaa kuvizingatia hususani ni hali za afya zetu...

Mathalani ni mara ngapi mimi, wewe na yule tumewahi jisikia vibaya kiafya lakini badala ya kutafuta tabibu tunaishia kwenda kulala, au kupumzika kivulini tukitaraji hali ya mwili itarejea kuwa sawa?

Kwa ukubwa wa umri wa Mfugale, maarifa ya elimu aliyokuwa nayo na hata pesa aliyokuwa nayo alipaswa awe na personal consultant wa afya ambaye bila shaka familia ndio ingekuwa ikimrushia hayo maswali kwa sasa...
 
We nae husomi.?
Alisema hajiskii vizuri lakini alikua anaweza kutembea mwenyewe ndo akaenda kujiskilizia kwanza chumba kingine..

haya hio first aid ukileta utafanya nini?.
Hata mkiahirisha kikao ndo yule anapona?.
Acha ujinga wewe kikao mlisogeza mbele kwa kuwa alisema hawezi kuja ana kazi zingine mkasogeza mbele ila siku ya kikao anaumwa na kikao kinaendelea sasa kama alikuwa sio muhimu kuwepo kwake mlisogeza kikao mbele cha nini? Mtu akisema hajisikii vizuri ghafla ni dalili mbaya ni lazima aende kupata huduma ya kwanza kwa hiyo ulitaka akianguka ndio apewe huduma. Juzi umeona mchezaji kaanguka kapona kwa sababu tu alipata huduma ya kwanza. Mimi mtu yoyote anaweza kufa hata akipata huduma ndio maana wengine wanafia mahospitalini wakitibiwa. Maelezo ya naibu waziri hayajanyoka na ndio maana family imeyasema hadharani sababu hata wao hawajui kimetokea nini. Sasa kainuka mweneyewe alienda kumuangalia nini tena ofisini? kuangalia kama kisha kufa au bado?
 
*save life....
Kwa wenye ujuzi nayo

mtu amekaa kwenye kiti anakwambia ongeza AC kwanza nijiskilizie nipoe kidogo utafanya huduma ipi ya kwanza?.
Sijui kama hapa Bongo tuna “Health and safety at work policies” . Nchi nyingine kila sehemu ya kazi ni lazima uwe na first aid responder kila shift. Ni mfanyakazi wa kawaida lakini pia wame train kuwa first aider. Hii ni course ya siku moja.
First aid inajumuhisha pia kuangalia vital signs.

Mfano huyu bosi aliposema anajisikia vibaya kitu cha kwanza ni ku check vital signs.

Wangeweza ku count pulse rate manually na respiration. Mfano:
HR - 110 per minute
Resp - ni above 24.
You know there is something is cooking. Angekipizwa hospital.
Na kama ukitumia observation kit. Unaweza ku check:
BP
Temp
BGL
Huyu inawezekana li saa lizima amesema anajisikia vibaya na solution ni AC…very sad. Life could have been saved here!
Usichukulie first aid ni CPR tu!
 
Jamani kuweni makini na hizo AC hasa ukiwa na magonjwa nyemelezi.
Kuna maofisi mengi tu watu wanajiua kimya kimya. Yaani unaingia ofisini unakuta baridi ya kwenye friji! Wapendwa! Mnajiua!
Ukiwa na AC zingatia yafuatayo:
1. Room temperature
2. Refrigerant iliyopo ndani ina madhara gani? Refrigerant nyingi huku Tz ni sumu kamili!
Kifo kikitokea kama hiki kunakuwa na nadharia nyingi sana. Nachojiuliza: hawakumfanyia post mortem kujua chanzo?
 
Sijui kama hapa Bongo tuna “Health and safety at work policies” . Nchi nyingine kila sehemu ya kazi ni lazima uwe na first aid responder kila shift. Ni mfanyakazi wa kawaida lakini pia wame train kuwa first aider. Hii ni course ya siku moja.
First aid inajumuhisha pia kuangalia vital signs.

Mfano huyu bosi aliposema anajisikia vibaya kitu cha kwanza ni ku check vital signs.

Wangeweza ku count pulse rate manually na respiration. Mfano:
HR - 110 per minute
Resp - ni above 24.
You know there is something is cooking. Angekipizwa hospital.
Na kama ukitumia observation kit. Unaweza ku check:
BP
Temp
BGL
Huyu inawezekana li saa lizima amesema anajisikia vibaya na solution ni AC…very sad. Life could have been saved here!
Usichukulie first aid ni CPR tu!
Maoni mazuri sana. Mimi niliondoka Tanzania sijui chochote kuhusu first aid lakini nchi niliyoenda nikuta mpaka mashuleni wanafundisha. Kazini ndiyo usiseme, kila baada ya miaka miwili lazima mpewe trainning na first aid kits hazikosekani. Tanzania hata watu ambao wangeweza kupona wanakufa.
 
Unajua Donald Trump alikua rais akiwa na umri gani? Pia angalia umri wa yule mama speaker wa bunge lao. Halafu uje tena na hoja ya umri.

Nadhani ni mazingira yetu na mfumo wa maisha yetu ndio shida
Mambo ya umri sidhani kama ni issue. Kuna watu mpaka miaka 80 wanaweza kufanya kazi hata kuliko mtu wa miaka 50. Marehemu hakuwa kwenye hali mbaya atleast kwa muonekano.
 
Ukifika 60 staafu acha ulafi maisha huisha na wengine wapo na wanazaliwa. Kuendelea zaidi ya hapo ni laana.
Mfugale ni mfano mbaya wa binadamu mlafi
 
Huyu mtu alikua na majukumu mengi sana wakati umri umeenda sana.
Mnafikiri wazungu waliposema watu wa staafu na miaka 55 mpaka 60 walikua wajinga?
Kuna mtu mmoja Sasa hivi mwendazake alikua anasema hadharani kwamba akiondoka yeye miradi hii itasimamiwa na nani?
Je? Sasa hivi hayupo, miradi inasimamiwa na nani?
Sasa hivi amekua mpendwa wetu lkn alipokua hai amepitiliza umri wa kustaafu hakuna aliyeweza kum face na kumuambia akacheze na wajukuu. Kwa sababu Kuna manufaa ambayo watu walipata kutoka kwa marehemu waliendelea kumsifia ili aendelee kuumia ili wapate ugali. Hata familia haikumshauri astaafu kwasababu kwa njia moja walikua wanafaidika huyu CEO akiwa kazini ilhal alikuwa anaonekana kabisa kwamba amechoka.
Hii kanuni yako nakubaliana nayo sana. Umri ukienda pumzika. Utajiepusha na mengi. Hata mzee Machache angejipunguzia majukumu ya mali na familia(asingeoa tena) tungekuwa naye hadi leo.
 
Watu wengine hapa Tanzania hawana elimu ya huduma ya kwanza. Wangeweza hata ku check heart rate(pulse) manually, and respiration!
Hivi unawezaje kuwa na mkutano kama huo bila first aid?

Hawa ndio tunategemea ni role models wa taifa, inakuwaje mtu anajisikia vibaya wanampeleka chumbani kupumzika badala ya kumwahisha hospital ama kuita Dr. kama hawana gari?

Mtu anataka kuwekwa kwenye lower temperature, below room temperature, unampunguzia halafu unamwacha!. Hivi hawa jamaa, if they can not be serious with the life of their peers, how can we expect them to be serious with national issues?

How many more decades do we need to defeat our three big enemies of development if this is the level of our role models?

Hi huzuni sana, tena sana, tena sana. Ni nini hiki ?
 
Acha ujinga wewe kikao mlisogeza mbele kwa kuwa alisema hawezi kuja ana kazi zingine mkasogeza mbele ila siku ya kikao anaumwa na kikao kinaendelea sasa kama alikuwa sio muhimu kuwepo kwake mlisogeza kikao mbele cha nini? Mtu akisema hajisikii vizuri ghafla ni dalili mbaya ni lazima aende kupata huduma ya kwanza kwa hiyo ulitaka akianguka ndio apewe huduma. Juzi umeona mchezaji kaanguka kapona kwa sababu tu alipata huduma ya kwanza. Mimi mtu yoyote anaweza kufa hata akipata huduma ndio maana wengine wanafia mahospitalini wakitibiwa. Maelezo ya naibu waziri hayajanyoka na ndio maana family imeyasema hadharani sababu hata wao hawajui kimetokea nini. Sasa kainuka mweneyewe alienda kumuangalia nini tena ofisini? kuangalia kama kisha kufa au bado?
We nae unajichangany hadi hueleweki
Na unafoka kwani mi nilikuwepo?ama mi ndo Waziri? Ama kwani Wizara ndo wamemuua?

hiyo first aid kila mtu anajua kufanya?

Tupunguze maneno na lawama
Siku zilifika Mungu kamchukua Apumzike kwa amani Baba wa Watu

Vikao vitaendelea huwezi jua wanafanyaje kazi
 
Sijui kama hapa Bongo tuna “Health and safety at work policies” . Nchi nyingine kila sehemu ya kazi ni lazima uwe na first aid responder kila shift. Ni mfanyakazi wa kawaida lakini pia wame train kuwa first aider. Hii ni course ya siku moja.
First aid inajumuhisha pia kuangalia vital signs.

Mfano huyu bosi aliposema anajisikia vibaya kitu cha kwanza ni ku check vital signs.

Wangeweza ku count pulse rate manually na respiration. Mfano:
HR - 110 per minute
Resp - ni above 24.
You know there is something is cooking. Angekipizwa hospital.
Na kama ukitumia observation kit. Unaweza ku check:
BP
Temp
BGL
Huyu inawezekana li saa lizima amesema anajisikia vibaya na solution ni AC…very sad. Life could have been saved here!
Usichukulie first aid ni CPR tu!
Hilo ndo la msingi awepo Afisa mmoja katika wale HR anaejua na kuwajibika na masuala hayo
 
We nae unajichangany hadi hueleweki
Na unafoka kwani mi nilikuwepo?ama mi ndo Waziri? Ama kwani Wizara ndo wamemuua?

hiyo first aid kila mtu anajua kufanya?

Tupunguze maneno na lawama
Siku zilifika Mungu kamchukua Apumzike kwa amani Baba wa Watu

Vikao vitaendelea huwezi jua wanafanyaje kazi
Sasa unaenda Hospital kufanya kama siku haijafika utaishi tu. Wewe unaongelea wepesi wana familia wanasema hawajui kimetokea nini haki yao kuuliza kumpa mtu huduma ya kwanza ni jambo muhimu kwa mgonjwa yoyote. Hakuna mtu analaumu mtu kufa wana familia wamehoji nini kilitokea hawajui anakuja mtu kutoa maelezo baada ya kuongea katika msiba mbele ya Rais kwanini wasingeambiwa kabla. Vikao kasema tulisogeza mbele kwa ajili yake alikuwa na majukumu mengine siku ya kikao kinaendelea yeye hayuko anajisikia vibaya. Ba uhakika hawahusiki na lolote ila hatua walizochukuwa ni dharau mtu hajisikii hovyo unasema kapumzike ofisi ile kwani alisema na usingizi sijalala mimi.
 
Maoni mazuri sana. Mimi niliondoka Tanzania sijui chochote kuhusu first aid lakini nchi niliyoenda nikuta mpaka mashuleni wanafundisha. Kazini ndiyo usiseme, kila baada ya miaka miwili lazima mpewe trainning na first aid kits hazikosekani. Tanzania hata watu ambao wangeweza kupona wanakufa.
Miaka miwili ni mingi sana. Kwa kampuni inayojali inatakiwa iwe after 6 months.
 
Back
Top Bottom