Mkuu Ngongo,
Ni kweli tena Lusinde unajua kabla ya hapo alikuwa Balozi Kenya, na ana miradi yake kule basi yy alikuwa na gari na dereva na alikuwa anapiga misele kama anavyotaka, na posho na madolari kibao. Sasa nadhani last time alikuwa Ret. mjeshi mmoja na najua uchaguzi uliopita walikomba pesa nyingi sana. Huyu mjeshi nae aliingia kwa mbwmbwe nyingi lkn alipotulizwa na kuonjeshwa utamu akatulia tuliii. Meghji enzi zake kwa kujua utamu kule, akamuweka mmewe kama moja ya members ...!! Only in bongo..
Huyu bitozi ngosha aliyeingizwa mjini akatumiwa kuuza twiga then wakamtosa (yy alipewa posho kidogo ya bei za ngiri na nyegere tuuu) yy alikuwa anakusanya fweza ili kuteua watu. Sasa hapo hujaangalia posho za vikao wanalipana kiasi gani- last time ilikuwa 1M per meeting (wakichacha au ikikaribia sikukuu kama mwisho wa mwaka kunakuwa na extra-ordinary kama 2, 3 so 3M) hapo bado wanalipiwa malazi, chakula na za nyumba ndogo !! Kuna milafi inachukua posho kwenda nje eti kutangaza usanii (utalii) so kikao kikipangwa huku hawapo bado inadai posho zao na wanapewa..
Sitashangaa huyu mwenyekiti wa kamati ya bunge sasa ya mazingira kama hawatamwekea zengwe na kumpiga chini, maana anajua undani wa huko (yy na Ndugai walikuwa huko pia) na ndiyo maana anajua namna ya kuwashika pabaya (kabla ya kuwa naibu spika Ndugai ndiye alikuwa mwenyekiti).
Nilishasema siku nyingi, bodi nyingi ni ulaji tuu, mtu hajawahi hata kuona mijusi au kujua mende wanakojoaje sasa leo hii unampa ukuu wa taasisi ya utafiti wa wanyamapori ili afanye nn na maamuzi gani ? Bodi ziwe na members wachache, wataalam wa fani husika- lawyers, mchumi, na rest wahusika wa fani hiyo basi, na hakuna kujaza retired officers kama njia za kuwaongezea mapato. Ona huyu mjeshi mfunga buti Mboma mambo anayofanya !!
Mkuu Mafuluto ni kweli NCAA fedha zinachotwa CCM wamekuwa wakihakikisha wanaweka watu wao kwaajili ya manufaa ya chama chao na wakati huo huo wafanyakazi wana take advantage ya kuchota fedha kwakuwa wanajua siri kibao.Kabla ya Pius Msekwa alikuwepo Job Lusinde TANAPA huyu ni mdhamini wa CCM mpaka leo Sijui mwenyekiti wa bodi siku hizi ni nani jaribu kutafiti utakuta ni wale wale watu wa system.