Waziri anapokataa kuwa hakuna mgawo wakti ndo unapamba moto!

Papa D

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
753
182
Wana jamvi:-
waziri wa nishati amesisitiza kuwa nchi haina mgawo wa umeme na hapatakuwa na mgawo katika tanzania yetu! Je, hili tatizo la kukatika umeme kila siku katika muda ule ule kwa muda wa mwezi sasa tulieze kwa kutumia lugha gani zaidi ya mgawo? Hii habari ya umeme kuwa na flactuation kubwa tulieleze kwa lugha ipi zaidi ya matokeo ya mgawo?
 
Watendaji Tanesco wanamhujumu waziri. Tanzania kama unavyojua ni wezi kuanzia juu mpaka kwa mwenyekiti wa kijiji
 
Wacha akane anajua fika sie watanzania mbu-mbu-mbu hata kukiwa na mgao mwaka mzima, ikifika 2015 kura zote CCM. Tatizo nini????
wanatuchezea kwa Umbu-mbu-mbu wetu
 
Anajiamini kwamba anaongoza mazezeta ambao hawana ubavu wa kuhoji wala kuchukua hatua dhidi ya ubabaishaji wa serikali. Yaani Tanzania inaongozwa na makomedians fulani ambao wao wenyewe wamekata tamaa kuliko hata wanaowaongoza. Bora hata tungewapa akina masanja na joti kuongoza nchi wangekuwa productive kuliko Kikwete na kundi lake.
 
Hilo la watendaji wanamuhujumu ni siasa uchwala za watawala:- hebu jiulize hili kwamba 65% ya umeme wa nchi hii unategemea mabwawa; mabwawa ya nchi hii yanategemea mvua; miaka ya karibuni mvua imekuwa ya kusuasua that means:- mvua ya kusuasua=upungufu wa maji katika mabwawa=upungufu wa umeme= mgawo wa umeme. je, nani anayefanya hujuma kati ya watendaji wa tanesco na mleta mvua?
Je, unajaribu kutueleza kuwa Mungu anaifanyia hujma serikali ya Tanzania?
Watendaji Tanesco wanamhujumu waziri. Tanzania kama unavyojua ni wezi kuanzia juu mpaka kwa mwenyekiti wa kijiji
 
Even here at Moro the electricity is fluctuating, you may find three days within a week the electricity fluctuate, that is come and go and it takes one to two hours to be stable and yet the responsible minister is saying that there is no any problem regarding the electricity shortage So if there is no any problem what causes such fluctuation to occur and he hasn't said anything so far regarding such situation
 
Hebu acheni kuwasaidia mafisadi wa Tanesco!!! Acha kabisa kufanya suala hili kisiasa. Usijaribu kuonyesha kitu cha wazi kikawa kama ni giza.

Yaani hukumbuki maana ya mgao? Mgao wa 2004 unaukumbuka? Hayo masaa 12 ya kutokuwa na umeme. Naona wengi wetu tunakuwa na kumbukumbu fupi.
 
Power corrupt, absolute power corrupts absolutely. Huyo msameheni kwani anaishi kwenye ulimwengu wa mawenge. Amekuwanywa sana kwenye kikombe cha madaraka hadi kalewa ukiachia mbali kula sana kwenye sinia la ufisadi hadi akavimbiwa hadi ubongo. Ipo siku atauona ukweli.
 
moro nzima jana hakuna umeme,leo kidogo pouwah,cjui kesho........napita tu wakuu.....idd njema
 
hapa hakuna mgawo, je wenzetu ambao hata umeme hawana wasemeje
Huwa sielewi umeme unapokatika na mimi nimeshanunua umeme wangu na ninao kwenye luku.
Wanasheria msaada jinsi ya kuwadai tanesco kushindwa kuniridhisha kwa huduma niliyoilipia tayari.
 
Hawa mawaziri wanatusumbua kichwa, ngoja ifike 2015 tuwaanzie kama ya akina Berlusconi huko Italiano aliyekula 4 years in jail kwa kudodge tax.
 
naomba niwatarifu pale mtera wanafanya matengenezo makubwa ya mitambo next week wanamaliza na wakimaliliza tu umeme utakuwa wa mgao hasa mikoa ya dodoma singida manyara na arusha baadhi mana hali ya maji ya c nzuri bwawa linakauka kwa kasi ya ajabu.hivyo hli la waziri kujiapiza hakuna mgao ni porojo
 
kwa kweli toka achukue madaraka huku kwetu umeme haukatiki kabisa....sema kama watendaji wa chini wanakata yeye anaweza asiwe na habari inabidi muwe mnatoa habari kwenye vyombo vya habari au kwenda ofsini kwake kulalamika ili na yeye aweze kufuatilia...kumbukeni yeye ni mtu mmoja tu hawezi kua anajua kila pembe ya hii nchi kama kuna mgao au la
 
Even here at Moro the electricity is fluctuating, you may find three days within a week the electricity fluctuate, that is come and go and it takes one to two hours to be stable and yet the responsible minister is saying that there is no any problem regarding the electricity shortage So if there is no any problem what causes such fluctuation to occur and he hasn't said anything so far regarding such situation

Sio lazima uandike Kingereza kama hukiwezi.Kingereza na Kiswahili zote ni lugha tu.
 
Kuna mambo mengi yanayofukuta chini kwa chini Nishati na Madini. Sipuuzi uwezekano wa hujuma upande wa TANESCO. Lakini mgao ni mgao, na upo. Sasa Waziri akikana anatuandaa tufikiri kuwa hana nia wala uwezo kushughulikia tatizo la mgao, kwa vile yeye halioni.
 
kwa kweli toka achukue madaraka huku kwetu umeme haukatiki kabisa....sema kama watendaji wa chini wanakata yeye anaweza asiwe na habari inabidi muwe mnatoa habari kwenye vyombo vya habari au kwenda ofsini kwake kulalamika ili na yeye aweze kufuatilia...kumbukeni yeye ni mtu mmoja tu hawezi kua anajua kila pembe ya hii nchi kama kuna mgao au la
Sasa nimeamini!wewe ni mtetezi wa matatizo!kila tatizo linaloonekana wazi wewe huwa mstari wa mbele kulitetea,hujawahi kuleta alternative solution,zaidi ya kuleta porojo zisizo na maana,maji hakuna=umeme hakuna wa kutosha=mgao wa umeme,,waziri anadai hakuna mgao,wewe unasema hakuna mgao huku upo gizani na luku umelipa!!!kinachogombewa si upungufu/ukosefu wa umeme,bali ukweli kuhusiana na tatizo lenyewe,wewe una divert tatizo kwa wahanga wa tatizo,eti tutoe taarifa!!mbona luku ikiisha hatuambiwi tutoe taarifa ili tukatiwe umeme?in short wewe ni Janga jingine.
 
Even here at Moro the electricity is fluctuating, you may find three days within a week the electricity fluctuate, that is come and go and it takes one to two hours to be stable and yet the responsible minister is saying that there is no any problem regarding the electricity shortage So if there is no any problem what causes such fluctuation to occur and he hasn't said anything so far regarding such situation

Sio lazima uandike Kingereza kama hukiwezi.Kingereza na Kiswahili zote ni lugha tu.

Kabisa kabisa hicho ni kiswahili ila ktk maneno ya kiingereza.
 
Back
Top Bottom