Wazee waitabiria kifo CCM: Anguko la CCM laja?

Mimi nimekimbia kejeli kwenye jukwaa la siasa, unataka nikimbie na MMU?
 
Kuna mzee hapa moro ametabiri kabisa. Nilishangaa sana. Aliuliza sijui hawa jamaa (CDM) sijui walikuwa wapi. wangeshachukua nchi zamani tu. Ni mzee wa miaka kama 90 hivi.
 
Amezeeka mwili, lakini brain yake bomba. Hao ulaya ndiyo humalizia PhD zao. Ana maono ya sasa hivi. Big up Babu.
 
Huwa sipendi siasa lakini katika hili yawezekana CCM isianguke bali kubadili mwelekeo (CCM may not fall but will change the route forward).This is always happens to most political parties in Africa where by leaders within the parties blaming others for safe of next by-election so as to save the part in power,although the risk may be to change the coluor/logs/nembo but still leaders are same.The fall of CCM may resemble with the swahili statemenT that "PORI JIPYA LAKINI NYANI NI WALE-WALE",of course we can change the Part but still we can't change the system.
 
Those who are blamming the part the are two possiblity
1.wivu tu sababu wenzao wanafaidi kwa sasa wakati wao enzi zile hawakufaidi.
2.wanajaribu kutafuta njia gani ya kuweza kukinusulu chama chao kupitia mlango wa uani.
 
Wazee wasitabiri,wachukuwe hatua.Otherwise ni usanii tu,maneno matupu hayavunji mfupa.
 
Mkuu LG,

Huitaji utabiri wa wazee wa CCM kujua CCM inaelekea wapi akili za kawaida kabisa zinatosha kubaiani chama kikongwe bara Afrika kina karibia kujizika chenyewe kama kambare anapobaiani msimu wa kiangazi umekaribia.

Ukitazama kampeni za CCM kuanzia Igunga na Arumeru unabaini jambo moja muhimu sana CCM imeacha misingi mikuu ya kuanzishwa kwake [Chama cha wakulima na wafanyakazi] CCM imegeuka kimekuwa chama cha matajiri na wezi wa rasilimali za taifa.CCM imeacha msingi wake mkuu wa kuwatetea wanyonge,imeacha kulinda rasilimali za taifa,inakumbatia wezi,sera zake hazitekelezwi,rushwa inapingwa majukwaani lakini nyuma ya pazia inapaliliwa,inawekewa mbolea na kuvunwa kwa ustadi mkubwa.

Kwakuwa CCM haina sera na hili limejitokeza katika chaguzi za Igunga Hijjab ikachukua nafasi kubwa badala ya kuufahamisha umma wa Igunga nchi inakwenda wapi,mafanikio yaliyofikiwa na changamoto zake,Arumeru CCM imekujua na sera za washili hawamtaki mgombea wa chama cha upinzani hawana kitu cha kuwaambia wapiga kura wa Arumeru wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa ardhi kwakuwa wanajua wanahusika kwa asilimia zote kuiuza ardhi kwa wawekezaji uchwara na kuwaacha wananchi bila ardhi.

Hii si ile CCM ya Nyerere iliyokuwa ikiwasemea wanyonge,wakulima na wafanyakazi hii ni CCM ya Kikwete,Mkapa na Mwinyi inawasemea wawekezaji wanaopora madini yetu,wanaopora ardhi yetu,wanaopora ajira zetu.CCM ya leo inazalisha ajira kwa kuongeza idadi ya mikoa na wilaya haina habari na viwanda !.Hii ni CCM ya washili na Hijabu,hii ni CCM ya Wasira na genge la wahuni hawana uchungu na umasikini wa watanzania,hawawezi kutueleza baada ya miaka 50 ya uhuru wamefanikiwa kupunguza umasikini vijijini kwa asilimia ngapi !.Rwanda ya Kagame baada ya mapigano ya muda mrefu inapiga hatua kubwa utashangaa haina rasilimali nyingi ukilingalisha na Tanzania.


Mkuu Ngongo, hii post yako ina vina hai haitapitwa na muda. Hatuhitaji wazee kutuambia CCM imepoteza dira na uhalali. Kwamba CCM wanafanya siasa za fitna na ufisadi, siyo sera na uadilifu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom