Wazee waitabiria kifo CCM: Anguko la CCM laja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee waitabiria kifo CCM: Anguko la CCM laja?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lole Gwakisa, Mar 26, 2012.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Wazee maarufu ndani ya Chama cha Mapinduzi, Dr Hassy Kitine,Mzee Ibrahim Kaduma na Mzee Joseph Butiku wametoa ya mwaka walipokuwa wakihojiwa katika luninga Channel 10, jumamosi.
  Habari hii imejirudia katika gazeti la Mwananchi leo(Machi ,26, 2012) ikisema:

  "Na Elias Msuya,

  Makada watatu wakongwe wa Chama cha Mapinduzi( CCM), Ibrahim Kaduma,Dk Hassy Kitine na Joseph Butiku wameibuka na kukutabiria anguko chama hicho tawala kwa kile walichosema, kwenda kinyume na misingi ya kuasisiwa kwake.

  Kauili za makada hao maarufu, zinakuja kipindi ambacho upepo wa kisiasa umekuwa ukivuma vibaya ndani ya chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika, kutokana na vita ya makundi kati ya watuhumiwa wa ufisadi na wale wanaojipambanua kwamba ni wazalendo na wapinga."


  Maoni Yangu:
  Asiyesikia la mkuu huvunjika guu!
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Msema ukweli ni kipenzi cha Mungu.
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Subirini Nape na Mkama waanze kutoa mapovu mdomoni wakisema wameongea nje ya vikao halali vya chama...
   
 4. K

  KAMANDA HANGA Senior Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao wazee wangekuwa watabiri wangeyanena hayo mapema sio wakati huu. Hapa wameona hali halisi ambayo haihitaji hata elimu ya kayumba school kuelewa anguko la ccm. Hakuna jipya walo liona ni mlolongo tu wa mambo, matukio, kasoro, makundi, ujinga, owongo, wizi, giriba nk ndani ya ccm na ukomavu wa upinzani hasa chadema.
   
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Nitashangaa sana kama haitamfia jakaya mkononi.
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Lakini mkuu hawa wazee are on record kwa kukumea ufisadi na mafisadi wa waziwazi ndani ya chama tawala.Hili zigo la ufisadi uliasisiwa na kundi la wanamtandao, kundi ambalo hadi leo linatamba serikalini na kwenye chama.
   
 7. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Subiri uone watakavyo chafuliwa hawa watu.
   
 8. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,909
  Likes Received: 2,336
  Trophy Points: 280
  Siku hizi kuna sera inaitwa FITNA ndani ya siasa za bongo, hili nina uhakika litafanyika.

   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu LG,

  Huitaji utabiri wa wazee wa CCM kujua CCM inaelekea wapi akili za kawaida kabisa zinatosha kubaiani chama kikongwe bara Afrika kina karibia kujizika chenyewe kama kambare anapobaiani msimu wa kiangazi umekaribia.

  Ukitazama kampeni za CCM kuanzia Igunga na Arumeru unabaini jambo moja muhimu sana CCM imeacha misingi mikuu ya kuanzishwa kwake [Chama cha wakulima na wafanyakazi] CCM imegeuka kimekuwa chama cha matajiri na wezi wa rasilimali za taifa.CCM imeacha msingi wake mkuu wa kuwatetea wanyonge,imeacha kulinda rasilimali za taifa,inakumbatia wezi,sera zake hazitekelezwi,rushwa inapingwa majukwaani lakini nyuma ya pazia inapaliliwa,inawekewa mbolea na kuvunwa kwa ustadi mkubwa.

  Kwakuwa CCM haina sera na hili limejitokeza katika chaguzi za Igunga Hijjab ikachukua nafasi kubwa badala ya kuufahamisha umma wa Igunga nchi inakwenda wapi,mafanikio yaliyofikiwa na changamoto zake,Arumeru CCM imekujua na sera za washili hawamtaki mgombea wa chama cha upinzani hawana kitu cha kuwaambia wapiga kura wa Arumeru wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa ardhi kwakuwa wanajua wanahusika kwa asilimia zote kuiuza ardhi kwa wawekezaji uchwara na kuwaacha wananchi bila ardhi.

  Hii si ile CCM ya Nyerere iliyokuwa ikiwasemea wanyonge,wakulima na wafanyakazi hii ni CCM ya Kikwete,Mkapa na Mwinyi inawasemea wawekezaji wanaopora madini yetu,wanaopora ardhi yetu,wanaopora ajira zetu.CCM ya leo inazalisha ajira kwa kuongeza idadi ya mikoa na wilaya haina habari na viwanda !.Hii ni CCM ya washili na Hijabu,hii ni CCM ya Wasira na genge la wahuni hawana uchungu na umasikini wa watanzania,hawawezi kutueleza baada ya miaka 50 ya uhuru wamefanikiwa kupunguza umasikini vijijini kwa asilimia ngapi !.Rwanda ya Kagame baada ya mapigano ya muda mrefu inapiga hatua kubwa utashangaa haina rasilimali nyingi ukilingalisha na Tanzania.
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Utabiri hauna nafasi tena karne hii
   
 11. K

  KAMANDA HANGA Senior Member

  #11
  Mar 26, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwezi kusafisha tope kwenye bwawa ukiwa ndani ya bwawa. Hawa wazee kama sio wanafiki, wazandiki, wafitini,. Waoga, wambea na wasaliti, wangeamua maamuzi mazito ya kusimamia maadili, malengo, katiba na kanuni za ccm ambazo ni nzuri sana. Hawa wazee baadhi wanatumia uozo wa ccm kulinda maslai na utajiri wao walopatia ndani ya ccm. Ukitoa mzee Butiku nani asiyejua utajiri na ukaribu wa hao walo baki na rais alo asisi ufisadi ndg Mkapa? Ndg yangu hakuna jipya wanajilinda tu na wakienda kwa jk wanamsifia tu. Nini sasa?
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe Mkuu kwa hii observation ambayo ni critical.
  Lakini, mie najiuliza kila siku, hivi CCM yenyewe haijioni kuwa inachungulia kaburi?
  Maana imeanza kukosa sifa za kuwa chama kinachomilikiwa na wananchi wenyewe na kwa ajili yao.
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mkuu,
  Hata 'MNYAMA aka mdudu' huwa hajui kuwa anakaangwa kwa kutumia mafuta yake mwenyewe!...
   
 14. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbona hawaondoki huko ccm,wanasubiriko nini?
   
 15. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu sikubaliani sifa hizo negative kwa wazee hawa, uzee ni dawa!
  Hawa wazee si mafisadi kwa hiyo hawana cha kupoteza kwa kusema hivyo, na ninavyo wafahamu wana uchungu na nchi hii.
  Vile vile kama unaijua vyema CCM , ni zaidi ya chama cha siasa, kwa hiyo kwa hawa wazee wazito si rahisi kusema umeondoka ndani ya chama na ukawa salama baada ya kukitumikia muda mrefu.
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu LG,

  Mkuu unategemea NEC ya CCM ya akina Asha Baraka & Co ina maono ya mbali ?. WaNEC aina ya Asha Baraka hawajui umuhimu wa Reli,hawajui mazao ya kilimo yanaongezwa thamani na viwanda,hawajui bila ujenzi wa viwanda tatizo la ajira kwa vijana litaongezeka maradufu,hawajui maendeleo ya nchi lazima yatawanywe nchi nzima na si kurundika maendeleo Dar pekee yake matokeo yake ongezeko la watu katika jiji la Dar halitaendeana na miundo mbinu iliyoko maji,mabaraba,nyumba,umeme na nk.Wajumbe wa NEC taifa ambao kazi yao kubwa ni pamoja na kuandaa sera za chama chao wako busy kwaajili ya fitina za uchaguzi wa mwaka 2015.


   
 17. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  But can cost them! Siku zote ukisema kweli ndani ya mfumo wa Serikali zetu zilizojaa unafiki pamoja na vyama uchwara kama hao wanaofukuzana sasa hivi basi wewe ni adui namba moja kwani wao hawafikirii hata siku moja kwamba wanaweza kukosea na sio watu wakurekebishwa bali kikubwa wananachoangalia ni ulaji wao, Angalia kina Butiku wameandika barua hawajajibiwa mpaka leo, Warioba kasema wee wao wameziba masikio, Tume nyingi zimeshauri wao wamevaa miwani za mbao:cool2:

  SUBIRI KESHO UONE WAHUSIKA WATAKAVYOJIBU KAMA VILE WANAWAJIBU CHEKECHEA

   
 18. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hakuna utabiri hapo, inaonekana kabisa kuwa ccm imekufa!
   
 19. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hawa wazee naona miili yao inawasha kwa kutamani matusi. Ngoja wenye chama chao waje wawaporomoshee mitusi ya nguoni hadi wakome.
   
 20. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mazishi ya CCM ni lini na wapi?
   
Loading...