Wazee waitabiria kifo CCM: Anguko la CCM laja?

Nakubaliana na wewe Mkuu kwa hii observation ambayo ni critical.
Lakini, mie najiuliza kila siku, hivi CCM yenyewe haijioni kuwa inachungulia kaburi?
Maana imeanza kukosa sifa za kuwa chama kinachomilikiwa na wananchi wenyewe na kwa ajili yao.


Mkuu,
Siku zote kichaa akitembea hata akiwa uchi yeye huona yupo sawa tu, na huwashangaa wote wanaomshangaa.
Usishangae pro ccm wanapinga kwa sauti zao zoote!
Vijisenti vimewapofusha macho kabisa.
 
Nakubaliana na wewe Mkuu kwa hii observation ambayo ni critical.
Lakini, mie najiuliza kila siku, hivi CCM yenyewe haijioni kuwa inachungulia kaburi?
Maana imeanza kukosa sifa za kuwa chama kinachomilikiwa na wananchi wenyewe na kwa ajili yao.


Nadhani hata kama hakitakufa kikishindwa 2015 wakifute kabisa kama cha kule zambia maana ni hatari kubaki hata na mzoga wake.
 
Mkuu LG,

Mkuu unategemea NEC ya CCM ya akina Asha Baraka & Co ina maono ya mbali ?. WaNEC aina ya Asha Baraka hawajui umuhimu wa Reli,hawajui mazao ya kilimo yanaongezwa thamani na viwanda,hawajui bila ujenzi wa viwanda tatizo la ajira kwa vijana litaongezeka maradufu,hawajui maendeleo ya nchi lazima yatawanywe nchi nzima na si kurundika maendeleo Dar pekee yake matokeo yake ongezeko la watu katika jiji la Dar halitaendeana na miundo mbinu iliyoko maji,mabaraba,nyumba,umeme na nk.Wajumbe wa NEC taifa ambao kazi yao kubwa ni pamoja na kuandaa sera za chama chao wako busy kwaajili ya fitina za uchaguzi wa mwaka 2015.


Kweli kabisa Mkuu.
Ukiwa na wajumbe legelege kwa ajili ya utungaji wa sera za kuwapeleka wananchi katika maendeleo yao, basi maendeleo hayo ni ndoto.
Kwa mfano huo wa Asha Baraka kuwa mjumbae wa NEC basi ndio tumejiwekea kipaumbele hafifu sana katika upangaji wa maendeleo yetu.
Kwa sasa inaelekea chama kimekuwa gulio la wafanya biashara na vigogo wenye maslahi binafsi.
CCM isipojirekebisha katika mapungufu haya,basi itayeyuka kama makapuni ya biashara kama RTC.
 
Huu sio utabiri, bali ni tahadhari. Utabiri hutolewa kwa hali au kitu kisichojulikana/fahamika. Ina maana kwamba kama CCM kitaweka mambo sawa hilo anguko halitakuwepo na kwa maana hiyo huo uatabiri hautatimia.
 
CCM na CDM sasa hivi wanafanana. CCM halisi imeshakufa kama ambavyo CDM halisi ilivyokufa.
 
bila shaka CCM ni miongoni mwa vyama vya muda mrefu vya afrika ambavyo bado vipo madarakani. ni vyema vyama vingine navyo vipewe nch tuone itakuwaje maana kwa sasa hali ni mbaya sana kimaisha kwa ujumla
 
huo si utabiri ni hali halisi. Kaburi imeishachimbwa, na jeneza tayari ccm imo ndani kilichobaki kuelekea makaburini
 
Hasy Kitine alimtibu mke wake Canada kwa milioni 60 matibabu hewa fedha za serikali/wananchi.........akajiuzulu kuwa waziri wa utawala bora awamu ya Mkapa leo ni kamanda wa kupampana na ufisadi.

sijawahi kusikia akijutia kitendo hiki au hata kuwaomba radhi watanzania kwa kufisadi fedha yetu

Kuishi kwingi ni kuona mengi.
 
Mie si shabiki wa siasa, lakini yaani kwa waliyosema Kitine, Butiku na Kaduma juu ya CCM, Chadema wala haihitaji kufanya kampeni tena; wanaweza ku wakachapicha makala nyingi za hii habari kama ilivyo katika mwananchi na kuigawa kama kampeni ya uchaguzi wowote.

Dk Kitine,Butiku wakitabiria kifo CCM
 
Mkuu LG,

Mkuu unategemea NEC ya CCM ya akina Asha Baraka & Co ina maono ya mbali ?. WaNEC aina ya Asha Baraka hawajui umuhimu wa Reli,hawajui mazao ya kilimo yanaongezwa thamani na viwanda,hawajui bila ujenzi wa viwanda tatizo la ajira kwa vijana litaongezeka maradufu,hawajui maendeleo ya nchi lazima yatawanywe nchi nzima na si kurundika maendeleo Dar pekee yake matokeo yake ongezeko la watu katika jiji la Dar halitaendeana na miundo mbinu iliyoko maji,mabaraba,nyumba,umeme na nk.Wajumbe wa NEC taifa ambao kazi yao kubwa ni pamoja na kuandaa sera za chama chao wako busy kwaajili ya fitina za uchaguzi wa mwaka 2015.

Kwani Khadija Omar Kopa, Mama yake Hayati, Ustaadh, Omar Kopa, si mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama chetu kitukufu? Mbona hamumtaji! Au mnataka mkipunguzie heshima Chama nyie Chadema tumeshawazoea.
 
Naomba watu wote hasa waliopo kwenye kampeni Arumeru Mashariki watumie maneno ya wazee wakongwe akina Dr kitine, mzee Kaduma na mzee Butiku Waliyoyasema ktk kipindi cha Je tutafika kilichorushwa hewani na channel 10kuendelea kuipa nguvu CDM na kuizika CCM. Poa hao viongozi mkapa na JK nawaomba wajibu mapigo hayo ya meremete, EPA kn. Kama ambavyo haonwazee wamesemaje anaebisha hakuna rushwa CCM ajitokeze.
 

Ukitazama kampeni za CCM kuanzia Igunga na Arumeru unabaini jambo moja muhimu sana CCM imeacha misingi mikuu ya kuanzishwa kwake [Chama cha wakulima na wafanyakazi] CCM imegeuka kimekuwa chama cha matajiri na wezi wa rasilimali za taifa.CCM imeacha msingi wake mkuu wa kuwatetea wanyonge,imeacha kulinda rasilimali za taifa,inakumbatia wezi,sera zake hazitekelezwi,rushwa inapingwa majukwaani lakini nyuma ya pazia inapaliliwa,inawekewa mbolea na kuvunwa kwa ustadi mkubwa.


Mimi sijaona viongozi wa CCM wakipiga vita rushwa amabyo ianzidi kuididimiza Tanzania. Rais Kikwete amepata kigugumizi cha ajabu sana kwenye kupiga vita rushwa na ufisadi. Akizungumzia rushwa basi anazungumzia rushwa ndani ya CCM tu wakati anajua maofisi yote ya serikali na taasisi zake zimejaa rushwa. Nani asiyejua kuwa ukitaka hati miliki ya kiwanja pale ardhi unahitaji siyo chini ya milioni mbili? Sijui kwa nini Rais Kikwete anashindwa kabisa kutamka kuwa rushwa ni mbaya wakati anaona nchi ikididimia kwa rushwa na ufisadi. Lakini naamini ipo siku mambo yote haya yatakwisha na mafisadi watapewa hukumu inayostahili.
 
Monday, 26 March 2012 12:53
000001dkkitibe.jpg
Dk Hassy Kitine


YUMO PIA KADUMA, WASEMA WANAMTANDAO NI CHANZO CHA UFISADI

Elias Msuya

MAKADA watatu wakongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ibrahim Kaduma, Dk Hassy Kitine na Joseph Butiku, wameibuka na kukitabiri anguko chama hicho tawala kwa kile walichosema, kwenda kinyume na misingi ya kuasisiwa kwake.Kauli za makada hao maarufu, zinakuja kipindi ambacho upepo wa kisiasa umekuwa ukivuma vibaya ndani ya chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika, kutokana na vita ya makundi kati ya watuhumiwa wa ufisadi na wale wanaojipambanua kwamba ni wazalendo na wapinga ufisadi.

Wakizungumza juzi usiku katika kipindi cha "Je, tutafika?" Kilichorushwa na kituo cha luninga cha Channel ten, makada hao walitoa kauli hizo nzito huku wakishambulia kundi la wanamtandao ndani ya chama hicho, vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi na vitendo vya ufisadi vinavyolitikisa taifa.

Kaduma
Kaduma ambaye aliwahi kuwa Waziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Mwalimu Julius Nyerere, alisema hali ndani ya CCM sasa ni mbaya na imefika hapo kwa sababu ya kuacha misingi ya TANU iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere.

"Kwa hali ilivyo, CCM kinaweza kusambaratika wakati wowote. Sisi tuliingia kwenye TANU kutokana na misingi ambayo Mwalimu Nyerere aliiweka," alionya Kaduma.

Kaduma aliitaja misingi hiyo kuwa ni pamoja na imani kuwa binadamu wote ni ndugu, kuwatumikia watu kwa moyo wote, kujitolea nafsi kuondoa umasikini ujinga na maradhi, rushwa ni adui wa haki hivyo ni kosa kutoa au kupokea rushwa, kutotumia cheo cha umma kwa maslahi binafsi, kusema kweli daima na kuacha fitina, kujielimisha kadiri ya uwezo na kutumia elimu hiyo kwa manufaa ya umma.

Alisisitiza, "Mwalimu hakuwa akiongea nadharia, ndiyo maana mwaka 1955 aliacha kazi aliyokuwa nayo ya ualimu iliyokuwa na mshahara mzuri na kwenda kuimarisha chama cha TANU ilikuwa ni ku-risk (kujiweka kwenye hatari).''

Dk Kitine
Dk Kitine akizungumzia barua zilizowahi kuandikwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku kwa wenyeviti wa CCM (Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete), na kutojibiwa na viongozi hao, alisema hata angekuwa yeye asingezijibu kwa sababu ndiyo mfumo wa chama hicho kutotatua na kuficha matatizo.

"Barua ya Butiku kwenda kwa Mwenyekiti wa zamani na wa sasa haikujibiwa..., hata ningekuwa mimi nimeandikiwa barua na mambo ninayofanya ni wazi, nisingeijibu. Mimi siwalaumu. Hiyo ni moja ya matatizo na utamaduni wa chama tawala kutokuwa na utamaduni wa kutatua matatizo," alisema Dk Kitine.

Akizungumzia chanzo cha kuporomoka kwa maadili ndani ya CCM, Dk Kitine ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, alisema yalitokana na kuanzishwa kwa makundi na mitandao ya kusaka madaraka kwenye chama.

"Mitandao na makundi ndani ya CCM, hakikuandikishwa mahali popote. Mtandao ulianzishwa mwaka 1995 na ulikuwa wa vijana. Mwaka huo mtandao huo ulifanya mgomo mbele ya Mwenyekiti Ali Hassan Mwinyi na mbele ya Mwalimu Nyerere wakati huo tunatafuta viongozi," alisema Dk Kitine na kuongeza:

"Wakati Mzee Mwinyi anatuongoza kama mwenyekiti na amekuja kutueleza maazimio ya Kamati Kuu kwamba kwanini baadhi ya wagombea hawakuwa na sifa, wanamtandao wakasema jambo hilo halikubaliki."

Aliongeza kwamba, mtandao huo ndiyo umekuwa chanzo cha ufisadi ndani ya chama na kufafanua; "Kundi hilo ndilo sasa linaendesha rushwa, linafanya wanachama wa CCM kuwa hawana maana, linakusanya kadi. Kama wanabisha waje kwenye kikao kama hiki wajieleze."

Dk Kitine alitaja kashfa za ufisadi zilizovuma kuwa ni pamoja na Deep Green, Kagoda, Meremeta, EPA na kubainisha kwamba zote zina mkono wa kundi hilo la mtandao.

"Lakini yote yanatokana na kuficha matatizo, kwa mfano unapowakataza watu kujadili suala la Muungano, unaficha nini? Sasa haya ya kuficha pia masuala ya Kagoda na mengineyo, ipo siku watu watataka majibu yao tu hata miaka 100 ijayo. Matokeo yake watakichukia chama," alisema.

Kauli ya Butiku
Katika mjadala huo, Butiku ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, alisema CCM kimebadilika kutoka kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi na kuwa chama cha wafanyabiashara na maslahi binafsi.

"Mnapofanya kazi katika Serikali au chama, wajibu wenu siyo kukiua chama mlichokianzisha kama ni chama chochote au CCM kinachojiita kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi. Kwa bahati mbaya sana wafanyabiashara wengi waliojiingiza katika Chama Cha Mapinduzi, wamegeuka, kazi yao na madhumuni ndiyo yamekuwa malengo mbadala ya chama," alisema Butiku na kuongeza:

"Mimi naamini biashara ni kazi, lakini kama unachukua malengo ya biashara na kuyafanya kuwa malengo mbadala ya Chama Cha Mapinduzi, chama hicho bado kipo?," Alihoji.

Butiku ambaye aliwahi kuwaandikia barua Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkapa na Mwenyekiti wa sasa Rais Kikwete akitoa angalizo kuhusu mweleko wa chama hicho, alisema hali ya sasa chama ni mbaya.

"Kwa hiyo wakati ule nilisema chama kimeanza safari ya kifo. Leo ukitazama, ukisikiliza viongozi wanavyosema, ukisiliza matendo yao, uwepo wao wote ni wa kibiashara na si kuimarisha chama hicho, ni kuimarisha malengo yao ya kibiashara na kibinafsi," alisema Butiku.

Aliongeza kuwa chama hicho kimepoteza maadili kiasi kwamba imekuwa kawaida kwa viongozi kununua kura na kwamba siku hizi, uongozi wa chama unanunuliwa.

"Nani anabisha kwamba CCM hatununui uongozi? CCM viongozi wote wa ngazi mbalimbali, mmoja mmoja anieleze kama siyo kweli kwamba CCM kimekuwa chama cha kukumbatia rushwa na kununua uongozi?," Alihoji na kuongeza:,

"Chama kimefikia wakati mtu anaweza kununua kadi 1,000 na kuweka kwenye mkoba wake wakati ndugu Kitine anazo 200, wewe ndiyo mshindi. Mkisha vunja maadili kwa kiwango hicho, bado mpo?"

Hata hivyo, alisema Katiba ya CCM bado inajieleza vizuri na kwamba hiyo ndiyo inamfanya aendelee kuwa mwanachama wa chama hicho japo viongozi wake hawaifuati.

"Katiba inasema chama hiki ni cha wakulima na wafanyakazi, waliokubali madhumuni hayo. Kama hatutaki basi tukibadili, lakini hatuwezi kukibadili kinyemela. Siku hizi naambiwa ukisikika unakikosoa chama, sauti hizo zimekuwa za watu wa Nyerere, hivi katika nchi hii nani asiyekuwa wa Nyerere? Alihoji Butiku.

CCM imetimiza miaka 35 tangu kuasisiwa kwake kwa kuunganishwa vyama vya ASP na TANU mnamo Februari 5, mwaka 1977 lakini, chama hicho katika siku za karibuni kimeshuhudia ukosoaji mkubwa kutoka kwa makada wake wenye mrengo tofauti na mwenendo wa chama hicho kwa sasa, kutokana na kile wanachosema ni chama kukiuka misingi ya waasisi.

Kauli ya Nape
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye alipotakiwa kuzungumzia hoja za makada hao alijibu kwa kifupi," No comment." (sina cha kusema)

 
Doa moja ni huyu Kitine, nakumbuka wakati akiwa Mbunge Mkewe alipata upendeleo na Wizara ya Afya wakati Ule kupelekwa nje kutibiwa, kama sikosei walipewa fedha taslimu za matibabu walizoomba na zilikuwa ni nyingi zaidi ya matibabu au walienda hospitali ghali zaidi ya waliyoomba; Kifupi waliilaghai serikali maskini ya Tanganyika na Zanzibar

Sasa Anazungumzia Ufisadi? Nakumbuka Jina lake halikurudi kwa kugombea Ubunge ndani ya CCM...
Alianza kuwageuka waliomshibisha...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom