Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,777
- 2,392
Lakini mkuu hawa wazee are on record kwa kukumea ufisadi na mafisadi wa waziwazi ndani ya chama tawala.Hili zigo la ufisadi uliasisiwa na kundi la wanamtandao, kundi ambalo hadi leo linatamba serikalini na kwenye chama.Hao wazee wangekuwa watabiri wangeyanena hayo mapema sio wakati huu. Hapa wameona hali halisi ambayo haihitaji hata elimu ya kayumba school kuelewa anguko la ccm. Hakuna jipya walo liona ni mlolongo tu wa mambo, matukio, kasoro, makundi, ujinga, owongo, wizi, giriba nk ndani ya ccm na ukomavu wa upinzani hasa chadema.
Wazee maarufu ndani ya Chama cha Mapinduzi, Dr Hassy Kitine,Mzee Ibrahim Kaduma na Mzee Joseph Butiku wametoa ya mwaka walipokuwa wakihojiwa katika luninga Channel 10, jumamosi.
Habari hii imejirudia katika gazeti la Mwananchi leo(Machi ,26, 2012) ikisema:
"Na Elias Msuya,
Makada watatu wakongwe wa Chama cha Mapinduzi( CCM), Ibrahim Kaduma,Dk Hassy Kitine na Joseph Butiku wameibuka na kukutabiria anguko chama hicho tawala kwa kile walichosema, kwenda kinyume na misingi ya kuasisiwa kwake.
Kauili za makada hao maarufu, zinakuja kipindi ambacho upepo wa kisiasa umekuwa ukivuma vibaya ndani ya chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika, kutokana na vita ya makundi kati ya watuhumiwa wa ufisadi na wale wanaojipambanua kwamba ni wazalendo na wapinga."
Maoni Yangu:
Asiyesikia la mkuu huvunjika guu!
Siku hizi kuna sera inaitwa FITNA ndani ya siasa za bongo, hili nina uhakika litafanyika.Subiri uone watakavyo chafuliwa hawa watu.
Wazee maarufu ndani ya Chama cha Mapinduzi, Dr Hassy Kitine,Mzee Ibrahim Kaduma na Mzee Joseph Butiku wametoa ya mwaka walipokuwa wakihojiwa katika luninga Channel 10, jumamosi.
Habari hii imejirudia katika gazeti la Mwananchi leo(Machi ,26, 2012) ikisema:
"Na Elias Msuya,
Makada watatu wakongwe wa Chama cha Mapinduzi( CCM), Ibrahim Kaduma,Dk Hassy Kitine na Joseph Butiku wameibuka na kukutabiria anguko chama hicho tawala kwa kile walichosema, kwenda kinyume na misingi ya kuasisiwa kwake.
Kauili za makada hao maarufu, zinakuja kipindi ambacho upepo wa kisiasa umekuwa ukivuma vibaya ndani ya chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika, kutokana na vita ya makundi kati ya watuhumiwa wa ufisadi na wale wanaojipambanua kwamba ni wazalendo na wapinga."
Maoni Yangu:
Asiyesikia la mkuu huvunjika guu!
Lakini mkuu hawa wazee are on record kwa kukumea ufisadi na mafisadi wa waziwazi ndani ya chama tawala.Hili zigo la ufisadi uliasisiwa na kundi la wanamtandao, kundi ambalo hadi leo linatamba serikalini na kwenye chama.
Mkuu LG,
Huitaji utabiri wa wazee wa CCM kujua CCM inaelekea wapi akili za kawaida kabisa zinatosha kubaiani chama kikongwe bara Afrika kina karibia kujizika chenyewe kama kambare anapobaiani msimu wa kiangazi umekaribia.
Ukitazama kampeni za CCM kuanzia Igunga na Arumeru unabaini jambo moja muhimu sana CCM imeacha misingi mikuu ya kuanzishwa kwake [Chama cha wakulima na wafanyakazi] CCM imegeuka kimekuwa chama cha matajiri na wezi wa rasilimali za taifa.CCM imeacha msingi wake mkuu wa kuwatetea wanyonge,imeacha kulinda rasilimali za taifa,inakumbatia wezi,sera zake hazitekelezwi,rushwa inapingwa majukwaani lakini nyuma ya pazia inapaliliwa,inawekewa mbolea na kuvunwa kwa ustadi mkubwa.
Kwakuwa CCM haina sera na hili limejitokeza katika chaguzi za Igunga Hijjab ikachukua nafasi kubwa badala ya kuufahamisha umma wa Igunga nchi inakwenda wapi,mafanikio yaliyofikiwa na changamoto zake,Arumeru CCM imekujua na sera za washili hawamtaki mgombea wa chama cha upinzani hawana kitu cha kuwaambia wapiga kura wa Arumeru wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa ardhi kwakuwa wanajua wanahusika kwa asilimia zote kuiuza ardhi kwa wawekezaji uchwara na kuwaacha wananchi bila ardhi.
Hii si ile CCM ya Nyerere iliyokuwa ikiwasemea wanyonge,wakulima na wafanyakazi hii ni CCM ya Kikwete,Mkapa na Mwinyi inawasemea wawekezaji wanaopora madini yetu,wanaopora ardhi yetu,wanaopora ajira zetu.CCM ya leo inazalisha ajira kwa kuongeza idadi ya mikoa na wilaya haina habari na viwanda !.Hii ni CCM ya washili na Hijabu,hii ni CCM ya Wasira na genge la wahuni hawana uchungu na umasikini wa watanzania,hawawezi kutueleza baada ya miaka 50 ya uhuru wamefanikiwa kupunguza umasikini vijijini kwa asilimia ngapi !.Rwanda ya Kagame baada ya mapigano ya muda mrefu inapiga hatua kubwa utashangaa haina rasilimali nyingi ukilingalisha na Tanzania.
Mkuu,Nakubaliana na wewe Mkuu kwa hii observation ambayo ni critical.
Lakini, mie najiuliza kila siku, hivi CCM yenyewe haijioni kuwa inachungulia kaburi?
Maana imeanza kukosa sifa za kuwa chama kinachomilikiwa na wananchi wenyewe na kwa ajili yao.
Huwezi kusafisha tope kwenye bwawa ukiwa ndani ya bwawa. Hawa wazee kama sio wanafiki, wazandiki, wafitini,. Waoga, wambea na wasaliti, wangeamua maamuzi mazito ya kusimamia maadili, malengo, katiba na kanuni za ccm ambazo ni nzuri sana. Hawa wazee baadhi wanatumia uozo wa ccm kulinda maslai na utajiri wao walopatia ndani ya ccm. Ukitoa mzee Butiku nani asiyejua utajiri na ukaribu wa hao walo baki na rais alo asisi ufisadi ndg Mkapa? Ndg yangu hakuna jipya wanajilinda tu na wakienda kwa jk wanamsifia tu. Nini sasa?
Nakubaliana na wewe Mkuu kwa hii observation ambayo ni critical.
Lakini, mie najiuliza kila siku, hivi CCM yenyewe haijioni kuwa inachungulia kaburi?
Maana imeanza kukosa sifa za kuwa chama kinachomilikiwa na wananchi wenyewe na kwa ajili yao.
Msema ukweli ni kipenzi cha Mungu.