Wazee wa Utemi wa Wanyanyembe Tabora Wamkataa Lowassa

Wazee wa Utemi wa Wanyanyembe Tabora Wamkataa Lowassa

Mmh,mpaka kufikia October,2015 tutaona na kusikia mengi..tuombe uhai!
 
Wanyamwezi ni Wabantu na Wabantu walitokea huko Cameroon na Africa ya Kati/Congo.

Haiwezekani kuwa Wangoni walitangulia kufika Tanganyika kwa sababu Wangoni nao ni Wabantu. Ina maana tuliondoka nao huko Magharibi na sisi tulipofika Tanganyika, tukaona inatosha na wenyewe wakaendelea kwenda chini hadi Kusini. Ila wakati wa Mfalme Chaka Zulu, Ngoni au Nguni wengi walikimbia kutoka Kusini na kuanza kupanda juu. Wengine waliishia nchi za jirani na wengine wakaja hadi Songea. Ndiyo maana vita vya Majimaji, Wangoni wa Malawi, Zambia na Msumbiji, walikuja kuwasaidia wenzao wa Tanganyika.

Wengine walianza kupanda juu zaidi hadi wakafika Tabora ila kufika Tabora, wakakutana na Mtemi Mirambo ambaye aliwapa kichapo hadi wakakubali kuacha Vita. Ila Mirambo akafurahia sana ujuzi wao wa kupigana na akawa anawaajiri kama Askari wake wa Kukodiwa na akawaita Walugaluga (jina limekaa kimatusimatusi).

Huko Senegal kuna kundi jingine kabisa la Kabila ambalo hatuna uhusiano nalo. Wengi inaaminika wanatokea Egypt yaani ile Egypt ya ukweli. Na ndiyo maana nchi kama Mali, kuna kabila linaloitwa Dogoni, wanafahamu sana mambo ya Sayari na nyota za ulimwengu huu. Jambo hilo lina uhusiano sana na Pyramid za Egypt na Latin America/Asia. Pia kuna majina ambayo walikuta yameandikwa kwenye hizo Pyramid, hayo Majina yapo West Africa.
pamoja na historia nzuri ya kutoka iwe senegal au cameroon, lakini maendeleo ya mkoa huo na majirani zake na katika utawala haya onyeshi huo umahiri wa wa senegal/cameroon zaidi ya kuwa bendera ufuata upepo. hata vyama vya ushirika siku hizi hamna watu walio bora mpaka watoke serikali.
 
Katika gazeti la Raia Mwema uk 17 kuna press release ambapo wakuu wa utemi wa Wanyanyembe Tabora wamelaani kitendo batili cha kisanii cha kumfanyia tambiko Mh Lowassa bila ridhaa ya ukoo wa utemi wa Unyanyembe. Mahali paliponichekesha kwenye hiyo press release ni hapa:

" Haiingii akilini, jiwe la msingi la kumbukumbu ya Mtemi shujaa Issike Mwanakiyungi, heshima hiyo apewe Mh Lowassa wakati Mtemi Issike aliishi na kujiua kwa kukataa ufisadi na udhalimu wa Wakoloni wa Kijerumani".

Vita hiyo ya Lowassa na Samweli Sitta!
Baada ya kula,kushiba,haja kubwa ndo wanamtosa?! He wanyamwezi kweli mmekithiri kwa utaperi,Lowasa hashkiki hata kwa superglue.
 
Hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha
 
Makanisani na nyie muamke na msikimbilie tu mihela anayotoa angalieni ni waTz wangapi alowadhulumu na kuzileta kanisani na je Mungu anapenda?

Anadhulumu kupitia wizara ama taasisi gani?Kiasi gani anadhulumu?Usiniambie Richmond kwani hiyo ndiyo tegemeo la mkakati wa'power Africa'.Zaidi ya hapo,ni wapi pengine unadhani amekuibia?Tuwe wakweli na kuacha kuimba fitina za madaraka alizozianzisha Sitta zinazoonekana kukolezwa na itikadi za kidini!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ingawa Chemistry na Biology zina uhusiano, bado ni vitu tofauti. Hata sijui umeandika nini... Samahani.
pamoja na historia nzuri ya kutoka iwe senegal au cameroon, lakini maendeleo ya mkoa huo na majirani zake na katika utawala haya onyeshi huo umahiri wa wa senegal/cameroon zaidi ya kuwa bendera ufuata upepo. hata vyama vya ushirika siku hizi hamna watu walio bora mpaka watoke serikali.
 
Back
Top Bottom